Kesi ya Sabaya: Shahidi asema Mwenye duka alilazimishwa aseme hatoi risiti

GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,431
19,775
Screenshot_2021-07-26-09-27-01-1.png


Arusha. Shahidi wa tatu wa Jamhuri, Ramadhan Ayubu Rashid (26) ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, jinsi mwenye duka alivyolazimishwa aseme hatoi risiti na watu waliokuwa eneo hilo, huku akimtambua aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Shahidi huyo ambaye ni mfanyabiashara mdogo alikuwa akitoa ushahidi mbele ya hakimu mkazi mwandamizi Odira Amworo, huku Jamhuri ikiwakilishwa na Wakili wa Serikali mkuu Tumaini Kweka, Wakili mwandamizi Abdallah Chavula na Wakili wa Serikali Baraka Mgaya.
Juzi katika kesi hii tuliona sehemu ya mahojiano ya shahidi wa huyo wa tatu na wakili Mgaya. Sasa endelea.

Wakili: Duka unalifahamu linaitwaje?

Shahidi: Nje ya duka wameandika Shaahid Store

Wakili: Eeeh ukakuta milango imerudishiwa?

Shahidi: Huwa wakienda kuswali wanarudishia, kwa kuwa wanarudishia kila siku, nikanyanyua geti na kuingia kwa ajili ya kuchukua ile neti yangu, baada ya kuingia ukiwa machinga unachukua kitu unachotaka unaenda kaunta kulipia.

Wakili: Umeshachagua neti unayotaka nini kilitokea
Shahidi: Baada ya kuchukua neti yangu nilishangaa wamekuja watu wawili, mmoja akaniuliza umefuata nini hapa?

Wakili: Hao watu wawili waliokufuata walikuwa wa jinsia gani?

Shahidi: Jinsia ya kiume.

Wakili: Ilikuwa mara ya ngapi kuwaona?

Shahidi: Ni mara ya kwanza

Wakili: Nini kiliendelea baada ya kukuuliza?

Shahidi: Macho yangu yakaanza kuangalia pembeni, kabla sijajibu chochote nikaona kuna anayepokea pesa ila sura yake hana raha na yule anayenihudumia siku zote dukani amekaa chini akiwa anatoka damu puani. Nikawajibu mimi ni machinga nimekuja kuchukua bidhaa kwa ajili ya kwenda kuuza
Wakili: Nini kilifuata??

Shahidi: Yule jamaa alitoa amri na kumwambia mwenzake mtoe lock, nikaanza kupigwa vibao vya masikio, nikasema Mungu mkubwa.

Wakili: Baada ya kutolewa lock kitu gani kiliendelea?

Shahidi: Nilisema Mungu wangu Mungu ni mkubwa. Niliendelea kupigwa na kwa muda huo huo nilianza kupekuliwa, nilichukuliwa pesa na simu yangu na ile karatasi niliyokuwa nimebeba ya kuandikia vitu vya kuchukua.

Wakili: Ilikuwa pesa kiasi gani?

Shahidi: Sh 35,000.

Wakili: Simu ilikuwa aina gani?

Shahidi: Tecno Pop 1.

Wakili: Baada ya kuchukuliwa vitu hivyo kitu gani kiliendelea?

Shahidi: Yule jamaa aliamuru nilale kifudifudi.

Wakili: Ukiwa umelala pale kitu gani kilikuwa kinaendelea.

Shahidi: Nilikuwa nasikia maneno wanayoongea hao na wale wenye duka.

Wakili: Unakumbuka walikuwa wanaongelea nini?

Shahidi: Huyu mwenye duka anaulizwa kwa nini hutoi risiti iliyokamilika endapo umeuzia wateja? Yule mwenye duka akawa anajibu mimi risiti natoa.

Wakili: Aeeeh.

Shahidi: Baada ya hapo huyo anayemhoji mwenye duka alikuwa anamlazimisha aseme yale ambayo anayataka yeye.

Wakili: Ni yapi alikuwa anataka aseme.

Shahidi: Alikuwa anataka aseme hawatoi risiti, yule mwenye duka kuna muda alikuwa anakubali kusema yale wanayoyataka.

Wakili: Umesema walikuwa wanabisha kuhusu mambo mawili, kitu gani kingine walikuwa wanaongea.

Shahidi: Mwenye duka alikubali hatoi risiti kama walivyotaka wao, wakachukua simu wakaanza kumrekodi; nilisikia akisema leta simu tuchukue ushahidi, sikujua ni ushahidi wa nini.

Wakili: Kitu gani kingine walikuwa wanaongelea?

Shahidi:
Mwenye duka akaulizwa nyie mnafanya biashara hii mbona mnabadilisha dola?

Wakili: Mwenye duka alikuwa anajibu nini?

Shahidi: Akajibu sisi hatubadilishi dola.

Wakili: Ukiwa umelala hapo chini?

Shahidi: Baada ya kusikia anasema lete simu tumrekodi nikawa naangalia, napigwa kibao naulizwa unaangalia nini narudisha kichwa chini.

Wakili: Mbali ya hayo mabishano nini kingine ulikisikia ukiwa umelala pale chini?

Shahidi: Baada ya muda kidogo huyuhuyu ambaye ni mwenye duka akawa ameachiwa akawa anaambiwa ampigie mwenye duka aweze kuja.

Wakili: Baada ya kumwambia hivyo iambie mahakama mwenye duka aliweza kufika na kama alifika nini kilitokea?

Shahidi: Baada ya hapo mdogo wa mwenye duka ndiye aliyekuja anaitwa Hajirin.

Wakili: Baada ya kuja Hajirin?

Shahidi: Akaingia dukani akawa anasalimia akamsalimia kwa jina lake,Lengai Sabaya mkuu heshima yako bwana vipi? Aliyekuwa anasalimiwa hakuitikia salamu akamuuliza wewe ndiyo Mohamed Saad ambaye ndiye mwenye duka hili? Hajirin akajibu mimi siyo mwenye duka mi ni mdogo wake amenituma nije kuangalia kwamba kuna nini?

Wakili: Baada ya hapo?

Shahidi: Baada ya kujibu vile yule anayemuuliza akamjibu ninayemtaka hapa ni mwenye duka piga simu aje hapa.

Wakili: Eeh baada ya hapo kitu gani kiliendelea?

Shahidi:
Hajirin alimjibu ndugu yangu yuko mbali ila akazidi kumlazimisha aje, lakini Hajirin akamjibu hayupo ndiyo maana amenituma shida nini.

Wakili: Kitu gani kingine kiliendelea?

Shahidi: Huyu jamaa alimwambia Hajirin mnafanya biashara kimakosa hamtoi risiti inavyostahili, ila Hajirin akajibu duka sio langu nimetumwa nije niangalie nini kinachoendelea.

Wakili: Baada ya Hajirin kuonekana hajui chochote.

Shahidi:
Tukakaa muda kidogo akaingia mtu mwingine pale dukani akasalimia habari ya saa hizi Mhe Lengai Ole Sabaya akarudia tena kusalimia. Aliyesalimiwa akauliza wewe umefuata nini hapa? Akaulizwa wewe ni Diwani wa kata ya Sombetini kitu gani kimekuleta huku?

Wakili:
Alijibu nini?

Shahidi: Akamjibu Sabaya wewe ni Mkuu wa Wilaya ya Hai sasa huku wewe inakuhusu nini, kwa nini unakuja huku wakati siyo sehemu yako?

Wakili: Kitu gani kilifuata?

Shahidi: Bado aliendelea kuongea huyu diwani akamwambia hapa kuna mkuu wa wilaya pia kuna TRA, hii ilitakiwa wao waje kushughulikia hili siyo wewe.

Wakili: Kitu gani kilifuata baada ya majibu hayo?

Shahidi: Sabaya akawa naye anatoa maneno akamwambia utakuwa unashirikiana na hawa Waarabu, akatoa amri huyu naye mtoeni lock.

Wakili: Ndio alifanywaje?

Shahidi: Ndio vile kama nilivyofanywa mimi, alipigwa vibao unasikia tu paa paa.

Wakili:
Kitu gani kiliendelea?

Shahidi: Baada ya kumalizana na Bakari, tukakaa muda kidogo kijana mmoja akapewa amri kwamba ondoka akaondoka akakimbia na mimi nikaambiwa na wewe ondoka.

Wakili: Iambie sasa mahakama uliondokaje pale mahakamani?

Shahidi: Nilikuwa natembea nilipofika mlangoni nikakumbuka nyuma nimeacha hela na simu, nikamwambia naomba simu na hela yangu, kwa sababu umeshaniruhusu niondoke. Yule jamaa akajibu huyu bado ana wenge mtoe tena lock, nikachuchumaa nikapigwa moja kubwa nikaulizwa bado unadai, nikakimbia zangu hela na simu nikaacha hapohapo.

Wakili: Huyu mtu uliyemuambia simu yangu na hela zangu vipi alikua anaonekanaje?

Shahidi: Alikuwa sio mnene sana na alikuwa mweusi alikuwa amevaa kaunda suti ya bluu.

Wakili: Ukimuona leo unaweza kumkumbuka?

Shahidi: Ndiyo naweza kumkumbuka kama atakuwepo.

Wakili: Hebu angalia watu waliopo huku mahakamani kama yupo sema yupo na yuko wapi?

Shahidi: Yule pale (alimtambua Sabaya na kumgusa bega)

Wakili: Ile hela na ile simu mpaka leo hii ziko wapi?

Shahidi: Wako navyo wao.

Wakili:
Ulieleza mahakama kule ndani ulipoenda kuchukua vitu ulivyotoka nje ulikuta kuna hali gani?

Shahidi: Kule nje kulishakuwa tayari ni usiku.

Wakili: Hebu ieleze mahakama kule ndani kulikuwa na hali gani mpaka ukamuona aliyechukua simu zako?

Shahidi: Kule ndani kuna taa zina mwanga mkubwa sana.

Wakili: Hebu iambie nini unakumbuka ulifanya tarehe 16/2/2021 kuhusiana na ishu ya tarehe 9/2/2021.

Shahidi: Nilienda Polisi kwani niliitwa.

Wakili: Uliitwa kwa ajili ya nini?

Shahidi: Nilienda polisi baada ya kupigiwa na Hajirin kwamba tunatakiwa tukatoe maelezo kutokana na tukio lile.

Wakili: Kwa nini hukwenda polisi kabla ya hapo?

Shahidi: Sikwenda kutokana na aliyetufanyia ni mkuu wa wilaya, sikuweza kwenda kwa sababu ya woga.

Akiongozwa na Wakili Kweka alidai kuwa kilichomfanya amkumbuke Sabaya, ni kutokana na ukweli kuwa alipofika mlangoni na kukumbuka ameacha simu, Sabaya ndiye aliyeamuru aliokuwa nao wampige (kumtoa lock).

Akihojiwa na wakili wa utetezi Moses Mahuna, shahidi huyo alidai kuwa licha ya kupigwa, kunyang’anywa simu na fedha alizokuwa nazo, hakuweza kuripoti katika kituo cha polisi kwa sababu ya hofu aliyokuwa nayo.

Akihojiwa na wakili Dancan Oola, shahidi huyo wa tatu alidai licha ya kukuta kundi la watu dukani hapo, anayemkumbuka ni Ole Sabaya peke yake ambapo shahidi huyo alimtambua kwa kumshika bega.
 
Back
Top Bottom