Kesi ya nyani unampelekea ngedere: iweje CAG akaripoti kwa rais badala ya Bunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya nyani unampelekea ngedere: iweje CAG akaripoti kwa rais badala ya Bunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Mar 30, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nimeshangazwa na utaratibu wa kiwizi na kulindana unaotengenezwa na sirikali ya CCM kupitia kwa mteule wa rais mh Rudovick Utouh kuwa taarifa zote za ukaguzi zianzie kwake na kisha wizarani then ndo ziende bungeni.

  Hivi toka lini mimi nikukague wewe sirikari then uwe wa kwanza kupokea riport then uipeleke ktk chombo/ muhimili mwingine ( bunge) ndo waujadili

  Kuna nini hapo katikati? Au mnataka kutwambia nn vile vimemo vya kupokea ugeni na misafara yako mkaviondoe au zile posho za vikao hewa
   
 2. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ni hitaji la kisheria
   
 3. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  sijaelewa mantiki ya vyombo vya habari kulipamba hili tukio!
  Sielewi tafsiri yake kwa mwananchi mvuja jasho wa kawaida.
   
 4. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huu ni utaratibu wa kimagamba tu,hatuna sheria inayoweka hitaji la hivyo.Waache magamba walindane
   
 5. bigcell

  bigcell JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Bunge ndio muidhinishaji wa bajeti ya serikali kwa kila msimu wa mwaka wa serikali, so imeekaaje hapa Utoh kupeleka ripoti kwa mtumiaji yulyule aliyepangiwa na bunge pasipo muidhinishaji kurudishiwa taarifa za matumizi. Wakuu hpo imekaaje labda mi sielewi.
   
 6. p

  politiki JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mjomba unachokisema ni cha msingi mno na solution yake ni katiba pamoja na CAG vyombo vyote vinavyosimamia serikali havikupaswa kuwa chini ya watu wale wale wanaowasimamia. lengo kubwa la kutengeneza mfumo wa kiubabaishaji namna hii ni kwa ajili ya serikali kuwa na control na vyombo hivi kwani vingekuwa na nguvu ya kweli basi wao ndio wangekuwa wa kwanza kuingia matatizoni kwahiyo vyombo hivi vinapoteza pesa za walipa kodi bure kwani vinaibua madudu ya serikali halafu vinaipa serikali ile ile ijichukulie hatua za nidhamu kwaiyo havifanyi kazi kumlinda mwananchi bali kuwalinda viongozi mafisadi.
   
 7. p

  pat john JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 245
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sheria inasema hivyo. Rais atapokea ripoti na baadaye aipeleke BUNGENI.
   
 8. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #8
  Mar 30, 2012
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kwani utaratibu au sheria inasema vipi? Msiwe mnalaumu watu wakiwa ndani ya sheria.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ndio maana jeikei kaona utouh kachemka akamwambia next tym peleka ripoti kwa ofisi ya pm na wwf wazipeleke bungeni lkn hapa ni usanii tu wa jk pamoja na utooh
   
 10. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #10
  Mar 30, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Si bora hilo la report!watumishi wake wanaajiriwa na ofisi ya utumishi ikimaanisha hana uwezo wa kuajiri anaemtaka,jukumu lote kakabidhiwa Katibu utumish ndg George yambesi,one day atajaziwa vilaza washindwe kupiga mzigo,hilo la wapi ipelekwe report linahitaji mjadala kwani kama kigezo ni kuwa yeye ndo anaikagua serikali so report iende moja kwa moja bungeni kwan si huyohuyo anaikagua ofisi ya bunge pamoja na pesa za mfuko wa bunge?
   
Loading...