Kesi ya Sabaya: Shahidi adai Polisi alimshawishi apokee Rushwa ili aachane na kesi

Shahidi wa sita, Bakari Msangi{38} katika kesi ya Unyang’anyi wa kutumia Sila inayomkabili Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili ameieleza mahakama kuwa askari wa upelelezi wa kituo kikuu cha polisi Arusha aliyemtambua kwa jina moja la Calleb alikuwa akimshawishi kwa rushwa ili aweze kuchukua fedha kutoka kwa Sabaya ili asiendelee na kesi hiyo inayomkabili mtuhumiwa huyo na hata maelezo yake polisi hakumpa nafasi ya kuyasoma.

Sabaya na wenzake wawili,Silvester Nyengu{26} na Daniel Mbura{38} wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa kosa la Unyang’anyia wa kutumia silaha ikiwa ni pamoja na kupora mali na fedha taslimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 3,159,000 katika duka la Shahiid Store linalomilikiwa na Mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha Mohamed Al Saad lililopo mtaani wa Bondeni katikati ya Jiji la Arusha.

Shahidi alisema hayo wakati akihojiwa na Wakili wa upande wa utetezi Mosses Mahuna anayemtetea mshitakiwa wa kwanza na kusema kuwa maelezo aliyotoa polisi hakupewa nafasi ya kuyasoma hivyo aliiomba mahakama kutoyapokea maelezo hayo na kusema kuwa ushahidi anaoutoa mahakamani hapo ndio uzingatiwe na kukubaliwa.

Alisema askari Calleb ambaye alidai mahakamani hapo kuwa ni marehemu na mungu amlaze mahala peponi alikuwa akimshawishi kwa rushwa ya pesa kuwa Sabaya amekuwa akimpigia simu na kutaka akubali na kuchukua kiasi cha pesa na asiendelee kutoa maelezo polisi.

Msangi ambaye ametoa ushahidi wake kwa siku nne mfululizo alisema hakukubaliana na ushawishi wa askari huyo na baada ya hapo askari huyo alikuwa akiandika maelezo yake na kumlazimisha kusaini bila kuyasoma kitu ambacho aliona hakikumfurashisha na yeye aliamua kwenda kumshitaki kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya aliyemtaja kwa jina moja la Gwakisa.

Alisema pamoja na marehemu kuonywa na mkuu wake wa kazi lakini aliamua kuandika alichotaka na kumlazimisha kusaini na baadae alikwenda kuandika maelezo mengine februal 16 mwaka huu katika kituo kikuu cha Polisi Arusha.

Msangi alisema kutokana na hali hiyo aliiomba Mahakama kutokuyakubali maelezo ya awali aliyoyatoa polisi februali 10 mwaka huu na kusema kuwa maelezo aliyotoa kwa siku tatu mahakamani hapo kabla ya kuhojiwa na upande wa uetetezi ndio sahihi na yakubaliwe.

Wakili Mahuna aliiomba mahakama kuyapokea maelezo ya Msangi aliyoyatoa februali 10 mwaka huu kama ushahidi hatua ambayo ilipingwa na upande wa Mawakili wa serikali na kusema kuwa utaratibu wa kutoa kielelezo hicho haukuzingatia muongozi wa kisheria hivyo hayastahili kupokelewa.

Mahuna alipinga hoja hiyo na kunukuu baadhi ya kesi katika mahakama ya Rufaa na kuiomba mahakama kuyakubali kwani Shahidi alichoandika polisi kinapingana na anachosema mahakamani hapo.

Baada ya malumbano hayo Hakimu Mwandamizi,Odira Amworo alitoa uamuzi wa kuungana na Mawakili wa serikali Tumaini Kweka,Abdallah Chavula na Baraka Mgaya kwa kusema kuwa wakili wa utetezi hakuwa sawa kisheria kwani alipaswa kuyasoma kwanza maelezo yote ya Shahidi Msangi aliyoyatoa polisi na baadae kuanza kumuuuliza maswali pale alipoona kuna utata kitu ambacho hakikufanyika hivyo hoja yake ya kutaka kielelezo hicho kipokelewe mahakama inakataa.


Ends...

View attachment 1874273
Kwa hiyo Shetani Calleb kasha danja na yeye? Watapukutika sana
 
Hakuagizwa na Rais, na kama aliagizwa na Rais soma kesi ya Zombe jinsi ambavyo Zombe alichomoka na Bageni anakabiliwa na adhabu ya kunyongwa.

Siku zote you must act upon lawful orders otherwise if you act upon unlawful orders you will be liable personally.

Hii imewakuta wengi sana kuanzia kesi za Holocaust na za General Pinochet etc.

BTW sitaki kuamini kwamba unaamini Sabaya was acting upon orders za Rais, kwamba Magu alimtuma kupora pesa na kupiga watu namna hiyo.

Kama unaamini alitumwa Ina maana unaamini huyo aliyemtuma alikuwa jangili si ndio hivyo ndugu yangu?
You must be an elite person. Bravo!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom