Ochu
JF-Expert Member
- May 13, 2008
- 976
- 47
Kesi ya wizi wa mkufu na simu ya mkononi iliyokuwa ikimkabili mke wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Naziri Karamagi, Nadia imeyeyuka baada ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kuifutilia mbali.
Akitangaza kufutwa kwa kesi hiyo, hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo John Msafiri alisema, Mahakama yake imefikia hatua hiyo baada ya mlalamikaji Bi. Maselina Rweymamu kuiomba mahakama ifute shitaka hilo...Mlalamikaji aliwasilisha hati ya kuiomba mahakama kukufutia kesi, kwa hiyo tunakueleza kuwa kesi yako imefutwa subiri taratibu zingine za kimahakama utakazotakiwa kufuata, Msafiri alimweleza Nadia .
Awali, mwendesha mashtaka wa Polisi Nassoro Sisiwayaa alidai mahakamani hapo kuwa, Bi. Rweymamu aliiomba mahakama hiyo kumfutia kesi Bi. Nadia ili wamalizane nje ya mahakama.
Mke wa Karamagi ambaye ni mzungu mwenye asili ya kirusi aliburuzwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo Juni 26, mwaka huu akikabiliwa na tuhuma za wizi.
Katika kesi hiyo ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa Polisi Nassoro Sisiwayaa kuwa, Juni 17 mwaka huu saa 5 asubuhi maeneo ya Oysterbay Jijini Dar es Salaam Nadia aliiba mkufu wa dhahabu wenye thamani ya Sh.90,000 na simu ya mkononi yenye thamani ya Sh.155,000 mali ya Maselina.
Hata hivyo, Nadia ambaye ni meneja wa mgahawa Colossian uliopo Jijini Dar es Salaam alikana mashitaka hayo na kuachiwa kwa dhamana hadi jana kesi yake ilipofutwa.

Last edited: