Kesi ya Sabaya: Shahidi amtambua baunsa aliyempiga

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
679
1,000
Shahidi wa Sita Bakari Msangi (38) amemtambua kwa kumgusa bega la kushoto mahakamani mshtakiwa namba tatu, Daniel Mbura kuwa ndiye baunsa aliyekuwa akimpiga kipigo kikali katika duka la Shaahid Store.

Hata hivyo amehoji mahakamani kutokuwepo kwa mtuhumiwa, Deogratias Peter ambaye alimtambua katika gwaride la utambuzi kituo kikuu Cha polisi jijini Arusha ambaye ni mmoja ya baunsa waliimpiga siku ya tukio

Akiongozwa na mawakili mkuu wa Serikali ,Tumaini Kweka Mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Msangi aliieleza mahakama hiyo kwamba kipigo alichokipata ni sawa na nusu kifo kwani alipoteza fahamu kwa muda huku akiwa amefungwa pingu mguuni na mikononi huku walinzi wa Sabaya walimwambia kosa lake ni kuingilia dili ya Mkuu wao na sijui kama anaweza kubaki salama.

Sabaya na wenzake Silyvester Nyengu(26) na Daniel Mbura(38) wanatuhumiwa Kutumia Silaha kupora katika tukio lililotokea Februari 9 mwaka huu katika duka la Shaahid Store lililopo mtaa wa Bondeni Jijini Arusha duka linalomilikiwa na Mfanyabiashara Mohamed Saad (45).

"Nilimsikia Sabaya alisema kuwa mkuu wa wilaya ya Arusha ni masikini Sana angalia kigari anachoendesha sijui amemtoa wapi"alisema Msangi

Shahidi alisema wafanyabiashara hao wa kiaarabu walitafutwa na Sabaya usiku kucha hadi majumbani mwao lakini hawakuweza kufanikiwa kuwapata usiku huu hadi walipoamua kukataa tamaa.

Alisema wakati anazungushwa mjini maeneo mbalimbali kumsaka Mmiliki wa duka la Shaahid Store ,Sabaya aliendelea kumtisha kwa Bastola akiwa ndani ya gari na Msangi aliomba asimuue kwa kuwa ana Mke na watoto ambao wote ni wagonjwa na wanamtegemea.

Msangi ambaye alikuwa akitoa ushahidi huku akilia kwa uchungu aliendelea kusema kuwa alimsikia Sabaya akisema kuwa shughuli zote anazifanya Arusha za kuwasaka Waarabu ni maelekezo kutoka ngazi ya juu hivyo hakuna kiongozi wa Arusha wala Polisi anayeweza kumuuliza chochote pindi anavyofanya shughuli Arusha

Shahidi aliieleza Mahakama kuwa Sabaya alitaka kumpiga Risasi mke wake baada ya kuja katika Lodge ya Tulia iliyopo Sakina Jijini Arusha alipokuja kunifuata kwa lengo la kumwomba Mkuu huyo asiniue mie lakini alishindikana.

Msangi Alisema mke wake alimpigia makoti Sabaya na Kumwomba asimuue lakini alichomolewa Bastola na kuwekewa mdomoni akitaka kumwua ndipo mke wake alipolia na kuangukia chini ya miguu na baadae aliishia kumsukuma akishirikiana na walinzi wake na kuondoka.

Alisema katika muda wote yeye alikuwa amefungwa pingu ya mkononi akiwa ndani ya gari na mlinzi wake alimsihii Msangi kutopiga kelele wala kumsemesha Sabaya vinginevyo atamkosa Mke wake na alifanya hivyo huku akiomba mungu.

Shahidi Alisema aliambiwa na Mmoja wa walinzi wa Sabaya kuwa mjadala unaendelea kuwa yeye kuuawa ama kutouawa na baada ya mabishano hayo Sabaya aliwaambia muamue chochote mtakachofanya juu yake kuuawa ama kuachiwa huru.

Msangi alidai kuwa Februari 16 mwaka huu aliitwa kituo kikuu Cha polisi jijini Arusha ili kuwatambua Watuhumiwa walioshiriki tukio la Februari 9 mwaka huu katika duka la Shaahid Store .

Alidai kuwa katika magwaride mawili ya utambuzi hapo polisi alimtambua Deogratias Peter na Daniel Bura kuwa ndio waliokuwa wakimpiga Sana kwa amri ya General Lengai ole Sabaya Ila alishangaa kwanini mtuhumia Peter hayupo mahakamani.


Ends......
 

Mgibeon

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
10,235
2,000
Dah, General Lengai Ole Sabaya!!!

Jamaa alikua na na jeshi lake.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,793
2,000
Ndio tatizo la kuwapa ma-teenager madaraka, iko siku watasababisha vifo ndio mamlaka za uteuzi zipate akili, wao wanadhani wanakomoa wapinzani kumbe wanaishia kuwatesa raia wasio na hatia.
 

nusaki1974

Member
Apr 11, 2019
70
125
Maagizo kutoka juu sasa yamegeuka kuwa maagizo kutoka chini futi sita kaburini chato. Hana pa kuegemea ndiyo ataelewa Mungu hakutania aliposema "mimi ndimi bwana Mungu wako usiabudu miungu wengine"
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,952
2,000
Pona ya General Lengai Ole Sabaya ni kufungwa la sivyo mtaani watamla Kiboga kwa namna yyt kama revenge!
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,148
2,000
Kwa ushahidi wa upande wa mashitaka sabaya hana pakujifichia
Ki ukweli, ktk sakata hili sioni Sabaya anachomokoe wapi, japo rais Nyerere aliwahi kusema sheria ina mambo ya ajabu sana, hayo maajabu nasubilia niyaone kwenye kesi hii!!kwani hata mawakili wake, maswali wanakosa yenye mashiko, kuwabana kwani kila anayekuja anatiririka mule mule!!!
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,640
2,000
Mahakama si ipitishe Life sentence tu au kumnyonga hadi kufa huyo Sabaya. Huyo ni binadamu katili sana, angenyongwa tu iwe funzo.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
88,463
2,000
HENRY_KILEWO_on_Instagram:_“Hii_ni_Picha_Bora__kabisa_ya_Wiki...”%22_.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom