Kesi ya Sabaya: Shahidi wa tatu aeleza Sabaya alivyomtoa 'Lock' kwa kipigo na kumpora

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
667
1,000
Shahidi wa tatu katika kesi ya Unyang'anyi wa kutumia Silaha inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Ramadhani Rashid (26) maarufu kwa jina la Anas ameieleza mahakama namna alivyopigwa na Sabaya na Kuporwa simu ya mkononi na fedha kiasi cha sh, 35,000.

Akitoa ushahidi katika mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi , Odira Amworo ,Anas ambaye ni mfanyabiashara mdogo (Machinga).

Katika soko la Kilombero jijini Arusha, alisema siku ya tukio Februari 9 mwaka huu alipigwa na kuporwa katika duka liitwalo Shaahid Store baada ya kwenda kununua bidhaa.

Huku akiongozwa na wakili wa Serikali ,Baraka Mgaya shahidi huyo ambaye alimtambua Sabaya kwa kumshika bega mahakamani alisema siku ya tukio alifika katika duka hilo kununua chandarua lakini alikuta lango la duka likiwa limerudishiwa ila alifanikiwa kuingia ndani na kukuta watu wamelala chini wakiwa chini ya ulinzi.

Alisema watu wawili walimfuata na kumuuliza amefuata nini hapo na alipoangalia pembeni aliona wahudumu waduka wakiwa wamelala chini huku anayepokea pesa kaunta akiwa anatoka damu puani.

Anas alidai kwamba Sabaya alitoa amri kwa wasaidizi wake hao wamtoe "Lock'

ambapo mmoja ya watu hao alianza kumpiga Makofi ya mikono miwili masikioni na baadaye kumpekuwa mfukoni na Kumpora kiasi cha sh,35,000 , simu ya mkononi aina ya Tecno pop 1 na karatasi aliyokuwa ameorodhesha bidhaa za kununua na kumwamuru kulala chini kifudifudi.

Shahidi huyo akiwa amelazwa chini alimsikia Sabaya akimhoji mhudumu wa duka kwa nini huwa hatoi risiti ,hata hivyo mhudumu wa duka alimjibu kwamba huwa wanatoa risiti lakini wakati huo alikuwa akiendelea kumpiga na kumlazimisha aseme kuwa huwa hawatoi risiti.

Alisema alisikia mhudumu wa duka akikubali kuwa kweli hawatoi risiti ndipo Sabaya alipomwamuru msaidizi wake amrekodi kupitia simu ya mkononi wakati akikiri kuwa huwa hawatoi risiti kwa wateja wao.

Shahidi alidai kwamba Sabaya aliendelea kumhoji mhudumu wa duka kuwa kwanini wanafanya biashara ya kubadilisha dola huku akimwambia ampigie simu mmiliki wa duka ili afike dukani kwake.

Alisema akiwa chini amelala alijaribu kuinua Kichwa lakini alipigwa kibao na kukandamizwa chini,hata hivyo alimsikia mtu mmoja akiingia dukani na baadaye alitambua sauti kuwa ni mdogo wake na Mmiliki wa duka aitwaye Hajirin Saad.

Anas aliendelea kusema kwamba Sabaya alimhoji Hajirin kwanini wanafanya biashara na hawatoi risti ambapo alimjibu kwamba hilo duka si Mali yake na alifika hapo kujua nini kilichotokea.

Aliieleza mahakama kwamba baadaye katika duka hilo aliingia diwani Bakari Msangi ambaye alisikia alimsalimia Sabaya lakini Sabaya hakuitikia badala yake alimuiliza Umefuata nini hapa.

Alisema alimsikia Bakari naye akimuuliza Sabaya kuwa yeye ni mkuu wa wilaya ya Hai kitu gani kimemleta Arusha wakati Kuna mkuu wa wilaya ,TRA na wengine.

