Kesi ya Mpendazoe Vs Dk. Mahanga itaanza rasmi kusikilizwa Mei

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
na Happiness Katabazi



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mei 25, 26 na 27 itaanza rasmi kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge jimbo la Segerea uliofanyika mwaka jana yaliyomtangaza Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, kuwa mbunge, iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya (CHADEMA), Fred Mpendazoe. Mbali na Dk. Mahanga washtakiwa wengine ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo.

Katika madai yake mlalamikaji ambaye ni Mpendazoe anataka Mahakama Kuu itengue ushindi wa Dk. Mahanga kwa kuwa taratibu za sheria ya uchaguzi ya mwaka 2010 hazikufuatwa.

Kwa mujibu wa hati ya wito wa kuitwa mahakamani iliyotolewa na mahakama hiyo ambayo gazeti hili limefanikiwa kuona nakala yake, wahusika wa pande zote katika kesi hiyo wameshapewa nakala ya wito huo, wakitakiwa kufika mahakamani hapo siku hiyo mbele ya Jaji Ibrahim Juma.

Kwa upande wake wakili wa Mpendazoe, Peter Kibatala, alilithibitishia gazeti hili jana kwamba tayari ameshapokea wito huo kwa niaba ya mteja wake na kwamba watafika bila kukosa siku hiyo ambapo kesi yao itaanza kuunguruma rasmi. Kesi ya Mpendazoe ni kesi ya kwanza kati ya kesi tisa za kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa mwaka 2010 kufikia hatua hiyo ya juu ya kuanza kusikilizwa. Kesi nyingine za aina hiyo bado ziko katika hatua za awali mbele ya Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.
 
Back
Top Bottom