BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,355
- 8,043
Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mwanafunzi wa Shule ya Sheria kwa Vitendo (Law School of Tanzania – LST), Alexander Barunguza, ambayo ameiomba mahakama iruhusu mwenendo wake utangazwe mubasahara kwenye vyombo vya habari, imepangiwa jopo la majaji watakaoisikiliza.
Akizungumza na Mwananchi, leo jana, Septemba 14,2022, Barunguza amesema amepata hati ya wito kwa wadaiwa na kwamba imepangwa kusikilizwa na jopo la majaji watatu litakaloongozwa na Jaji Deo Nangela. Majaji wengine katika jopo hilo ni Ephery Sedekia Kisanya na Dk. Theodora Mwenegoha.
“Pia kesi imepangwa kutajwa Septemba 16, saa 8 mchana. Tayari nimeshapokea summons (hati ya wito wa mahakama), kwa ajili ya kuwapelekewa (wadaiwa) respondentsm,” amesema Baranguza.
Barunguza mwenye usajili namba SLT/2019/30/104 chuoni hapo, amefungua shauri la kikatiba Mahakama Kuu Masjala Kuu dhidi ya Shule hiyo ya Sheria, Jaji Dk. Benhajj Masoud (mkuu wa shule hiyo ya sheria) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Katika Shauri hilo la kikatiba namba 11 la mwaka 2022, Barunguza anapinga matokeo ya mitihiani yake ya muhula wa kwanza na wa pili mwaka 2019/2020 ambayo yanaonesha kwamba ameshindwa kufikisha alama za ushindi katika kozi mbili.
Anapinga kanuni na taratibu za rufaa baada ya rufaa yake ya kupinga matokeo ya mitihani hiyo, kuwa ni kinyume cha Katiba na kwamba katika mchakato wa rufaa yake hiyo ilyotupiliwa mbali hakupewa haki ya kusiklilizwa.
Vilevile anadai kuwa haki zake ya kuishi na usalama zimekiukwa au zinaelekea kukiukwa kutokana na kutishiwa maisha na mmoja wa walimu chuoni hapo wakati akiwa katika mchakato wa rufaa ya kupinga matokeo hayo, huku akidai kutengwa, kubaguliwa na kutokutambuliwa kama mwanafunzi.
Kufuatia kesi hiyo, Barunguza amemwandikia barua Jaji Kiongozi akiomba aridhie wakati wa usikilizaji wa shauri hilo tangu liendeshwe mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Barua hiyo ya juzi Jumanne, Septemba 13, 2022, anaeleza anaomba kesi hiyo iendeshwe mubashara ili kutoa fursa kwa ndugu na marafiki zake walioko nje ya nchi kufuatilia.
“Ninaomba mahakama yako Tukufu, kuruhusu na kuridhia kurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja au mubashara (live) ya mwenendo wa shauri hili tangu siku ya kwanza ya shauri hili litakapotajwa na kuanza kusikilizwa,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.
Hata hivyo, anabainisha lengo la kuomba kesi hiyo iendeshwe mubasahara kuwa ni ili kutoa fursa kwa ndugu, marafiki na jamaa zake waishio nje ya nchi washriki kwa nji ya mtandao na vyombo vya habari kushuhudia yanayojiri katika shauri hilo.
Amezitaja baadhi ya nchi hizo waliko ndugu marafiki na jamaa zake hao kuwa ni pamoja na ngu waishio Marekani, Sweden, Lebanon na Afrika Kusini.
“Aidha ili kuhakikisha zoezi hili linafanyika kwa ufanisi mkubwa na kwa wakati, nimeandaa timu yangu ya wataalamu wa IT (Teknolojia ya Habari), ambao wako tayari kuanza kazi yao mara moja katika kurusha matangazo ya shauri hili.”anasema Barunguza na kuongeza:
“Pia niko tayari kutoa ushirikiano wote na wa kutosha pale ambapo mahakama itapendekeza njia tofauti ili kuhakikisha ndugu, rafiki na jamaa zangu waishio ughaibuni kuweza kupata matangazo ya moja kwa moja ya shauri hili kutokea mahakamani.”
“Aidha shauri hili ni la kikatiba na linahusisha kuvunjwa (zinazoelekea kuvunjwa) kwa haki zangu za binadamu ikiwemo haki ya kuishi au kuwa hai pamoja na usalama wangu (right of life and safety.”, anasisitiza Barunguza kwenye barua hiyo.
Hata hivyo uongozi wa mahakama bado haujatoa majibu ya maombi yake katika barua hiyo kuhusu kesi hiyo kuendeshwa kupitia vyombo vya habari mubashara iwapo utamkubalia au la.
MWANANCHI