Kesi ya Mwangosi, vigumu sana haki kutendeka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Mwangosi, vigumu sana haki kutendeka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mystery, Sep 14, 2012.

 1. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #1
  Sep 14, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,951
  Likes Received: 6,711
  Trophy Points: 280
  Tumeshuhudia tokea Mwangosi auawe kinyama na polisi, septemba 2, mwaka huu, na jinsi, jeshi hilo la polisi, lilivyojitahidi kwa juhudi zote, kujifanya kuwa wao hawakuhusika, badala yake wakadai, kuna kitu kizito kimerushwa toka kwa wafuasi na viongozi wa Chadema, lakini kwa jinsi Mungu alivyo mkuu, aliwapa ujasiri wapiga picha, wakapata picha zenye ushahidi wa wazi, kuwa polisi ndiyo wamehusika na mauaji hayo. Sasa wasiwasi wa wananchi wengi ni kuwa huyo polisi waliyemfikisha mahakamani, wamelazimika tu kumfikisha mahakamani, kutokana na shinikizo kubwa sana la vyombo vya habari na wananchi, pamoja na wanaharakati. Sasa kutokana na mlolongo wa matukio, kama vile kumfikisha mtuhumiwa mahakamani na gari la kifahari, la Land Cruiser, polisi kuzuia kabisa, mtuhumiwa huyo, asipigwe picha na paparazi. Vile vile, kitendo cha Kamuhanda kutoshtakiwa na kuendelea na kazi, wakati inafahamika wazi kuwa yeye, ndiye aliyesimamia hiyo operesheni ya mauaji ya Mwangosi. Kwa mazingira hayo nadhani ipo haja kwa wanaharakati na wanasheria wazalendo, kutoa taarifa ya kuwa hatuna imani na mahakama hiyo, kama mashahidi wa kesi hiyo, ndiyo hao hao mapolisi, wanaozuia hata mtuhumiwa asipigwe picha! Kwa hiyo nadhani ingekuwa vyema, wanasheria wazalendo wakaangalia vifungu vya sheria, vinavyoweza kuruhusu kesi hiyo, ihamishiwe mahakama ya kimataifa,ya the Hague, ambako tunaamini haki itaweza kutendeka
   
 2. M

  Mlyafinono Senior Member

  #2
  Sep 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatakama watazuia haki kutendeka lakini Damu ya Mwangosi haiwezi kwenda bure katika midomo ya ardhi.They will pay for it
   
 3. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #3
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wangekuruhusu ukapiga izo picha, zingesaidia lolote kwenye ushahidi? kwa wao kuzuia kupiga picha, je? kuna defect yeyote kwenye ushahidi? uliwauliza watoe sababu yeyote ya kwanini wanazuia kupiga picha na kwanini wamemleta kwa escort ya landcruiser na ulinzi kabambe wa polisi? pengine wangekuwa na sababu maalumu kukueleza na ungepata jibu hukohuko wala usingeleta hapa.

  kuhusu kutokuwa na imani na mahakama husika, unataka watu waikatae mahakama hiyo kwamba hawana imani nayo halafu shauri lipelekwe mahakama ipi? kwani mahakama ile ya wilaya/mkazi ndiyo yenye mamlaka kusikiliza shauri la mauaji?....kwaakili yako unafikiri mahakama ile ndiyo itakayosikiliza kesi hiyo?

  kwa ushauri na kufahamishana ni kwamba, pale ile kesi haitasikilizwa na mahakama ile, labda kwa direction ya High court ikaliwe pale kama ni RM kwa extended power. ila shauri lile lipo pale wakati uchunguzi unaendelea, upelelezi ukikamilika vijalada vitafungwa na accused atakuwa committed to the High court...yaani pale PI yake itakapofungwa...hapo lipo kwaajili ya committal proceeding tu...na si vinginevyo...kwahiyo usiwe na wasiwasi, wala usipotezee watu muda kujadili hili, kwasababu mahakama itakayosikiliza shauri lile siso ile ya wilaya/mkazi, ni mahakama kuu na kutakuwa na majaji sio mahakimu, na kama upande wa mashitaka hawataridhika kuna nafasi kukata rufaa hadi court of appeal.

  kuhusu mashahidi kuwa ni polisi...hapana, sio polisi peke yake, hata wewe kama una maelezo yeyote yatakayosaidia kwenye ushaidi nenda pale polisi iringa katoe maelezo watakuweka kwenye folio C na utakuwa shahidi mzuri tu, hata wale polisi waliopiga picha na wananchi wa kijiji kile kama hawatakataa kutoa maelezo watakuwa mashahidi wazuri tu wakichukuliwa maelezo. hivyo si polisi peke yao watakaotoa ushaidi....kama hujaelewa chochote uliza nitakujibu.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wewe ndio umeongea point, mahakama za hapa duniani si mahakama za haki. kuna sababu nyingi tu, hata ushahidi na mashahidi vinaweza kuharibiwa na kesi kufa. kuna mambo mengi yanaweza kufanya kesi isishinde. sasa, cha kuelewa ni kwamba, mhukumu mkuu ni Mungu aliye juu, aliyeumba mbingu na dunia na kila mtu aliyepo duniani, huyo ndiye anayeweza kuhukumu na kutoa kisasi. imeandikwa kisasi si cha mwanadamu, kisasi ni changu mimi Mungu, ....ina maana kwamba, wanadamu hatuwezi kutoa kisasi kikakolea, anayejua kutoa kisasi na kuhukumu na hukumu ikakolea na ikawa ya haki, ni Mungu aliye juu...huyu ndiye hakimu na jaji wa kila mtu. auae kwa upanga atakufa kwa upanga....lakini yote katika yote, hapo ndio utamshangaa Mungu, ANASAMEHE, ANA REHEMA, REHEME ZA MUNGU NI KUU KULIKO DHAMBI ZETU...the mercy of the Lord is greater than our sins....na Mungu angehesabu maovu, nani angesimama? sisi sote tu watenda dhambi,....ukigeuka na kutubu kwa kweli, Mungu anakusamehe hata kama umetenda dhambi nyekundu kama damu....huu ni ujjumbe kwa polisi wote ambao walishiriki yale mauaji na hawajakamatwa labda wamejificha au wamefichwa akafikishwa tu yule mmoja mahakamani....kama hamtatubu na kuacha, damu ya huyo inalia mbele za Mungu....tubuni basi.
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,739
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Kuna mahakama mbili hapa, moja lazima itatenda haki...je waijua ni ipi? Ni Mahakama ya Wananchi.

  Hii nyingine ijue fika hukumu kuu/rufaa imeshatolewa na wananchi kuwa Polisi, kwa niaba ya serikali ambayo nayo kwa niaba ya CCM imekuwa ikitekeleza ukatili na mauaji kwa kisingizio cha (vurugu za) kisiasa. Kwa hivyo CCM hadi polisi wamehusika na kifo cha Mwangosi. PERIOD.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sasa wewe unaongelea haki au upendeleo?

  Kwani askari aliyeshikwa yeye hana haki zake?
   
 7. r

  raymg JF-Expert Member

  #7
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kwa jinsi mtuhumiwa anavyofikishwa mahakaman bila kuonekana sura....ninahisi sio mwenyewe huenda n pandikizi kutoka kwenyebaadhi ya mageraza nchi waliokua watumike kwenye issue ya Ulimboka.....
   
 8. r

  raymg JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  how...
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Ubungoubungo unakumbuka hili uliloliandika?
  Haki itatendeka vipi kama ushahidi wenyewe ndio kama huu uliotolewa hapo nyuma na Ubungoubungo? Halafu unadai kuwa kama yupo asieelewa, mwenye majibu ni wewe, duh! Why dont some people just shut up and disappear!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #10
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  yap, niliandika mimi mwenyewe, lakini unachotakiwa kujua ni kwamba, kuna principle of complimentarity ambayo itachukua si chini ya mwaka mmoja hata icc kuamua kutia timu. na pia kwa kosa kama hili, ninachofikiri ni kwamba, local courts ndio zitashughulikia kulingana na ingredient za makosa yale manne ukilinganisha na tukio hili. you are the one who should shut up and disappear forever. unachotakiwa kuelewa ni kwamba, suala hili icc haitalipokea, hata kama haki haitatendeka hapa ni kwamba, waendesha mashitaka wetu/ AG/DPP watatakiwa kukata tu rufaa na si vinginevyo, halikubaliki kwenye vigezo ya icc....you need to understand and shut up, and disappear forever too.
   
 11. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #11
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  walimficha kwako au walimficha na kwa waendesha mashitaka pale mahakamani....wewe ulitaka umwone halafu kiongezeke nini kwako au katika kusaidia kesi....kama ni pandikizi au la, nani kati yako wewe na hakimu aliyetakiwa kudetermine?
   
 12. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #12
  Sep 14, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Hivi yule muuaji mwingine aliyeitwa Ukiwaona Ditopile Mzuzuri naye alikuwa akifunikwa sura asitambulike kila wakati alipokuwa akifikishwa mahakamani?
   
 13. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #13
  Sep 14, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  icc imeingiaje hapa...
   
 14. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #14
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  what do you mean....inaingiaje wapi...mbona haueleweki, funguka tukueleweshe.
   
 15. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #15
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kufunikwa vile ni kosa kisheria? kuna madhara gani umepata au haki gani umenyimwa kisheria?
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Sep 14, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Unieleweshe! nani? wewe? thanx but no thanx...
  Jibu swali na kama huwezi kaa kimya...niliuliza kama Ukiwaona Ditopile Mzuzuri naye alikuwa akifunikwa sura.
   
 17. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #17
  Sep 14, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,926
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  kamhanda na polis wake wana kesi ya kujibu lini na wapi time will tell
   
 18. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #18
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Hivi wauaji wa Imran Kombe walishanyongwa au badoooo? Jibu la hili swali litatupa picha kamili ya mwenendo mzima wa hii kesi na matokeo yake!
   
 19. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #19
  Sep 14, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Wako huru, na wamepewa bonge la ardhi katika Tanzania yetu ya amani na mshikamano.
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Sep 14, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Basi hakuna hata haja ya kuhangaika na kesi ya hawa wahuni wa Polisi. Tungojee muda ukifika tuyafukue maovu yote kuanzia ya deep green, epa hadi hii ya mwangosi. Kiutaratibu Polisi mwenye cheo anapotoa kauli inakuwa ni amri. Yule Polisi aliyekuwa kamkumbatia mwangosi akiwazuia wenzake wasimuadhibu alikuwa akiwaambia kuwa anamjua yule ni mwandishi lakini wale constable walipuuza kauli ya afande wao wakaendelea kumuadhibu Mwangosi. Ni wazi kuwa walikuwa wakitekeleza amri na maelekezo waliyopewa na mkubwa zaidi ya jamaa aliyekuwa akiwakataza wasimpige Mwangosi!
   
Loading...