Kesi ya Ponda Mapya yaibuka yule Mganga aliyekamatwa na Tunguli mahakamani ni Mshabiki wa PONDA

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,864
1,225
19 DECEMBER 2012

Kesi ya Ponda Mapya yaibuka yule Mganga aliyekamatwa na Tunguli mahakamani ni Mshabiki wa PONDA*Ugonjwa wakwamisha usikilizwaji wa kesi

Na Rehema Mohamed

KESI inayomkabili Shekhe Ponda Issa Ponda na wenzake, jana imeibua mapya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam baada ya mtu mmoja kukamatwa na tunguli pamoja na vifaa vya uganga mahakamani hapo.

Mtu huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Bw. Rajabu Zuberi (30), mkazi wa Kerege, Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga, alikamatwa katika geti la mahakama akiwa na vifaa hivyo
wakati akikaguliwa kwa kifaa maalumu na wana usalama.

Mahakama hiyo imeanzisha utaratibu wa kuwakagua watu wote wanaofika mahakamani hapo kila inaposomwa kesi ya Shekhe Ponda kwa kutumia vifaa maalumu vya kiusalama.

Jana wakati wana usalama wakiendelea na kazi ya ukaguzi, saa 2:25 asubuhi, ilifika zamu ya Bw. Zuberi ambaye baada ya kupitishiwa kifaaa hicho katika begi hilo, kifaa hicho kikapiga mlio.

Baada ya wana usalama kusikia mlio huo, walimuuliza Bw. Zuberi alichoweka katika begi hilo lakini alisuasua kujibu na kushindwa kutoa majibu ya kueleweka.

Kutokana na hali hiyo, alitakiwa kufungua beki hilo ndipo alipokutwa na vifaa vya uganga ikiwemo tunguli na pembe.

Alipohojiwa kuhusu vitu hivyo alisema, yeye ni mganga wa kieneji kutoka Kerege, mkoani Tanga ambapo vitu hivyo alibebeshwa na mfanyabiashara aliyemtaja kwa jina la Bi. Senorisa Urasa (35).

Wakati mganga huyo akiendelea kuhojiwa, mfanyabiashara huyo alikimbilia katika vyoo vya mahakama hiyo ndipo wanausalama walipokwenda kumkamata.

Bi. Urasa alipohojiwa alikiri kumleta mganga huyo mahakamani hapo ili amsaidie katika kesi yake ya bila kutaja inahusiana na
madai gani.

Kesi ya Ponda
Makamaha hiyo jana ilishindwa kusikiliza kesi ya Shekhe Ponda na wenzake kutokana na mshtakiwa huyo kuumwa hivyo kushindwa kufika mahakamani.

Wakili wa Serikali Bw. Tumaini Kweka, aliieleza mahakama hiyo mbele ya Hakimu Victoria Nongwa kuwa, amepata taarifa kutoka kwa askali Magereza kuwa mshtakiwa Shekhe Ponda anaumwa hivyo ameshindwa kufika mahakamani.

Wakili anayewatetea washtakiwa hao Bw. Juma Nassoro, naye hakuwepo mahakamani baada ya kupata hudhuru hivyo Bw. Kweka aliomba ipangiwe tarehe nyingine ya kusikilizwa shauri hilo.

Kutokana na sababu hizo, Hakimu Nongwa, aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 31 mwaka huu. 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom