Kesi ya Sabaya: Shahidi adai Polisi alimshawishi apokee Rushwa ili aachane na kesi

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
693
1,000
Shahidi wa sita, Bakari Msangi{38} katika kesi ya Unyang’anyi wa kutumia Sila inayomkabili Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili ameieleza mahakama kuwa askari wa upelelezi wa kituo kikuu cha polisi Arusha aliyemtambua kwa jina moja la Calleb alikuwa akimshawishi kwa rushwa ili aweze kuchukua fedha kutoka kwa Sabaya ili asiendelee na kesi hiyo inayomkabili mtuhumiwa huyo na hata maelezo yake polisi hakumpa nafasi ya kuyasoma.

Sabaya na wenzake wawili,Silvester Nyengu{26} na Daniel Mbura{38} wote kwa pamoja wanashitakiwa kwa kosa la Unyang’anyia wa kutumia silaha ikiwa ni pamoja na kupora mali na fedha taslimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 3,159,000 katika duka la Shahiid Store linalomilikiwa na Mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha Mohamed Al Saad lililopo mtaani wa Bondeni katikati ya Jiji la Arusha.

Shahidi alisema hayo wakati akihojiwa na Wakili wa upande wa utetezi Mosses Mahuna anayemtetea mshitakiwa wa kwanza na kusema kuwa maelezo aliyotoa polisi hakupewa nafasi ya kuyasoma hivyo aliiomba mahakama kutoyapokea maelezo hayo na kusema kuwa ushahidi anaoutoa mahakamani hapo ndio uzingatiwe na kukubaliwa.

Alisema askari Calleb ambaye alidai mahakamani hapo kuwa ni marehemu na mungu amlaze mahala peponi alikuwa akimshawishi kwa rushwa ya pesa kuwa Sabaya amekuwa akimpigia simu na kutaka akubali na kuchukua kiasi cha pesa na asiendelee kutoa maelezo polisi.

Msangi ambaye ametoa ushahidi wake kwa siku nne mfululizo alisema hakukubaliana na ushawishi wa askari huyo na baada ya hapo askari huyo alikuwa akiandika maelezo yake na kumlazimisha kusaini bila kuyasoma kitu ambacho aliona hakikumfurashisha na yeye aliamua kwenda kumshitaki kwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya aliyemtaja kwa jina moja la Gwakisa.

Alisema pamoja na marehemu kuonywa na mkuu wake wa kazi lakini aliamua kuandika alichotaka na kumlazimisha kusaini na baadae alikwenda kuandika maelezo mengine februal 16 mwaka huu katika kituo kikuu cha Polisi Arusha.

Msangi alisema kutokana na hali hiyo aliiomba Mahakama kutokuyakubali maelezo ya awali aliyoyatoa polisi februali 10 mwaka huu na kusema kuwa maelezo aliyotoa kwa siku tatu mahakamani hapo kabla ya kuhojiwa na upande wa uetetezi ndio sahihi na yakubaliwe.

Wakili Mahuna aliiomba mahakama kuyapokea maelezo ya Msangi aliyoyatoa februali 10 mwaka huu kama ushahidi hatua ambayo ilipingwa na upande wa Mawakili wa serikali na kusema kuwa utaratibu wa kutoa kielelezo hicho haukuzingatia muongozi wa kisheria hivyo hayastahili kupokelewa.

Mahuna alipinga hoja hiyo na kunukuu baadhi ya kesi katika mahakama ya Rufaa na kuiomba mahakama kuyakubali kwani Shahidi alichoandika polisi kinapingana na anachosema mahakamani hapo.

Baada ya malumbano hayo Hakimu Mwandamizi,Odira Amworo alitoa uamuzi wa kuungana na Mawakili wa serikali Tumaini Kweka,Abdallah Chavula na Baraka Mgaya kwa kusema kuwa wakili wa utetezi hakuwa sawa kisheria kwani alipaswa kuyasoma kwanza maelezo yote ya Shahidi Msangi aliyoyatoa polisi na baadae kuanza kumuuuliza maswali pale alipoona kuna utata kitu ambacho hakikufanyika hivyo hoja yake ya kutaka kielelezo hicho kipokelewe mahakama inakataa.


Ends...

IMG_20210719_185258_831.jpg
 

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,404
2,000
Kesi ya ajabu haijawahi kutokea. Serikali kumshitaki mtumishi mwakilishi wa rais wilayani kwa kufanya kazi anazoagizwa kupiga vita ufisadi na ukwepaji kodi.
Hakuagizwa na Rais, na kama aliagizwa na Rais soma kesi ya Zombe jinsi ambavyo Zombe alichomoka na Bageni anakabiliwa na adhabu ya kunyongwa.

Siku zote you must act upon lawful orders otherwise if you act upon unlawful orders you will be liable personally.

Hii imewakuta wengi sana kuanzia kesi za Holocaust na za General Pinochet etc.

BTW sitaki kuamini kwamba unaamini Sabaya was acting upon orders za Rais, kwamba Magu alimtuma kupora pesa na kupiga watu namna hiyo.

Kama unaamini alitumwa Ina maana unaamini huyo aliyemtuma alikuwa jangili si ndio hivyo ndugu yangu?
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
23,605
2,000
Kesi ya ajabu haijawahi kutokea. Serikali kumshitaki mtumishi mwakilishi wa rais wilayani kwa kufanya kazi anazoagizwa kupiga vita ufisadi na ukwepaji kodi.
Umeandika kishabiki mno..Hujazingatia matumizi ya bunduki yaliyofanywa, hujazingatia uombaji rushwa uliofanywa, hujazingatia unyang'anyi uliofanywa, hujazingatia kwamba huyu mshitakiwa alitoka wilayani kwake, akamruka mkuu wa mkoa wake, akaingia kwa mkuu wa mkoa mwingine, akaingia wilaya nyingi kuyafanya yote aliyoyafanya!!... Yaani umeandika kishabiki tu
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
9,075
2,000
Kesi ya ajabu haijawahi kutokea. Serikali kumshitaki mtumishi mwakilishi wa rais wilayani kwa kufanya kazi anazoagizwa kupiga vita ufisadi na ukwepaji kodi.
Kwa hiyo ukiwa Mtumishi Mwakilishi wa rais maana yake uvunje sheria?
Kuwa kiongozi unatakiwa kufanya lolote katika misingi sawa na sheria, Kanuni na taratibu, kinyume na hapo utashitakiwa kama mwingine yyt as far as no one is above the law.

Mnahubiri utawala bora wakati hata hamjui hata maana yake.

Haya sasa Mtakula mafi yenu.
 

JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,234
2,000
Kesi ya ajabu haijawahi kutokea. Serikali kumshitaki mtumishi mwakilishi wa rais wilayani kwa kufanya kazi anazoagizwa kupiga vita ufisadi na ukwepaji kodi.
Kesi yenyewe ya kubumba, mashaidi wa kulazimisha. Sabaya asiposhinda kwenye ngazi hi, atashinda kwenye rufaa.

Maelezo hapo juu yanaonyesha shahidi kaja na maelezo ya uongo sasa hivi, lakini kwa siku za nyuma alishatoa maelezo tofauti tena kwa maandishi! Tusubiri hukumu.
 

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
10,467
2,000
Alisema askari Calleb ambaye alidai mahakamani hapo kuwa ni marehemu na mungu amlaze mahala peponi alikuwa akimshawishi kwa rushwa ya pesa kuwa Sabaya amekuwa akimpigia simu na kutaka akubali na kuchukua kiasi cha pesa na asiendelee kutoa maelezo polisi.

Huyo Calleb alikuwa anapambana kumtetea Shetani akaishia Kufa..
 

mazagazagatza

Senior Member
Jul 15, 2021
104
225
Kesi ya ajabu haijawahi kutokea. Serikali kumshitaki mtumishi mwakilishi wa rais wilayani kwa kufanya kazi anazoagizwa kupiga vita ufisadi na ukwepaji kodi.
Acha kutetea jambazi mwenzio wewe.

Serikali ilimtuma Sabaya kwenda kufanya uhalifu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom