Kesi ya Said Ali Biyad: Msomali aliyeiangamiza familia yake nchini Marekani…! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Said Ali Biyad: Msomali aliyeiangamiza familia yake nchini Marekani…!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Oct 5, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Said Ali Biyad
  [​IMG]
  [​IMG]
  Said Biyad akifikishwa mahakamani....
  [​IMG]
  Mkewe Fatuma Amir akitoa ushahidi mahakamani

  [​IMG]
  Wakili wa mshitakiwa Mike Lemke akitoa majumuisho ya utetezi wake....

  Ilikuwa ni siku ya Ijumaa ya oktoba 6, 2006 majira ya asubuhi, mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Said Ali Biyad aliyekuwa na umri wa miaka 49 raia wa Somalia ambaye alikuwa ni mkimbizi aliyekuwa akiishi nchini Marekani, alikwenda katika makao makuu ya Polisi ya Louisville Metro yaliyoko katika mji wa Oregon jimboni Kentucky nchini Marekani na kumweleza askari mmoja wa upelelezi kwamba ameua familia yake.

  Akiongea kwa utulivu kwa kiingereza chake kibovu chenye lafudhi ya Kisomali huku akiwa amekunja mikono kifuani alimweleza askari huyo kwamba amemnyonga mkewe aliyemtaja kwa jina la Fatuma Amir 29, na kuwachinja watoto wake wanne, Sidi aliyekuwa na umri wa miaka 8, Fatuma aliyekuwa na miaka 7, Khadija aliyekuwa na miaka 4, na Goshany aliyekuwa na miaka 2.Akiongea kwa kiingereza chake kibovu Biyad aliendelea kusema, "Nililia na kwenda kuosha mikono yangu jikoni. Nilijisemea moyoni, nimefanya nini sasa? Ni wapi natakiwa kwenda sasa? Hata sijui ni nini kimetokea……."

  Aliendelea kumweleza yule askari wa upelelezi….

  "Naomba uniweke chini ya ulinzi, si haki kabisa, nimefanya jambo baya sana….si haki kabisa….."Awali Mpelelezi huyo wa Polisi alidhani kwamba Biyad alikuwa ni mwendawazimu, kwani kutokana na lugha ya kiingereza kumpa shida, lakini hata kujieleza kwake na muonekano wake ulikuwa ni wa kutiliwa mashaka kwa sababu nywele zake zilikuwa zimejisokota kama vile mtu anayetaka kufuga rasta.

  Askari huyo wa upelelezi kwa kutumia simu ya upepo (radio call) aliwajulisha askari wa doria na kuwaelekeza waende katika nyumba iliyotajwa na mtuhumiwa ili kuthibitisha madai yake….. "Niko hapa na huyo mtu, anadai kwamba ameua mke na watoto wake wanne, lakini siamini kama anasema kweli na ninadhani hii itakuwa ni kesi ya kitengo cha CIT" alisema askari huyo wa upelelzi akiongea na askari wenzie wa doria (CIT ni kitengo cha polisi kinachojihusisha na matukio ya watu wenye matatizo ya akili nchini humo).

  Lakini baada askari hao wa doria kufika katika nyumba hiyo, walipokelewa na hali ya kutisha, kwani nyumba yote ilitapakaa damu. Askari hao wa doria walikuta watoto watatu wakiwa wamekufa kwa kuchinjwa huku mtoto mmoja mdogo akiwa ameweka dole gumba mdomoni kabla hajafa. Mtoto mwingine alikutwa akiwa kwenye chumba kingine akiwa amekufa na akiwa amefunikwa kwa blanket. Bahati nzuri mkewe alikutwa chumba kingine akiwa amejeruhiwa kwa nyundo kichwani na kupoteza fahamu. Alikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

  Historia inaonyesha kwamba Fatuma Amir aliolewa na Said Ali Biyad akiwa na umri wa miaka 13. Walikuwa wakiishi kwa amani hadi mwaka 1991 yalipotokea mapigano ya kikabila nchini Somalia ndipo wakakimbilia nchini Kenya ambapo baadae mwaka 2004 waliondoka na kuhamia nchini Marekani ili kutafuta hifadhi kutokana na machafuko yaliyoikumba nchi yao kutoonyesha dalili ya kumalizka.Said Biyad na familia yake alikuwa ni miongoni mwa Wasomali 12,500 waliokimbilia nchini Marekani na kutawanyika katika miji 50 iliyoko katika majimbo 38 ambapo wakimbizi kati ya 600 mpaka 700 wanaishi katika mji huo wa Louisville. Awali walifikia katika mji wa Portland ambapo walianza kujifunza kiingereza huku wakitafuta kazi kwa ajili ya kujikimu. Baadae walihamia katika mji wa Oregon.

  Wakiwa hapo Oregon ndoa yao iliingia katika vurugu na hivyo Fatma aliamua kumkimbia mumewe na kuhamia katika mji wa Louisville akiwa na watoto wake wanne: Goshany, Khadija, Fatuma na Sidi Ali, ambao walikuwa na umri kati ya miaka 2 mpaka 8.

  "Ni jambo la kusikitisha sana kwa kile kilichotokea" alisema Abanur Saidi, mfanyakazi wa taasisi kujitolea ya Kanisa Katoliki inayowasaidia wakimbizi kujifunza kiingereza na kuwasaidia kutafuta makazi na kazi.

  Omar Eno, mkurugenzi wa National Somali Bantu Project katika mji huo wa Portland alisema kwamba wanandoa hao waliomba msaada kutoka katika taasisi yake ili wasaidiwe kujifunza kiingereza na kutafutiwa kazi. Wote kwa pamoja walimudu mapema kuijua lugha hiyo na walijumuika vyema na jamii ya wasomali waishio katika mji huo. Hata hivyo baadhi ya marafiki zao walidai kwamba wanandoa hao walikuwa na matatizo katika mahusiano yao.

  Basko Kante ambaye alikuwa kifanya kazi na Biyad katika bodi ya African Community Coalition katika mji huo wa Portland alisema kwamba, kuna wakati Biyad alikuwa anazungumzia matatizo katika ndoa yake lakini hakuwa anaeleza kwa undani juu matatizo hayo. Kante alisema kwamba, tofauti kubwa ya umri wao huenda ikawa ndio chanzo cha migogoro iliyoikumba ndoa yao. (Biyad alikuwa na umri wa miaka 42 na mkewe Fatma Amir alikuwa na umri wa miaka 29).

  "Alikuwa akisema mara kwa mara kwamba watu wanaingilia ndoa yake, watu wa kwao Somalia na watu wa nchini humo. Hata hivyo hapakuwa na taarifa za matukio ya kupigana" Alisema Kante.

  Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Polisi waliwahi kuitwa katika nyumba waliyokuwa wakiishi wanandoa hao hapo mnamo March 2005, ambapo ilidaiwa kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya wanandoa hao. Kwa mujibu wa ripoti ya Polisi, ilibainika kwamba, kulikuwa na kupishana kwa lugha kati ya wandoa hao ambapo ilisababisha Fatuma kunywa dawa ya kung'arishia (Bleach) na kukimbizwa hospialini. Hakuna mashitaka yoyote yaliyofunguliwa.

  Eno na Dana Van Lehman makamu wa taasisi ya National Somali Bantu Project, walisema kwamba, waliwahi kusikia kuhusu ugomvi wa mara kwa mara wa wanandoa hao, lakini hawakujua undani wa ugomi wao. "Kuna idadi ya kutosha ya ndoa na talaka katika jamii hiyo ya wakimbizi wa Kisomali." Alisema Van Lehman.

  Hata hivyo kutokana na ndoa yao kukumbwa na vurugu za mara kwa mara, Fatuma alikimbia pamoja na wanae. Mmoja wa rafiki wa familia hiyo Hassan Muya alisema kwamba, Portlanda umekuwa ni mji ambao si salama kwake kutokana na ndoa yake kukumbwa na migogoro isiyoisha. Fatuma alikimbilia katika mji wa Louisville ambapo aliungana na kaka yake aitwae Osman Noor.Kwa upande wa Biyad, aliwaeleza marafiki zake kwamba Mkewe Fatuma amemtoroka. "Alikuwa hajui alipokwenda yeye na watoto wake." Alisema Kente.

  "Ni baada ya miezi kadhaa ndipo Biyad alipoweza kumpata mkewe" aliendelea kusema Kente. Kente alisema kwamba Biyad hakumweleza namna alivyompata mkewe, lakini alikumbuka kumsikia akisema kwamba alitaka kuungana na familia yake huko Kentucky.

  Kwa hiyo Biyad alikuwa katika mji huo wa Louisville kwa majuma kadhaa kabla ya kuishambulia familia yake na kuuwa watoto wake wote kumbaka mkewe na kisha kumjeruhi kwa kumpiga kwa nyundo kichwani.Polisi waliamini kwamba, tukio hilo lilitotokea mkatika mtaa wa 1427 Bicknell ulitokana na mabishano kati ya wanandoa hao kuhusiana na watoto. Msemaji wa Polisi Luteni Kanali Phillip Turner alisema kwamba, wanandoa hao walikuwa na ugomvi lakini ilikuwa haijulikani kama Biyad alikuwa kiishi na familia hiyo au la.

  Siku hiyo umati wa jamii ya Wasomali na wenyeji mji huo walikuwa wamekusanyika nje ya nyumba hiyo huku wakiwa na nyuso za huzuni wakiwaangalia askari wa upelelezi na wataalamu wa kukusanya ushahidi wakiwa wameizingira nyumba hiyo.

  "Hili ni tukio ambalo halijawahi kutokea." Alisema Hassana Muya raisi wa Bantu Community Association. "Hatujawahi kuona mtu akiuwa familia yake mwenyewe." Aliendelea kusema Hassan Muya.

  Moja ya mambo yaliyoitatiza jamii ya Kisomali iishiyo katika eneo hilo ni kuhusiana na mazishi ya watoto hao. Kwa mujibu wa taratibu za kiislamu inatakiwa mtu aliyekufa kuzikwa ndani ya saa 24, lakini kutokana na miili ya watoto hao kufanyiwa uchunguzi hakujuliakana kama jambo hilo lingewezekana.

  "Wanachotaka kufanya, sicho tunachotaka kufanya. Ni vigumu." Alisema Hassan Muya.
  Naye Omar Ayyash Mkurugenzi wa Metro International Affairs alisema kwamba, alijaribu kuwasiliana na maafisa wa mamlaka ya kisheria nchini humo ili wasaidie kuharakisha utaratibu mzima wa kuchunguza miili ya marehemu hao ili waweze kukidhi matakwa ya dini yao ya Kiislamu inayotaka marehemu hao wazikwe ndani ya saa 24.

  "Tuko makini sana na matakwa ya mila na desturi zetu." Alisema Ayyash.Mmoja wa watu waliokuwa wakifuatilia kwa karibu mwennendo mzima wa shughuli ya kukusanya ushahidi na uchunguzi wa miili ya marehemu hao alikuwa ni kaka yake na Mke wa Biyad Bi, Fatuma Amir, aitwae Osman Noor.

  Noor alisema kwamba alipata simu jana asubuhi kutoka kwa shangazi yake, ambaye alipigiwa simu na Fatuma na kuelezwa juu ya shambulio hilo lililofanywa na mumewe. Noor ambaye anaishi eneo la Park Hill Public Housing Complex alikwenda haraka katika eneo la tukio, lakini wakati anafika akakuta dada yake amekwishakimbizwa hospitalini, lakini alijulishwa kwamba watoto wote wameuawa.

  "walikuwa ni watoto wazuri sana, nitawakumbuka sana." Alisema NoorNoor alisema kwamba, Biyad alikuwa ni mtu mzuri sana aliyekuwa akiipenda familia yake, lakini hajui ni kitu gani kimemtokea.

  Kesi hiyo ilibidi isubiri kwa takriban miaka minne na nusu ili kuanza kusikilizwa. Hiyo ilitokana na uchunguzi wa akili ya mtuhumiwa na pia swala la ugumu wa mtuhumiwa kutoelewa lugha ya kiingereza kwa ufasaha.

  Biyad aliwekwa ndani kuanzia hiyo Octoba 6, 2006 bila uwezekano wa kuachiwa kwa dhamana, wakati aikisubiri kusikilizwa kwa kesi yake.

  Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mapema lakini ilisimama kusikilizwa mnamo January 27, 2010 na kusogezwa hadi hapo mnamo April 18, 2010 ili kupisha uchunguzi zaidi wa akili ya mtuhumiwa kabla ya kuanza kusikilizwa tena rasmi.

  Sababu ya kusogezwa kwa kesi hiyo ni kutokana na hali ya mtuhumiwa kiakili kuonekana kuwa na dosari kubwa. Akiwa hapo Mahakamani Biyad alikuwa mtulivu huku akiwa amezungukwa na wakalimani wawili. Pale mahakamani ilielezwa kwamba Biyad alikwenda kuitembelea familia yake na ndipo alipogundua kwamba mkewe anayo ndoa nyingine ya siri, jambo hilo lilimkera sana Biyad kwani alikuwa anaamini kwamba familia ile ni mali yake…

  Kwa mujibu wa maelezo ya Polisi ilidaiwa kwamba, Biyad aliwaeleza askari wa upelelezi kwamba, alimlazimisha mkewe kufanya naye mapenzi na baada ya kumaliza alimpiga na nyundo kichwani mara mbili ambapo alipoteza fahamu. Baada ya mkewe kurudiwa na fahamu, Biyad alimkabili na kisu akitaka kumchoma nacho, lakini mkewe alimudu kukimbia na kujifungia katika chumba kingine.

  Hapo ndipo inapodaiwa Biyad kuwauwa watoto wake wanne kwa kuwachinja. Wawili walikuwa chumbani na wawili walikuwa jikoni. Gail Norris msaidizi wa mchunguzi wa maiti katika ofisi ya uchunguzi wa maiti ya mkoa ya Jefferson Medical Examiner katika ripoti yake alidai kwamba watoto wote walichinjwa kwa kisu na ilionyesha kwamba wale watoto wakubwa walikabiliana na baba yao kabla ya kuuawa, kwani walikuwa na majeraha ya kukatwa na kisu katika mikono yao.

  Mkewe Fatuma Amir akitoa ushahidi wake hapo mahakamani alidai kwamba mumewe alikuwa ni mkorofi kila arudipo kutoka kazini, alikuwa na kawaida ya mkupiga na kumbaka. Biyad akijitetea pale mahakamani alimwambia Mheshimiwa Jaji James Shake kwamba, siku ya tukio hilo, watu watatu walivamia nyumbani kwake n akumshikilia kama mateka ambapo walimtaka awape dola milioni kumi. "Sijawahi kumbaka mke wangu wala kumpiga hata siku moja" alisema Biyad akijitetea.

  "Waliniambia, unataka kinywaji? Na ndipo waliponipa soda na ninadhani ile soda ilikuwa imewekwa kitu lakini sikujua ni kitu gani, na nilipokunywa ile soda nilipatwa na vurugu kichwani ambazo hazikuwa na kawaida, nilihisi kama kichwa change kinataka kulipuka… nilibadilika moja kw moja na sikujua kilicoendelea kuanzia hapo….." Alisema Biyad akijitetea.

  Aliendelea kusema kwamba, wakati anamweleza mkewe juu ya watu hao na madai yao ya kutaka fedha ndipo walipoanza kubishana, na hatimaye wale watu waliwauwa watoto wake wote.

  "Mke wangu alianza kunifokea na kuninyooshea vidole…" Alisema Biyad kupitia kwa mkalimani wake. "Wakati mimi na mke wangu tukiendelea kubishana, wale watu walienda vyumbani ambapo watoto wetu walikuwa wamelala. Waliaanza… unasikia.. kuwadhuru kwa kuwakata shingoni…" Alisema Biyad

  Aliendelea kusema kwamba alifuatana na mmoja wa watu hao hadi makao makuu ya Polisi."Kabla sijaingia katika kituo hicho cha polisi, mtu huyo aliniambia, ‘hey, usije ukasema lolote kuhusu sisi. Katu usije ukasema jambo lolote kuhusu sisi la sivyo tutakuuwa. Ninafanya kazi serikalini. Unanijua mimi. Mimi ni FBI?'"

  Hata hivyo Polisi walikuwa na maelezo tofauti na walicheza mkanda waliorekodi maelezo ya Biyad wakati alipofika Polisi na kudai kuwa ameua familia yake. Biyada alikataa kuwa yale sio malezo yake na alipinga kuwa ile haikuwa sauti yake. "Nadhani wametengeneza huo mkanda, hiyo sio sauti yangu kabisa.." Biyad alisema kupitia mkalimani wake.

  Mwanasheria aliyekuwa akimtetea Biyad, wakati wa kufunga utetezi wake alisema kwamba, ingawa mteja wake anakanusha kuhusika na mauaji hayo, lakini kuna uwezekano kuwa ni yeye aliyehusika, hata hivyo kwa mijibu wa vipimo vya hospitalini inaonyesha kwamba mtuhumiwa anayo matatizo ya akili kwa takriban mwaka mzima kabla ya tukio hilo na hakuwa na uwezo wa kudhibiti vitendo vyake vya kuvunja sheria.

  "Kilichowatokea wale watoto wanne siku ile ya Octoba 6, 2006, inaweza kuelezewa kama ni kitendo kilichofanywa na mtu asiye na akili timamu" Alisema mwanasheria aliyekuwa akimtetea aitwae Ray Clooney.

  Mwanasheria mwingine aliyekuwa akimtetea aitwae Mike Lemke alidai kwamba, wanamini kuwa Biyad anayo matatizo ya kiakili na kwa mujibu wa wataalamu wa akili walithibitisha kwamba Biyad alikuwa na matatizo ya schizophrenic.

  Lemke aliendelea kusema kwamba, Biyad kwa miaka minne alikuwa anaamini kwamba, watu walikuwa wanataka kumuuwa na kuchukuwa fedha zake, na alikuwa anaamini kuwa yeye ni Bilionea na ni mtu maarufu.

  Walimuomba Mheshimiwa Jaji Shake kumuona Biyad kutokuwa na hatia kwa kosa hilo kwa sababu ana matatizo ya akili. Mwanasheria wa serikali alisisitiza kwamba Biyad alikiri mwenyewe mbele ya Polisi kwamba ni yeye aliyehusika na mauaji hayo. Hapo mnamo June 7, 2011, Mheshimiwa Jaji James Shake alimhukumu Saidi Biyad kifungo cha maisha bila uwezekano wa kifungo cha nje.

  Akihitimisha hukumu yake Mheshimiwa Jaji Shake alisema, "kwa miaka 18 niliyokaa katika kiti hiki sijawahi kushuhudia kesi ya mauaji ya kikatili kama hii…."

  Mkewe ambaye hakuwepo mahakamani siku ya hukumu hiyo akizungumzia hukumu hiyo, alisema kwamba ni vyema akafungwa maisha na kuozea jela

  Hata hivyo Lemke alisema kwamba atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mtambuzi at it again....thanks a lot for sharing.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Ila jamaa anaonekana kama hana network na mwili na akili yake!
   
 4. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,292
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nilipoiona tu picha yake ya kwanza nikajua huyu lazima atakuwa MWENDAWAZIMU, tunaweza kushangaa aliwezaje kuwaua watoto wake kikatili namna hiyo?? Si mnajua hawa muslims wao kuua ni kama kwenda msalalani tu, kama wale akina BOKO HARAM, AL SHABIBI, AL QAEDA, UAMSHO, etc. Cha msingi ni kuwaombea watoto wale mungu aendelee kuwakumbatia.
   
 5. lukatony

  lukatony JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hakika kuna mengi yaliyojificha kwenye kesi hii!!!!!!sijakubaliana na hukumu na uchunguz wa kesi hii,but nashukuru nimejifunza kitu!!!!!!
   
 6. Rashdind

  Rashdind Senior Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  i
  inasikitisha ila jamaa ni zaid ya wale waarabu wanaojitoa muhanga anaweza kuan na homon za simba uyo sio bure.
   
 7. Paloma

  Paloma JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 22, 2008
  Messages: 5,341
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mhhhh sooo touching jamani............
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu Rashdind nashukuru kwa kutoa maoni yako kwenye posti hii, lakini nakuomba ufanye editing na kuondoa hiyo quote, kwani unawapa shida wanaosoma kwa kutumia simu...

  nakuomba sana mkuu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. waza_makubwa

  waza_makubwa Senior Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  inasikitisha
   
 10. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Inaonekana kabisa jamaa alikuwa ni mwendawazimu, lakini hiyo hukumu alistahili.
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Wala hakuwa na sababu ya ku-quote habari yote hiyo.....
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Laiti angejua kero aliyoisababisha kwenye post hii asingefanya hivyo alivyofanya.......................
   
 13. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  dah aisee too sad ...hivyo vitoto ....nafikiria vya kwangu?
   
 14. lutayega

  lutayega JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 29, 2012
  Messages: 1,215
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hata mwenye matatizo ya akili sio rahisi kufanya unyama wa nana hii pekeyake mi nadhani huyu jamaa alishirikiana na watu wengine ambao walimchanganya kwa madawa ya kulevya kupitia kwenye soda km ye anavyosema. Inasikitisha sn
   
 15. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii kesi inaumiza kwa kweli! dha!, Wanadamu tumekuwa na roho ya kikatili zaidi ya wanyama, OOOO Mwenyezi Mungu tunusuru.
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Duh tangu nikiwa kinda mpaka leo sijui ni kwanini si imani na waSomali,hawa jamaa ni mwisho wa matatizo ukikutana na waSomali mia tisini na tisa ni vichaa bila shaka Said Ali Biyad ni mmoja wao.Unakumbuka kituko cha Rage na bastola katika mkutano wa kampeni Igunga,sakata la Bashe na Kigwangallah kutishiana bastola bado sijaenda kwa wale wafanyabishara wa kisomali Dar.

  Naunga mkono adhabu ya kifo Biyad hastahili kuishi.
   
 17. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Tumwamini nani jamani wale tunao waamini na kuwaona ndio walinzi wetu na ndi wanaotufanyia ukatiri wa hali yajuu
  Kwa kweli inaumiza sana.

  Wivu wake kwa mke anaishia kuangamiza watoto wasiokuwa na hatia kabisa.

  Kwakweli hawa wanaume na ukatiri huu ni zaidi ya ubinafsi, faida iko wapi.
  Inafanana sana na ya huyo mkenya aliye waua watoto wake wanne juzijuzi.
  Hapo mtu unajiuliza usalama wa watoto uko wapi wanapokuwa mikononi mwa wazazi wao.

  Thans Mtambuzi
   
 18. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Asante bro.....
   
 19. S

  Safhat JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah mackini watoto hao hawana hatia wamekufa kinyama km ivo!kwa kwel byad anastahili kuny...!
   
 20. manumbu1

  manumbu1 JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 572
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kwa taarifa yako mu uwaji no mziguwa
   
Loading...