Shahidi alisema baada ya maswali hayo Sabaya alitoa amri kwa wasaidizi wake kwa kuwataka wamtoe 'wenge' ambao walimpiga Bakari vibao vya mkupuo wa mikono miwili masikioni.

Alisema baadaye Sabaya alimtaka Anas atoke nje na atokomee lakini wakati alitoka nje akiwa mlangoni alikumbuka simu yake na fedha zilichukuliwa alijaribu kwenda kuzidai lakini Sabaya aliamrisha atolewe 'Loku' kwa kupigwa tena vibao na kutakiwa kuondoka.

Hata hivyo wakili wa Serikali alimtaka shahidi kumtambua mshtakiwa mahakamni hapo ,ambapo Shahidi alienda kizimbani na kumgusa bega la kushoto Sabaya aliyekuwa amekaa na washtakiwa wenzake wawili Silvester Nyegu na Daniel Mbura.

Kesi hiyo inatarajia kuendelea siku ya jumatatu kwa mashahidi kuendelea kuthibitisha mashtaka .

Ends....

Vesuvius

JF-Expert Member
Jun 27, 2021
330
500
Dadekiii watu hawana hamu na Sabaya tena (zawadi ya Idd kutoka kwa mama) wako na hashtag tu za mbowe sio gaidi..uzi hauna wachangiaji...nyie jameni..hii tz ni fyoko sana.
 
  • Thanks
Reactions: cmp

nsibirwaha

Member
Jun 10, 2021
57
125
halafu kuna wanasema huyu alikuwa Mtetezi wa wanyonge na kusema anaonewa!!!tulio Arusha tunajua uhuni na ujambazi wa huyu dogo Sabaya,anavuna alichopanda
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,687
2,000
Aliieleza mahakama kwamba baadaye katika duka hilo aliingia diwani Bakari Msangi ambaye alisikia alimsalimia Sabaya lakini Sabaya hakuitikia badala yake alimuiliza Umefuata nini hapa.

Alisema alimsikia Bakari naye akimuuliza Sabaya kuwa yeye ni mkuu wa wilaya ya Hai kitu gani kimemleta Arusha wakati Kuna mkuu wa wilaya ,TRA na wengine.

Shahidi alisema baada ya maswali hayo Sabaya alitoa amri kwa wasaidizi wake kwa kuwataka wamtoe 'wenge' ambao walimpiga Bakari vibao vya mkupuo wa mikono miwili masikioni.
Watahoji: ulionaje akipigwa kwa mikono miwili wakati ulikuwa umelala kifudifudi?
 
Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,556
2,000
Shahidi wa tatu katika kesi ya Unyang'anyi wa kutumia Silaha inayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai,Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, Ramadhani Rashid (26) maarufu kwa jina la Anas ameieleza mahakama namna alivyopigwa na Sabaya na Kuporwa simu ya mkononi na fedha kiasi cha sh, 35,000.

Akitoa ushahidi katika mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi , Odira Amworo ,Anas ambaye ni mfanyabiashara mdogo(Machinga)

Katika soko la Kilombero jijini Arusha, alisema siku ya tukio Februari 9 mwaka huu alipigwa na kuporwa katika duka liitwalo Shaahid Store baada ya kwenda kununua bidhaa .

Huku akiongozwa na wakili wa Serikali ,Baraka Mgaya shahidi huyo ambaye alimtambua Sabaya kwa kumshika bega mahakamani alisema siku ya tukio alifika katika duka hilo kununua chandarua lakini alikuta lango la duka likiwa limerudishiwa ila alifanikiwa kuingia ndani na kukuta watu wamelala chini wakiwa chini ya ulinzi.

Alisema watu wawili walimfuata na kumuuliza amefuata nini hapo na alipoangalia pembeni aliona wahudumu waduka wakiwa wamelala chini huku anayepokea pesa kaunta akiwa anatoka damu puani.

Anas alidai kwamba Sabaya alitoa amri kwa wasaidizi wake hao wamtoe "Lock'

ambapo mmoja ya watu hao alianza kumpiga Makofi ya mikono miwili masikioni na baadaye kumpekuwa mfukoni na Kumpora kiasi cha sh,35,000 , simu ya mkononi aina ya Tecno pop 1 na karatasi aliyokuwa ameorodhesha bidhaa za kununua na kumwamuru kulala chini kifudifudi.

Shahidi huyo akiwa amelazwa chini alimsikia Sabaya akimhoji mhudumu wa duka kwa nini huwa hatoi risiti ,hata hivyo mhudumu wa duka alimjibu kwamba huwa wanatoa risiti lakini wakati huo alikuwa akiendelea kumpiga na kumlazimisha aseme kuwa huwa hawatoi risiti.

Alisema alisikia mhudumu wa duka akikubali kuwa kweli hawatoi risiti ndipo Sabaya alipomwamuru msaidizi wake amrekodi kupitia simu ya mkononi wakati akikiri kuwa huwa hawatoi risiti kwa wateja wao.

Shahidi alidai kwamba Sabaya aliendelea kumhoji mhudumu wa duka kuwa kwanini wanafanya biashara ya kubadilisha dola huku akimwambia ampigie simu mmiliki wa duka ili afike dukani kwake.

Alisema akiwa chini amelala alijaribu kuinua Kichwa lakini alipigwa kibao na kukandamizwa chini,hata hivyo alimsikia mtu mmoja akiingia dukani na baadaye alitambua sauti kuwa ni mdogo wake na Mmiliki wa duka aitwaye Hajirin Saad.

Anas aliendelea kusema kwamba Sabaya alimhoji Hajirin kwanini wanafanya biashara na hawatoi risti ambapo alimjibu kwamba hilo duka si Mali yake na alifika hapo kujua nini kilichotokea.

Aliieleza mahakama kwamba baadaye katika duka hilo aliingia diwani Bakari Msangi ambaye alisikia alimsalimia Sabaya lakini Sabaya hakuitikia badala yake alimuiliza Umefuata nini hapa.

Alisema alimsikia Bakari naye akimuuliza Sabaya kuwa yeye ni mkuu wa wilaya ya Hai kitu gani kimemleta Arusha wakati Kuna mkuu wa wilaya ,TRA na wengine.

Shahidi alisema baada ya maswali hayo Sabaya alitoa amri kwa wasaidizi wake kwa kuwataka wamtoe 'wenge' ambao walimpiga Bakari vibao vya mkupuo wa mikono miwili masikioni.

Alisema baadaye Sabaya alimtaka Anas atoke nje na atokomee lakini wakati alitoka nje akiwa mlangoni alikumbuka simu yake na fedha zilichukuliwa alijaribu kwenda kuzidai lakini Sabaya aliamrisha atolewe 'Loku' kwa kupigwa tena vibao na kutakiwa kuondoka.

Hata hivyo wakili wa Serikali alimtaka shahidi kumtambua mshtakiwa mahakamni hapo ,ambapo Shahidi alienda kizimbani na kumgusa bega la kushoto Sabaya aliyekuwa amekaa na washtakiwa wenzake wawili Silvester Nyegu na Daniel Mbura.

Kesi hiyo inatarajia kuendelea siku ya jumatatu kwa mashahidi kuendelea kuthibitisha mashtaka .

Ends....

View attachment 1864499
Duh!!!! Hatari sana! Tulikuwa na majambazi viongozi!!!!! Halafu watu wanamtetea!!!!! Na hawa walioumizwa? Nani atawatetea kama sheria haitawasikiliza na kuwatetea?
 
Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,556
2,000
Huyu Sabaya inaelekea alikuwa jambazi hata kabla hajapewa ukuu wa wilaya,huko alienda kuendeleza ujambazi wake tu ngoja nayeye wamtoe 'Lock' kwanza
Alikuwa na kesi ya kujifana usalama wa taifa. Kesi ilikufa baada ya mwendazake kumpa ukuu wa wilaya!!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom