Kesi ya Mwangosi: Mwandishi atiwa nguvuni Iringa

Nsaji Mpoki

JF-Expert Member
Nov 5, 2007
396
65
February 13, 2014

E84A0505.JPG

Yametimia polisi wamemakamata mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard (kushoto) ambae ni mwandishi wa magazeti ya serikali wakimtuhumu kupiga picha mahakamani ,hadi sasa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi huku kesi ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi
 
Polisi wa Tanzania utadhani wanavutishwa bangi kwa mambo wanayoyafanya hata huko Somalia hatuyasikii kama haya.
 
February 13, 2014

Yametimia polisi wamemakamata mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard (kushoto) ambae ni mwandishi wa magazeti ya serikali wakimtuhumu kupiga picha mahakamani ,hadi sasa amewekwa chini ya ulinzi wa polisi huku kesi ya mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi

Mbona aliyepiga hii picha hakukamatwa?

dawa.jpg
 
Hivi kunasheria za kuzuia picha mahakamani kabla kesi aijaanza?
 
Mtuhumiwa wa mauaji yuko wapi? kwanini wamemhamisha kazi badala ya kukaa mahabusu?
 
Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa sheria wa Westminster, unaofuatwa na nchi zote za Jumuiya ya Madola, ambapo mtuhumiwa yoyote anahesabika "innocent until proven guilt", hivyo ni makosa kupiga picha zozote ndani ya chumba cha mahakama!, ni kinyume cha sheria, hivyo polisi kwa upande mmoja wako right!.

Kwa upande mwingine, ni polisi hao hao huwa wanaruhusu picha zipigwe mahakamani kwa baadhi ya kesi zinaitwa "public interest cases" hivyo hiyo kesi ya mauaji ya Daudi Mwangosi, nayo ni public interest case yenye haki zote kwa kamera kuruhusiwa, ila kama polisi wanazuia kamera kwa sababu mtuhumiwa ni polisi mwenzao, then polisi hawako right!.

Mimi binafsi msimamo wangu ni tuitekeleze sheria kama ilivyo, lengo la kuzuia picha mahakamani, ni ili kuzuia, kuwahukumu kwa picha hivyo kuingilia uhuru wa mahakama!.

Pasco.
 
Wanaingilia uhuru was viombo vya habari kwanini polisi wetu hawa hawaelimiki.shule nayo inasaidia.kwenye matukio wanaita vyombo vya hbri kova kila cku na wanahabari wanahabari wangewasusia.shughuli za polisi zote tuone kova atauza sura wapi
 
Hakuna sheria inayozuia picha mahakamani! si juzi tu tumemuona Madabida wa CCM na ARV zake feki? au haikuwa mahakamani?
 
Tanzania ni nchi inayofuata mfumo wa sheria wa Westminster, unaofuatwa na nchi zote za Jumuiya ya Madola, ambapo mtuhumiwa yoyote anahesabika "innocent until proven guilt", hivyo ni makosa kupiga picha zozote ndani ya chumba cha mahakama!, ni kinyume cha sheria, hivyo polisi kwa upande mmoja wako right!.

Kwa upande mwingine, ni polisi hao hao huwa wanaruhusu picha zipigwe mahakamani kwa baadhi ya kesi zinaitwa "public interest cases" hivyo hiyo kesi ya mauaji ya Daudi Mwangosi, nayo ni public interest case yenye haki zote kwa kamera kuruhusiwa, ila kama polisi wanazuia kamera kwa sababu mtuhumiwa ni polisi mwenzao, then polisi hawako right!.

Mimi binafsi msimamo wangu ni tuitekeleze sheria kama ilivyo, lengo la kuzuia picha mahakamani, ni ili kuzuia, kuwahukumu kwa picha hivyo kuingilia uhuru wa mahakama!.

Pasco.
Ila kwa utaratibu wa kenya ndio mzuri hadi video na si mahakama za chini tu hadi mahakama kuu.Hakuna rongorongo nyingi, hata nchi za ulaya nyingi hawafanyi hivyo!!!!
 
Back
Top Bottom