Kesi ya mbunge Badwel yaanza kusikilizwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya mbunge Badwel yaanza kusikilizwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Sep 5, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeeleza jinsi walivyoweka mtego na kufanikiwa kumnasa, Mbunge wa Bahi, Omary Badwel (CCM) na rushwa.

  Akitoa ushahidi wake jana mbele ya Hakimu Faisal Kahamba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Ofisa wa uchunguzi kutoka TAKUKURU, Mkoa wa Pwani, Janeth Machulya, alidai waliamua kuweka mtego baada ya kujiridhisha na taarifa alizopewa kutoka kwa mlalamikaji ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Sipora Liana.

  Machulya alidai waliweka mtego wa fedha taslimu sh milioni moja, vinasa sauti, gari pamoja na vifaa vingine, ili kuweza kukamilisha mchakato huo.
  Huku akiongozwa na Wakili wa Serikali, Willa Haonga, shahidi huyo alidai Liana alimueleza kuwa mshtakiwa alimtaka wakutane Mtaa wa Lumumba, CCM, ambapo yeye alimwambia abadilishe eneo la kukutana.
  “Nilimwambia amwambia mshtakiwa wakutane katika Hoteli ya Peacock, Kasuku Bar, kwa sababu ni karibu na Mtaa wa Lumumba CCM,” alidai shahidi huyo.

  Alidai walipokuwa njiani kuelekea katika hoteli hiyo, Badwel alimpigia simu Liana akimuhimiza afanye haraka, naye Liana akamwambia dakika chache atakuwa ameshafika.
  Shahidi huyo alidai mawasilano hayo alikuwa akiyasikia na kwamba baada ya kufika Liana alishuka kwenye gari na kuelekea ndani ya hoteli hiyo, ambapo alidai kuwa timu ambayo alikuwa nayo katika kuchunguza suala hilo nao walikuwa wameshaingia ndani.

  Alipoulizwa na Haonga kuwa kwanini aliamua kubaki nje, alidai kuwa kiuchunguzi alitakiwa abaki nje, pia kwa usalama wa fedha sh milioni moja ambazo ziliwekwa mtego.
  Machullya alidai Liana alipotoka nje ya hoteli kwa mara ya pili aliambiwa na Badwel kuwa anahitaji sh milioni nane ili aweze kuwapatia wajumbe wengine wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) sh milioni moja kila mmoja.

  “Wajumbe wa kamati hiyo wako 15, lakini wajumbe wanane wao ndio wapo katika ule mtandao wa hesabu na kati ya hizo sh milioni 8, Badwel na yeye angepata sh milioni moja,” alidai shahidi.
  Hata hivyo shahidi huyo alidai kuwa Liana alimwambia Badwel kuwa kwa wakati huo hana fedha hizo, lakini anacho kiasi kidogo, nilimpa sh milioni moja zikiwa ndani ya bahasha ya kaki akarudi tena ndani.
  Pia Badwel alimwambia Liana kuwa kiasi cha fedha kilichobaki amuingizie kwenye akaunti namba yake ambayo ni 5051602671 NMB, ambapo aliifungulia mkoani Dodoma Mei 5, mwaka 2008.

  Machullya alidai alipoingia ndani ya hoteli hiyo alimkuta mshitakiwa ameshawekwa chini ya ulinzi na ile timu iliyoingia ndani ya hoteli hiyo na kuanza kuhakiki fedha hizo.
  Hata hivyo, shahidi huyo alidai waliendelea kujiridhisha kama kweli mshitakiwa alikuwa na nia ovu na kwamba walipochapisha mawasiliano waliona kuwa ni kweli kulikuwa na mawasiliano kati ya namba ya Liana na Badwel. Alidai namba zilizokuwa zikitumika ni 0784 858855 ambayo ni namba ya mlalamikaji na 0789 089189 namba ya Badwel.

  Baada ya ushahidi huo, Hakimu Kahamba aliahirisha kesi hadi Oktoba 10 itakapoendelea kusikilizwa.
  Katika kesi hiyo, Badwel anadaiwa kuomba rushwa ya sh milioni nane kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Sipora Liana. Ilidaiwa alitenda kosa hilo kwa wakati tofauti kati ya Mei 30 na Juni 2, mwaka huu katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

  Katika shitaka la pili, mshitakiwa huyo anadaiwa Juni 2, mwaka huu katika Hoteli ya Peacock, Dar es Salaam alipokea rushwa ya sh milioni moja kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.


  Wakati huo huo, upelelezi wa kesi ya kudharau amri ya Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na kuwashawishi madaktari kugoma inayomkabili Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MALT), Dk. Namala Mkopi umekamilika.
  Wakili wa Serikali, Willa Haonga, alidai jana mbele ya Hakimu Faisal Kahamba kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika na kuomba tarehe ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali.

  Kahamba alikubaliana na ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Septemba 27, mwaka huu.
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Rushwa kubwa ya rada vipi?
   
Loading...