Kesi ya Ndugai kumtambua Mwambe kama Mbunge: Wakili wa Serikali adai maamuzi ya Spika hayaruhusiwi kuhojiwa na chombo chochote

Serikali imeieleza Mahakama ya Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa maamuzi yoyote yanayotolewa na Bunge hayaruhusiwi kuhojiwa na chombo chochote na kuomba pingamizi hilo likubaliwe na mahakama itoe uamuzi kwamba haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kuifuta kwa gharama.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Vicent Tango wakati akiwasilisha mapingamizi ya awali yenye hoja tano mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Issa Maige katika kesi ya kikatiba namba 10/2020 iliyofunguliwa na Wakili Paul Kaunda anayeiomba Mahakama Kuu kutengua amri ya Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kumtambua Cecil Mwambe kama Mbunge halali wa Ndanda.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Mei 28, mwaka huu kwa ajili ya kutolewa uamuzi ambapo Jaji Maige amemuagiza mdaiwa wa pili Mwambe, kuwasilisha mahakamani hapo hati ya kiapo na kumpatia mdai.

#Mahakamani #SpikawaBunge #JobNdugai #Bunge #kesikikatiba #VicentTango
Huyo wakili ni kilaza wa aina yake.Hajataja hata ibara ya Katiba au kifungu cha sheria inayompa mamlaka hayo!
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi. Mahakama haiwezi kutengua maamuzi ya spika. Lakini inaweza kutoa tafsiri sahihi ya kikatiba/kisheria kuhusu jambo linalolalamikiwa. Kama kikatiba jambo alilofanya spika ni batili, spika ataamua mwenyewe cha kufanya.
Duh, kwa hyo hakuna chombo cha kumdhibiti spika hata akavunja katiba ya nchi.duh tumekwisha.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Serikali imeieleza Mahakama ya Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuwa maamuzi yoyote yanayotolewa na Bunge hayaruhusiwi kuhojiwa na chombo chochote na kuomba pingamizi hilo likubaliwe na mahakama itoe uamuzi kwamba haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kuifuta kwa gharama.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Vicent Tango wakati akiwasilisha mapingamizi ya awali yenye hoja tano mbele ya jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Issa Maige katika kesi ya kikatiba namba 10/2020 iliyofunguliwa na Wakili Paul Kaunda anayeiomba Mahakama Kuu kutengua amri ya Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kumtambua Cecil Mwambe kama Mbunge halali wa Ndanda.

Kesi hiyo imehairishwa hadi Mei 28, mwaka huu kwa ajili ya kutolewa uamuzi ambapo Jaji Maige amemuagiza mdaiwa wa pili Mwambe, kuwasilisha mahakamani hapo hati ya kiapo na kumpatia mdai.

#Mahakamani #SpikawaBunge #JobNdugai #Bunge #kesikikatiba #VicentTango
Courts cannot entertain hypothetical issues.
 
Sasa wewe naye kama kipofu, aliyefuta ubunge wao ni mbowe anayewatetea wapiga kura waliowachagua ni Spika, ww unakwama wapi?? au una ugonjwa wa Spikaphobia?
Wewe ni mzito sana sana wa kuelewa au haujui kiswahili, nakushauri futa ulichoandika.
Nilichosema kinahusu maamuzi ya Spika kutohojiwa.
 
Kw
Duh, kwa hyo hakuna chombo cha kumdhibiti spika hata akavunja katiba ya nchi.duh tumekwisha.
Sadly! Obviously kuna tatizo la kisheria/katiba. Anachofanya spika ni sawa na kumlazimisha mtu awe au aendelee kuwa mbunge wakati mwenyewe hataki.
 
Inasikitisha sana, bila kuwa Na vyombo huru ikiwemo mahakama Ni hatari.katiba inavunjwa hovyohovyo mahakama IPO tu
 
Wanasheria uchwara wa bongo hata hili hamlioni?
Ibara ya 107(A)_1
Tuwekee hicho kifungu hapa ndugu Na unukuu pia..
 
Inasikitisha sana, bila kuwa Na vyombo huru ikiwemo mahakama Ni hatari.katiba inavunjwa hovyohovyo mahakama IPO tu
Tuwekee hicho kifungu hapa ndugu Na unukuu pia..
"Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika jamuhuri ya Muungano itakuwa Ni mahakama"
 
Daaah! Huyu ndugu yangu Vicent Tango hajawa Jaji hadi leo? Wenzake akina Elvis na Juma (Jaji Mahakama kuu kanda ya Katavi/Sumbawanga) mbona wametoboa kitambo? Anakwamia wapi?
 
Kasoro Mbowe tu anayeruhusiwa kuvunja katiba kwa kukiuka ibara ya 13 ya haki ya kusikilizwa!!! wabunge wanafukuzwa kama mtu anaswaga kuku!!

Mbowe amemfukuza nani? Sidhani kama ana hayo mamlaka.
Aidha, kaisome tena hiyo ibara 13. Ibara hiyo anazungumzia haki mbele ya Sheria. Chadema kama taasisi nyingine zinaongozwa na Katiba na kanuni ambazo zimejiwekea. Kama mtu hakubaliani na alivyotendewa ana haki ya kwenda Mahakamani ambako atapewa nafasi ya kujieleza.

Amandla...
 
Back
Top Bottom