Kesi ya Rwekatare polisi yakwaa kisiki; mahakama yachefuliwa na mwenendo wa kesi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Rwekatare polisi yakwaa kisiki; mahakama yachefuliwa na mwenendo wa kesi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Mar 21, 2013.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Kuna mkanganyiko na mgongano katika kesi hii kwa kuangalia mwenendo wake, na giza kutanda kutokana jinsi mwanzo na mwendelezo wake unavyotendeka katika mahakama, jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa mashaka nchini.

  Jeshi la Polisi lagonga mwamba mahakamani kumbakiza Ludovick mahabusu baada ya mahakama kuamuru Ludovick aende gerezani badala ya madai ya kutaka abaki mikononi mwa polisi (mahabusu) kuendelea na upelelezi zaidi.


  1. Ombi la polisi kutaka Ludovik abaki mahabusu ili kuendelea na upelelezi wa kesi ambayo ilifutwa na kufunguliwa upya lagonga mwamba baada ya hakimu kuamuru apelekwe gerezana pamoja na Rwekatare.
  2. Je, Mahakama inaona kuna usumbufu na kiza katika kesi hiyo na kuamua kufuata mkondo wake kwa kuamuru Ludovick aende gerezani badala ya kubaki mahabusu walivyotaka polisi?
  3. Iwapo kesi hiyo iliyofunguliwa awali hati ya mashtaka kuwa na makosa, kimahakama kuna utaratibu ya kufanyia masahihisho kuirekebisha hati ya mashtaka bila kuifuta na hivyo kuondoa mlolongo wa kuanza upya kwa madai yale yale. Je, kuna mgongano kati ya polisi na mkurugenzi wa mashtaka katika kesi hii?
  4. Mkurugenzi wa mashtaka ndiye aliyeifuta kesi ambaye pia ana mamlaka ya kuifanyia marekebisho hati ya mashtaka, lakini polisi kumshika na kumfungulia tena mashtaka yale yale, Mkurugenzi wa mashtaka atakuwa na utetezi upi dhidi ya upande wa watetezi wa washtakiwa?
  5. Je, kuna shinikizo fulani nje ya Polisi ambalo linatifua mwenendo wa kawaida wa keshi hii mahakamani?
  Tundu Lissu atoa tamko
  Kauli ya Tundu Lissu baada ya mahakama kumwachia huru Rwekatare kisha kushikwa tena kuwekwa chini ya ulinzi na kufunguliwa upya mashtaka yale yale yaliyofutwa na mkurugenzi wa mashtaka ni kama ifuatavyo.


  • Mshtakiwa kabla hajajibu mashtaka na kumfungulia mashtaka yaleyale inaonyesha matumizi mabaya ya taratibu za kimahakama.
  • Mahakama kutumiwa vibaya ili hakimu asitoe majibu kwa mambo ambayo yalitarajiwa kutolewa maamuzi. Kwa maneno mengine ni kutifua taratibu za kimahakama.
  • Mashtaka ya Lwekatare licha ya kutajwa kuwa ya kigaidi yapo katika kanuni za adhabu kama makosa ya kawaida kwa mujibu wa sheria kifungu cha 384, hivyo ni makosa yanayodhaminika.

   
 2. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2013
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,385
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mwenendo wa hili jambo, inaleta picha ya haki kuto kutendeka na sheria za nchi kupindishwa kwa makusudi kwa manufaa ya genge fulani.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Binafsi nampongeza busara ya Hakimu kuwatolea nje polisi matakwa yao ya kutaka kumbakiza Ludovick, kuna kila dalili angefanyizwa mambo yasiyo ya kawaida ili tu kumshinikiza aseme kile ambacho hakipo kichwani mwake Ludovick.
   
 4. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2013
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,487
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Jamani, samahani kuwatoa kwenye mada. Nimeangalia hii picha, hivi huyu polisi kweli anaweza kufukuzana na kibaka na akamkamata?
   
 5. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2013
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,385
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Candid Scope mkuu : ili swala la wao kuachiwa na kushikwa tena ni dhahiri lilikua limepangwa, na maanisha hata hakimu alikua anajua kinacho tokea hata IGP na DPP. Inshort yote wanayo fanyiwa ni ya kupangwa kama filamu za maigizo
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Holo hata mimi nimeliona, naona siku hizi hata yale magwaride ya kujiweka sawa kiafya na kiulinzi yameshasahauliwa, vinginevyo hapa ni kutafuta mno tu kwa kwenda mbele.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Inawezaka ikawa imepangwa, lakini kuna kitu ambacho kinaonekana mahakama na polisi kuna mgongano kama ilipangwa iwe hivyo kutokana na ombi la kutaka Ludovick abaki mahabusu ili aendelee kutoa ushahidi katika upelelezi, lakini hakimu amewatolea nje, ni jambo linaloleta mkanganyiko kama yote yaliyotokea mahakamani jana yalipangwa na pande zote tatu yaani mahakama, mkuruguenzi wa mashtaka na polisi.
   
 8. Return Of Undertaker

  Return Of Undertaker JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2013
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2,765
  Likes Received: 11,002
  Trophy Points: 280
  Ajira za kujuana hakufaa kuwa askari na ukiona hivyo ujue kawekwa mahakamani hapo wakijua kazi yake ni kupanga watu na si kutafta waalifu
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2013
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,932
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ndiye huyo sasa kapewa jukumu la kuwa'escort 'MAGAIDI'.
  They can't be serious.
   
 10. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2013
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,697
  Likes Received: 1,426
  Trophy Points: 280
  Mkuu pia hakimu Mchauru polisi wanamuogopa sana kwa misimamo yake, angeqweza kutoa uamuzi wa kuwatia aibu mno!
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kuna uwezekano pia hakimu wa awali aliyepangiwa kesi hiyo upande wa mashtaka hawakuwa na imani naye, ndio maana wakafanya mchezo huo ili kubadilisha wapate hakimu wanayemtaka wao ambaye yupo kwenye system yao.

  cc; Mzizi wa Mbuyu
   
 12. N

  Newcastle Senior Member

  #12
  Mar 21, 2013
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tuko ndani ya maombi Mungu awapige upofu wote wanaokula njama za kuhujumu haki.MUNGU wa sasa ni kijana atatujibu mapema.amen.
   
 13. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2013
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,957
  Likes Received: 702
  Trophy Points: 280
  Candid Scope ... you have a strong urgument which is very very concealed
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2013
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,410
  Likes Received: 2,316
  Trophy Points: 280
  kwani lazima kibaka afukuzwe? Maisha ya kufukuzana yesha pitwa na wakati. Siku hizi unakamatwa kama kuku aliyeatamia mayai au anayetaga. Kama hujawahi kukamatwa na polisi, waulize waliokamatwa kama hata wanaweza kufikiria kukimbia.

  By the way, lwakatare sio kibaka, hawezi kukimbia. Ndi maana hata pingu hafungwi ni kutembea kikakamavu, macho mbele!!!!
   
 15. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  kumbe mnafahamianae? LWAKATARE kumbe ni KIBAKA? teh teh teh.
   
 16. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  Hofu aliyonayo kwa mambo aliyotenda ya ugaidi hata akijikwaa kwenye unyasi lazima ataanguka tu.
   
 17. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2013
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,385
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hapo tunaona Polisi ndio wanao tumiwa na si mahakama, kwasababu wanajua kesi ingendeshwa mahakamani Lwakatare angeshinda kwaiyo kinacho fanyika hapo ni kumpotezea mda na kutaka kujaribu kumchafua Lwakatare na hata chama ikiwezekana pia.
   
 18. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  Hasa aina ya LWAKATARE, hawaogopi hata hofu ya Mungu.
   
 19. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,793
  Likes Received: 13,797
  Trophy Points: 280
  Cha msingi tu amshkishe adabu yao mengine endeleeni nayo ni kawaida yenu, watanzania tunataka amani.
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2013
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mwendesha mashtaka anawezaje kukubali kuiendesha kesi ambayo alishaifuta na kuona hakuna haja ya kuendelea nayo? Hilo jambo ni usanii wa pekee nchini, maana mamlaka ya uendeshaji kesi kuna dalili ya kutojua vema sheria au mazoea ya kupindisha. Sipati picha utetezi mpya atakaokuja nao mwendesha mashtaka kwa kesi aliyoifuta na kuirudisha tena upya baada ya saa moja kufutwa.
   
Loading...