Kesi ya Mbowe Novemba 4, 2021: Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Sebastian Madembwe atoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Novemba 5, 2021

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Baada ya jana kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani. Jana kesi iliahirishwa kutokana shahidi kupata dharura ya kiafya na upande wa utetezi haukutoa kikwazo chochote kwenye sababu hiyo. Jaji aliahirisha mpaka leo. Kuwa nami.

==============

Jaji ameingia.

Kesi inatajwa

Robert Kidando anatambulisha Jopo lake

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Tulimanywa Majige

Peter Kibatala anatambulisha Jopo la mawakili wa utetezi

Peter Kibatala
John Malya
Fredrick Kiwhero
Dickson Matata
Idd Msawanga
Nashon Nkungu
Maria Mushi
Khadija Aron

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri lina kuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja Tupo tayari kuendelea

Wakili wa Serikal: Mmoja anatoka kwenda Kumfuata

Jaji: upande wa Utetezi

Wakili Peter Kibatala: Na sisi pia tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi Wenu?

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ameenda Kufuatwa Anaingia Shahidi Mfupi Kavaa Kaunda

Jaji: Majina yako

Shahidi: SSP Sebastien Madembwe

Jaji: umri

Shahidi: 46

Jaji:
Kabila

Shahidi: Mhehe

Jaji: Shughuli zako

Shahidi: Afisa wa Polisi

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkrito

Shahidi: Mimi SSP sebastian Madenge Naapa Kwamba Ushahidi nitakaotoa ni Kweli tupu Eeeh Mwezi Mungu nisaidie

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ataongozwa na Wakili wa Serikali Pius Hilla

Wakili wa Serikali: Shahidi umesema Majina yako kwa ukamilifu ni nani

Shahidi: SSP sebastian Madenge

Wakili wa Serikali: Unaishi Wapi

Shahidi: Iyumbu Kule Dodoma

Wakili wa Serikali: Mkazi wa Dodoma tangu lini

Shahidi: Mwezi wa Nane 2020

Wakili wa Serikali: Kabla ya hapo ulikuwa unaishi Wapi

Shahidi: Nilikuwa naishi Muongo la Ndege Ukonga, Nikiwa Ofisa wa Polisi Makao Makuu, iliyokuwa Makao Makuu Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Uliajiliwa lini kama Polisi

Shahidi: 02 Mwezi 09 Mwaka 1999

Wakili wa Serikali: Katika Jeshi la Polisi Upo kamisheni gani

Shahidi: Nipo kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai

Wakili wa Serikali: Kitengo Gani

Shahidi: Udhibiti na Usajili wa Silaha

Wakili wa Serikali: Kwa Kizungu Mnaitaje

Shahidi: Arms Management and Registration Unit

Wakili wa Serikali: Kitengo hilo kina husika na Nini

Shahidi: Usajili wa Silaha za Raia Utoaji wa Leseni za Kumiliki silaha Kibali Vya Kuingiza Silaha Nchini Vibali Vya Usafirishaji wa Silaha na Risasi Hapa Nchini

Shahidi: Vibali Vya Upotoshaji wa Silaha zinazoenda Nchi mbalimbali kupitia Kwetu Tunatoa Vibali Vya Uuzaji wa Silaha na Risasi Yote yanahusiana na Usajili wa Silaha Tunahusika pia na Nchi Mbalimbali katika Udhibiti wa Silaha katika Kutekeleza Mikataba ya kikanda na Kimataifa

Wakili wa Serikali: Umesema Usajili wa Kiraia Je Unamaanisha Nini Shahidi: Ni zile Silaha zilizoruhusiwa Kwa Mujibu wa Sheria namba 02 ya Mwaka 1995 Sheria imetaja Silaha zinazoruhusiwa ni Pistol, Riffles, Short gun na Silaha yoyote ambayo Bodi ya Udhibiti wa Silaha itapendekeza iingie Miongoni Mwa silaha za Kiraia

Shahidi: Samahani Mheshimiwa Jaji, Silaha Nyingine ni Gobole

Wakili wa Serikali: Silaha Ndogo na nyepesi Fafanua hapo

Shahidi: Udhibiti Wa Silaha hizi tunazomiliki za Kiraia, Silaha Ndogo Ndogo ni zile ambazo Mtumiaji ni Mtu Mmoja. Kwa Mfano AK47 ni Silaha Ndogo Lakini Silaha Nyepesi yani Light Weapon ni Ile ambayo inatumika kwa Urahisi

Wakili wa Serikali: Kwenye Kitengo wewe ni nani

Shahidi: Ni Mrajisi Wa Leseni za Bunduki

Wakili wa Serikali: Kwa Kizungu

Shahidi: ni CEO arms Register

Wakili wa Serikali: Majukumu yako wewe ni Yapi

Shahidi: Ni Kuhakikisha kwamba napokea Maombi yote ya Waombaji wanataka Kumiliki silaha, Yaliyopitishwa na Kamati za Ulinzi na Usalama Kuanzia ngazi ya mtaa ambalo Mwombaji anaishi, Kata, Wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama Ya Mkoa

Wakili wa Serikali: Jukumu la Pili..?

Shahidi: Kuyakagua Maombi hayo niliyoyapokea ilikuina kama Yana Vigezo kwa Mujibu wa Sheria, Licha ya Kwamba Maombi hayo yatakuwa yamepitishwa kwenye Kamati nilizozitaja Na Kwamba Maombi Yaliyokodhi Vigezo huendelea Kuya Shughulikia Ngazi inayofuata

Maombi Yaliyokidhi Vigezo nayarudisha yalikotoka Kutoa Vibali Vya Uuzaji wa Silaha hapa Nchini, Kibali cha Usafirishaji WA Silaha hapa Nchini na Upitishaji Vibali kwenda Nchi Jirani hasa wanatumia Bandari yetu Tunatoa Vibali Vya Kutunza Silaha (Warehouse License)

Shahidi: Tunatoa silaha Gunsmith Lisence (Kibali Cha Kufanyia Matengenezo silaha kwa Raia endapo itapata hitilafu Na Pia kutoa Leseni kwa wale waonataka Kumiliki Silaha Kutunza Kumbukumbu ya Silaha na Wamiliki wote ambao wamesajiliwa

La Mwisho ni Kupokea Maombi ya Kiuchunguzi pale silaha Inapo okotwa Ili tuweze Kuangalia Kwenye Data Base Kama Silaha hiyo imesajiliwa Au lah

Wakili wa Serikali: Mbali na Maombi hayo, Maombi Mengine huja kwa Namna gani

Shahidi: Ninapozumgumzia Uchunguzi no Uchunguzi wa Taarifa

Yoyote inayohitajika kwa ajili ya Shughuli ya Kiupelelezi, Ni Kitengo Kinacho Support Upelelezi katika Maswala ya Silaha

Wakili wa Serikali: Moja ya Jukumu umesema kutoa Vibali au Leseni za Umiliki wa Silaha Je Mchakato Ukoje Utaratibu wa Mpaka Mtu apewe Leseni

Shahidi: Wa Kwanza ni Kupokea Maombi ambayo yamepitishwa katika Kamati za Ulinzi na Usalama

Wakili wa Serikali: Kabla ya Hilo anaanza na Jambo gani Shahidi Ni Kununua Silaha, anaweza Kununua Katika Vyanzo Vitatu 1. Kwenye Duka ambalo wamepewa Leseni ya Kuuza Silaha (Lisenced Dealer)

2. Kwa Kununua kwa Mtu aliyekuwa anamiliki hiyo silaha Kihalali kwa kuandikishiana Mkataba wa Kisheria Na Kama Silaha ya Mirathi basi Kikao cha Ndugu wa Marehemu Kitakaa chini ya Mwenyekiti ambaye atakuwa amepitishwa na Mahakama Kwamba ni Msimamizi wa Mirathi kwamba ni nani wa Kuirithi Silaha hiyo Endapo wataamua Basi Mrithi anaweza Kumiliki Mwenyewe Kwa Utaratibu wa Kisheria au Kuuza Lakini Mrithi atahakikishq Kwamba Mteja anaye Muuzoa anamkabidhi Nyaraka zote za Mirathi pamoja na Mkataba walioandikishana Kisheria

3. Muombaji anaeleza Kununua Nje ya Nchi kwa Kuomba Kibali cha Kuingiza Hiyo silaha Nchini (Import Lisence) iwe Bandarini au Uwanja wa Ndege TASAKI ndiye atahusika Ku Clear hiyo silaha na Kuhifadhi wakati Muhusika ataendelea na Taratibu za Kuomba Kumiliki Silaha Hiyo

Shahidi: Kwa hiyo katika Vyanzo Vyote VitatuSilaha utatakiwa kuwa Kwenye Ghala, yeye atakuwa na Nyaraka za Mauziano ili ziweze Kumsaidia kama attachments katika Maombi yake Zipo fomu za Umiliki wa Silaha Kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni zinaitwa Fomu A

Mwombaji hupaswa kuzijaza na Kuambatisha Nyaraka zote zinazoomyesha Chanzo cha Silaha hiyo Ata attach Fomu za Silaha hiyo, Kama Mfanya Biashara basi Leseni ya Biashara, Kitambulisho Cha Taifa na Nyaraka yoyote ile itakayodhibitisha Anamatishio Kutokana na Kazi anayofanya

Wakili wa Serikali: Inaambatana na nini hiyo fomu Ni lazima Kuwa muhtasari Kuanzia Ngazi ya Mtaa, Kata, Wilaya na Mkoa Wakili wa Serikali: Kingine?

Shahidi: Hati ya Tabia Njema inayotolewa na Jeshi la Polisi kupitia Kitengo cha

Kibatala: SAMAHANI Mheshimiwa Jaji Naomba Kwanza Kumuombea Wakili Jeremiah Mtobesya Aweze Kuingia Kwenye Orodha yetu Ambaye kachelewa Kwa sababu nilizotoa Mwanzoni Baada ya hayo nitaomba Sasa Wakili Mtobesya aweze kusema alichotaka

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Shahidi hana Maelezo katika Kifurushi cha Comito Kwa hiyo Ushahidi wake Hauwezi Kuingia Kwa Mujibu wa Kifungu cha 246 cha CPA Hakuna Maelezo yake, na Nimeulizana na Wenzangu Kama Upande wa Mashtaka Uliomba Mwanzoni Ombi lolote nimeambiwa Hapana

Mahakama Kimyaaaaaaa!

Upande wa mashtaka ni kama wamebutwa fulani hivi.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Tutaomba Pia Maelekezo endapo Wenzetu watafanya Kwa Usahihi, Vipi kuhusu Ushahidi ambao Shahidi ameshaanza kuutoa hapa Mahakamani?

Mtobesya: Na ninataatifiwa hapa na kaka yangu, shahidi anatakiwa aondoke na ushahidi wake tuendelee na ushahidi Mwingine kwa Sababu hawawezi kupata faida baada ya sisi kusema kama wao hawakuomba mwanzoni Mawakili wa Serikali: Wananong'onezana Jaji anainama na kuandika

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ombi hilo halina mashiko yoyote ya kisheria

Jaji: maombi au pingamizi

Wakili wa Serikali: Ahaaa pingamizi, halina mashiko yoyote ya kisheria Sababu limeletwa katikati ya ushahidi Wa PW6 kinyume na sheria

Na Kama wangekuwa na hoja hiyo walitakiwa kufuatilia mapema, Lakini kwa wakili ambaye hakufuatilia tangu mapema proceedings hizi, Hoja yetu ya Pili ni kwamba Shahidi huyu aliorodheshwa tangu Kipindi Cha Committal Proceedings na anasomeka Kama Shahidi namba 23 tangu Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu Na hata katika Barua yetu ya 11 August 2021

Wakili wa Serikali: Ukurasa wa 32 na Jina lake linaonekana Katika 23 Labda lile neno S liondoke isomeke Sebastian

Wakili wa Serikali: Lakini Substance ilikuwa Committed na Ilisomwa Katika Mwenendo wa Shauri hilo katika Proceedings za Tarehe 23/8 Siku ambazo COMMITTAL Proceedings zilifanyika Na Jina lake limeandikwa sebastian Madembwe SSP

Lakini pia Katika Ile list ya Exhibit katika Ukurasa wa 33 Nyaraka Anayokuja Kuzungumzia imekuwa Litsted pale Namba 18 Ambayo pia imesainiwa na Sebastian Madembwe SSP nilikuwa Committed na Substance yake ilisomwa

Kwa hiyo kwa namna yoyote ile Hatukutakiwa Kuleta Ombi kupitia Kifungu cha 289 cha CPA ili Shahidi huyu aweze Kutoa Ushahidi Wake.. Na tunasema Pia Matakwa ya Rule 8 Sub 2 ya The Economic and Organized Crime Control (Corruption and Procedure Rules ya 2016),

Takwa hili la Kisheria lilitekelezwa na Mahakama. Iwe Jina ama Substance ya Ushahidi Anaotoa Leo hii hakuna Kitu Kipya kama Ambavyo wakili anajaribu Kuonyesha Mahakama yako Tukufu Na Kama hali Iko hivyo hakuna Haja Wa Kutoa Amri yoyote ile Kutokana na Ushahidi ambao Umeolewa na Shahidi Kwa sababu Shahidi Yupo Sahihi Kwa Mujibu wa sheria Hivyo Mheshimiwa Jaji tunaomba hilo Pingamizi ulitupilie Mbali ili Shahidi wetu aweze Kuendelea na Ushahidi Wake

Jaji anaandika Kidogo

Mtobesya: Kwanza Kabisa Wenzangu wameni attack, Personally Sikuwepo Kwenye Proceedings tangu Mwanzo, Mimi Kuchelewa Kufika sidhani kunaweza Kuathiri. Sisi tunachofanya hapa ni Kuisaidia Mahakama Kufanya Shughuli Zake Kwa Mujibu wa Sheria

Mtobesya: Nimesema Kwenye Committal Documents hakuna Ushahidi wa shahidi i huo. Substance inaongelea mambo matatu. 1. MAJINA Ingawa yamekosa hatuna Shida na hilo, 2 Cheti atakachotoa na 3. Hakuna Kile ambacho "Ataongea nini Mbele ya Mahakama"

Mtobesya: Tumeongea mara Nyingi kuhusu hili Kuwa kuna Sababu Ipo ya Kumpatia Mtu Nyaraka za Ushahidi kupitia Committal, Na Wasipokuwa wamefanya Upo Mlango Mwingine wa wao Kuomba kupitia Kifungu cha 289 Criminal Procedure Act

Wakili wa Serikali: Kama namwelewa Mtobesya anazumgumzia % Documents kutosomwa

Jaji: kama nimekuelewa umesema haipo kwenye Committal Bandle!

Mtobesya: Nimesema haipo kwenye Committal bundle kwa maana hiyo haijakidhi matakwa hayo ya kwenye 246 CPA

Jaji: Umeridhika na line yake ya argument sasa
Wakili wa Serikali: Hapana Sikubaliani na Mtobesya. Yeye ana argue kwamba haijasomwa, Maana akianza kujielekeza kwenye mengine na mengine inakuwa siyo sawa

Jaji: Hoja yao ni Kwamba argue kwa namna ambayo umeletea pingamizi

Mtobesya: Kwasababu Haipo ina maana haijasomwa, na kwa sababu haijasomwa inakiuka sheria aliyosoma Kaka yangu Kidando ya uhujumu uchumi na makosa ya uchumi ya mwaka 2016 Kingine Kaka Yangu anasema P. O imeletwa Kinyume na Sheria Kwa sababu Ilishapitwa

Hiyo siyo Sawa, Jambo lolote linaweza Kuibuliwa pale tu tunapoona tunaenda Kinyume na Sheria, tunalo hilo Jukumu Kama Wawakilishi wa wateja wetu na Pia kama Maafisa wa Mahakama Kwa hiyo kama ilivyoombwa Mwanzoni Mahakama Itoe Maelekezo na Kukidhi Matakwa YA Sheria. Ni hayo tu

Jaji anainama na kuandika kidogo

Jaji: Mmesikia hoja zote, Naomba nipate muda na mimi Tutarudi tena hapa saa tano na robo. Anasimama na kutoka nje ya chumba cha mahakama

Jaji alitoka Mahakamani 10:50 saa za Afrika Mashariki, akasema atarudi saa 11:15 ili akapitie sheria ambazo zimetajwa. Sasa ni saa 11:52 na bado hajarejea katika chumba cha mahakama. Tunaendelea kusubiri.

Jaji Ameingia 12:00 Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe imetajwa tena

Wakili wa Serikali: Upande wa Jamhuri tupo tayari na Hakuna Mabadiriko ya column

Kibatala: Na sisi Pia Mheshimiwa Jaji tupo vizuri

Jaji: Tuli' break Kwa muda Kwa nia ya kuandika maamuzi madogo, maamuzi yanalenga kutatua mgogoro wakati shahidi namba 06 anatoa ushahidi Mtobesya alieleza mahakama shahidi huyo anakiuka kutoa ushahidi wakati ushahidi wake haukuwa umesomwa kwenye committal mahakama ya Kisutu

Na akaeleza Kuwa hivyo Inakiuka Kifungu 246 cha Sheria 8 Sub ya CPA Sura ya 20 Na Pia GN 267/2017 na Kifungu cha 63 cha CPA na Sheria Ya Uhujumu Uchumi

Jaji: Hivyo Inakiuka Haki ya Washitakiwa na wao Kama wawakilishi Wa Washtakiwa Kutokuona Nyaraka hiyo na Pia Kwamba Haikusomwa Anaomba Mahakama imkatae SHAHIDI na Ushahidi Wake utupwe Upande wa Serikali Walikuwa na Hoja Mbili

1. HAINA Mashiko Kwa sababu Pingamizi limekuja Kwa Kuchelewa 2. Ushahidi wa Ushahidi Huo (Substance) ni sehemu ya Ushahidi tu, Mahakama Ijeielekeze Ukurasa wa 33 ambapo Inaonyesha Ushahidi Wake Ulisomwa Mahakamani

Akaongeza Kuwa Ushahidi Ambao unakuja Kutolewa Mahakamani Unakuwa Umesomwa basi Shahidi anatakiwa kuendelea Kutoa Ushahidi Wake Na Kwamba Kanuni zilifuatwa kama ambavyo imefanyika Kwenye Mahakama ya HAKIMU Mkazi Kisutu

Jaji: Mtobesya kwenye Kuhitimisha Hoja ya Serikali ya Kuchelewa haina Mashiko Yoyote, Pingamizi Linaweza Kuletwa Wakati wote wote Ni Jukumu la Upande wa Mashtaka Kutoa Nyaraka Mapema na Orodha Ya Watu wanaopangwa Kufanya Ushahidi Mahakamani

Jaji: Anaomba Mahakama Itamke Shahidi amefika Kinyume na Sheria na Ushahidi alitoa Upo Kinyume na Sheria Na Kwamba Disclosure ni kwamba Mahakama itumie Hivyo kama Msimamo wake

Jaji: Sasa Katika Hukumu nitatumia Sheria zilizotaja hapo Juu Pande Mbili wanakubaliana kuwa Malengo Mahususi Ni kwamba Ushahidi Unaokuja kutolewaa Mapema Unajulikana Mapema Ushahidi Wote Unaotakiwa Kuja Mahakama Kuu Unatakiwa Kujulikana

Moja kwa Kusomwa Kwa Kuandaliwa Kwa Mfumo wa kitabu na Kukabidhiwa Majukumu haya yanafanywa na Upande wa Mashtaka Kusambaza Ni kazi ya Mahakama Pingamizi lolote linaweza Kuja wakati wowote Pale anapogundua Kuwa kuna Mapungufu anaweza Kuleta Mahakamani

Jaji: Ni Msimamo wa sheria Kuwa pale ambapo Ushahidi unakuwa haujasomwa basi hauwezi kupokelewa mahakamani labda kama wataomba kama ilivyoelezwa na Wakili Mtobesya kwenye Kifungu cha 289 CPA Jambo linalobishaniwa ni kwamba ushahidi haukusomwa hapa mahakamani

Jaji: Mahakama inayo Jukumu la kukagua Kama Ushahidi Kama Ulisomwa au Haukusomwa Mbele Ya Hakimu Mkazi wa Kisutu wakati Wa Committal Inasomwa Mahakama Wakati Ina Examine Record Imeona Kwenye Ukurasa wa 21 Maneno Yafuatayo Kwamba Ushahidi Na Mashahidi Yamesomwa kwa Washtakiwa

Akasema Hakimu Simba Tarehe 23 08 2021 Akaorodhesha Mashahidi 21 na Jina la Shahidi Namba 06 linaonekana Katika Ukurasa wa 31 Na Kwamba Mashahidi hao waliorodheshwa na Maelezo yao yalisomwa Mbele ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Huo ndiyo Msimamo na Kumbukumbu za Mahakama

Kwamba Maelezo yote yalisomwa na Kwamba Ushahidi huo Ukisomwa Na Mahakama haikuishia hapo Kama Nilivyosema Katika ku' Examine Mahakama Ikaona Kuna Maelezo Ya Shahidi namba 06 Kumbe yalisomwa na Kwamba Tatizo Maelezo hayo hayakuunganishwa Katika Kifurushi cha Comito Proceedings

Jaji: Kutokwemo Katika kifurushi haimaanishi Ushahidi Wa shahidi Namba 06 haukusomwa Mahakama Inaona Pingamizi Halina Mashiko Lengo la Pingamizi Ilikuwa Ku Impeach Record za Mahakama Maelezo Yalipo Mahakamani Yana onyesha Ushahidi Ulisomwa hivyo naelekeza Sasa Shahidi Aendelee

Mawakili Wote wanamyanyuka Ishara ya Kukubaliana na Jaji

Jaji: Mara Ya Mwisho alisema huyo Mwombaji lazima awe na Cheti cha Tabia Njema kutoka Jeshi la Polisi

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Iwapo zipo Nyaraka zingine zinaambatanishwa na Maombi

Shahidi: Zile zinazo onyesha Mwombaji kuwa Upo Umuhimu wa Yeye Kumiliki Silaha Vielelezo anavyoweza Kuambatanisha ni Ile kazi anayofanya WS: Maombi ya kisha wakilishwa

Shahidi: Yakishawakilishwa kwangu nayakagua ili Kujiridhisha Kama Yanakidhi Vigezo Vilivyowekwa Kwa Mujibu wa Sheria

Wakili wa Serikali: Ka Maombi hayajakidhi Vigezo nini hufanyika

Shahidi: Mambo Mawili hufanyika 1.Yanaweza Kurudihswa Kwenye Mkoa Husika Ilikukamilisha Vigezo Vinavyokksekana 2. Endapo itaonekana Mwombaji hana Sifa zilizo ainiahwa Kisheria na Kwamba hata akirekebisba

Vigezo vianvyopungua basi Maombi hayo ubaki Makao Makuu na Mkoa unaohusika Ujulishwa kuwa Mwombaji hana Sifa

Wakili wa Serikali: Maombi Yanayokidhi Vigezo? Nimi hufanyika

Shahidi: NiKumjulisha Mwombaji Kwamba amekubaliwa

Wakili wa Serikali: Kwenye Barua hii husika Muhisika atakiwa nini

Shahidi: Mwombaji anajulishwa Kuwa Maombi yake yamekubaliwa anatakiwa kwenda Kwa Mkuu Wa Wilaya Kwenda Kukamilisha Malipo Na Baada ya Kukamilisha Malipo arudi Katika Ofisi ya Mrajisi Akiwa na Barua aliyopewa ya akumjulisha kuwa ameruhusiwa Kumiliki Silaha Kutoka Ofisi ya Mrajisi ikiwa imeambatanishwa na Risiti ya malipo Ambapo Malipo hayo hufanyika kwa mkuu wa polisi Wilaya

Wakili wa Serikali: Nini tena hufanyika Shahidi: Kama amekamilisha malipo, kinachofuata ni Hatua ya Usajili

Wakili wa Serikali: Unakamilishwaje

Shahidi: Kwa Mambo Mawili Kwanza Kwa kuipa Silaha Husika Registration Number, Central Arm Register Numbe Kwa kifupi tunaita CAA number Ambapo kitabu hicho Chenye CAA namba kitaandikwa Mambo yafuatayo Maelezo ya Silaha ambayo Muhusika ameomba

Wakili wa Serikali: yanapatikana wapi Shahidi: Kwenye Ukurasa wa Kwanza kwenye hicho Kitabu

Wakili wa Serikali: unayapata wapi Mambo ya Kujaza

Shahidi: Ile Barua ya Kumjulisha Mwombaji inakuwa na Maelezo yote Pamoja na Maelezo ya Muhusika yanaingizwa Kwemye Kitabu

Shahidi: Na Kisha Kuandika Picha Kwenye Kitabu hicho Chenye CAA Namba Nitaffungua faili na Kuingiza Document kwenye Faili Na Juu ya faili Nita andika Registration namba yani CAA namba Kwa ajili ya Kumbukumbu

Nilisha Kamilisha Sasa Kusajili Katika Mfumo wa Makaratasi namuingiza sasa Katika Electronic Data Base

Wakili wa Serikali: kwenye Mfumo ni taarifa zipi unazoingiza

Shahidi: Mfumo utanitaka Kuingiza Kwanza CAR namba

Shahidi: Mfumo utanitaka niingize aina ya silaha

Mtengemezaji kwa Maana ya Kampuni iliyotengemeza na Serial Namba Ambayo Mtengemezaji ameigonga Kwenye silaha Husika

Shahidi: Kuna parameters za Nyongeza Kama Nchi ambayo Silaha hiyo Imetengenezwa, Model Namba pamoja na Callibre Size

Hizi parameters nilizo it aja Mwishoni siyo za a Umuhimu sana Bali za Nyongeza Katika Kusaidia Utambuzi

Wakili wa Serikali: Ulizungumzia particular za Mhusika, Ni kitu gani

Shahidi: kwa Ruhusa ya Mheshimiwa Jaji, tunaingiza IDADI ya Risasi ambazo Mmiliki anaruhusiwa Kuzimiliki kwa Wakati Mmoja

Shahidi: Majina, Uraia wake, Jinsi a Yake, Kazi yake, Namba ya Kitambulisho Cha Taifa au Mpiga Kura kwa wale ambao hawana Cha Taifa, Makazi yake Tukiingiza kuanzia Mtaa, Kata anayotaka Mwombaji, Tarafa, Wilaya na Mkoa

Wakili wa Serikali: Kama Kuna Taarifa zingine mnazo ingiza kwa simu

Shahidi: namba ya Simu, anuani ya Barua pepe, Chanzo cha silaha Kama ameinunua

Wakili wa Serikali: Ukiisha Kamilisha Kuingiza Taarifa zote kwenye Mfumo Kinachofuata ni nini Shahidi Kinachofuata ni Kusave, na baada ya kubonyeza Button ya Kusave hakuna Chochote Kitakachokuwa ammended

Shahidi: Kuweka Kumbukumbu, Kurejea Kumbukumbu endapo Silaha itakuwa inatafutwa Pangine imepatikana katika Tukio la Uhalifu ili Kujua inaweza Ikawa Miomgoni Mwa silaha zilizo sajiliwa

Wakili wa Serikali: Nyaraka zipi sasa Muhusika upewa Shahidi Kwa Mujibu wa Sheria kesi ya Udhibiti wa Silaha ya Mwaka 2015 na Kanuni zake za 2016 Mmiliki anacbokabidhiwa ni Kule Kitabu

Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa umesema kumbukumbu za Umiliki kwa Maana Hard copy na Sosty Copy, na Madhumuni ni Ka. MAOMBI ya Uchunguzi wa Silaha yatafanyika Je ni watu gani huketa Maombi

Shahidi: Sisi Upokee Kutoka Kwenye Ofisi inayopeleleza Kwenye Shauri husika

Wakili wa Serikali: Pengine ni wapi

Shahidi: Kwenye Taasisi zinazosimamia Utekelezajibwa Sheria mbalimbali Mfano tumepokea Maombi Kutoka PCCB Kutoka Nna Taasisi inayodhibiti Madawa ya Kulevya

Wakili wa Serikali: Maombi ya Uchunguzi wa Silaha Yanatakiwa Kwmuwa na nini

Shahidi: Yawe na Taarifa 03 za Msingi, Taarifa za lazima au zile za ziada Taarifa ya Kwanza iwe ni Aina ya Silaha Kingine ni Jina la Mtengemezaji (Makers name au Manufacturer name) Namba zilizohongwa na Mtengenezaji (Manufactural serial number) Itatuwezsha Kujua hii silaha Imesajiliwa au Haikusajiliwa

Wakili wa Serikali: Unapopokea Maombi kama hayo unafanyia Nini

Shahidi: Kwanza Tunagongq Muhuri kwamba tumepokea Baada ya hapo tunaanza Kufanyia Kazi

Wakili wa Serikali: Kwa namna gani

Shahidi: Kwa Kuingiza Parameters ya Yale a Maombi katika Mfumo Sababu Parameters ni Unique hata Kama Silaha zimetemgezwa NA Mmiliki huyo huyo bado pan kuwa hakuna Coalition

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kinafanyika Kuwa na Unique Serial Number

Shahidi: Hawa watenhenezajonwanakutana Kupeana kuhusu Serial number na Kuhakikisha Namba haziingiliani

Wakili wa Serikali: Mkishaingiza kwenye parameter kwenye mifumo

Shahidi: Na Click Okey Kama Silaha Imesajiliwa itaketa amatokeo Chanya na ninaweza Sasa Kwenda Kwenye Hard Copy

Wakili wa Serikali: Matokea Hasi ni Yapi

Shahidi: Nilipo ingiza Parameters na Mfumo Kutafuta Nakubaini Hakuna Kumbukumbu zozote katika Mfumo huo

Wakili wa Serikali: Mwisho wa Siku unafanya nini Shahidi Kama Matokeo Chanya Nafanya Mambo Mawili kwenye Taasisi iliyooomba Uchunguzi ufanyike

Nita Print Out Mfumo Umetuleeza Hivi na Itakuwa Kiambatisho Katika Barua Yangu Kama Matokeo Yatakuwa Hasi itaandikwa Barua na Haoatakuwa na Printout Yoyote

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama tarehe 25 Nov 2020 ni Kitu gani Kilitokea

Shahidi: Nikiwa Ofisini Kwangu Makao Makuu Dodoma Nilipokea Barua ya Kufanya Uchunguzi Silaha aina ya Bastola

Wakili wa Serikali: Ilitoka Wapi

Shahidi: Makao Makuu Madogo Police Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Idara Gani

Shahidi: Idara ya Upelelezi Makosa ya Jinai Barua ilinitaka Kufanya Uchunguzi wa Aina Ya Silaha Bastola Mtengenezaji ni Luger na Serial Number A5340

Wakili wa Serikali: Maombi hayo Ukitanyia kazi kwa namna gani

Shahidi: kama ifuatavyo, Kwanza nilijiridha Matokea ya silaha ya

naweza Kunifanya niendelee Nikaingiza parameter kwenye Mfumo Na Matokea yakwa silaha hiyo haijawahi Kusajiliwa

Wakili wa Serikali: Baada ya Matokeo hayo

Shahidi: Niliandika Barua ya Matokeo Ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Uliandika kwenda Kwa nani Shahidi Kwa mwombaji aliyeomba Uchunguzi Kufanyika

Wakili wa Serikali: Ulimueleza Kitu gani

Wakili wa Serikali: Nilieleza Kwamba Kufuatia Uchunguzi uliofanyika, SILAHA HAIJAWAHI KUSAJILIWA

Wakili wa Serikali: Barua Yako uliyoandika Ukiona Utaweza Kuitambua

Shahidi: Nililetewa naweza Kuziona na Kuitambua

Wakili wa Serikali: Utaitambuaje

Shahidi: Nitaitambua Kwa Kuangalia Majina yangu Pamoja na Sahihi yani Siganture

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaonyesha Uwezo wa Kuutambua kwa a ridhaa ya mahakama naomba Kumuonyesha

Wakili wa Serikali: Tizama Nyaraka hii ninayokuinyesha

Shahidi: Nimeiona

Wakili wa Serikali: Mueleze Jaji Nyaraka hiyo ni Kitu gani

Shahidi: Barua niliyo andika Kuonyesha, Sahihi yangu Mwenyewe

Wakili wa Serikali: Kingine Kuna a Majina yangu Pamoja na wadhifa nilionao

Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama

Shahidi: Ni aliomba Mahakama Kwamba Barua hii inayo onyesha Taarifa ya Kiuchunguzi Ipokelewe na Mahakama Kama Ushahidi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomba Nyaraka hii Ipokelewe

Wanapelekewa Mawakili wa Utetezi na wote wanasema hawana pingamizi Sasa anapelekwa Jaji

Jaji: Basi Tunaipokea Barua hii inayoelekezwa kwa ASP Msangi Kama Kielelezo Namba 10 JAJI naomba Shahidi Utusomee

Shahidi: Barua Kutoka Kwa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai CID HQ CAR C12 VOL VII Kwenda Kwa Msangi Yahusu Kupatiwa Taarifa ya Bastola Luvern A5340 Rejea Barua Kutoka Kwa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai CID HQ CAR C12 VOL VII Kwenda Kwa Msangi

Ofisi umefanya Uchunguzi Wa Silaha aina Ya Luger A5340 haikusajiliwa na Ofisi hii

Wakili wa Serikali: Barua Yako ni ya Tarehe ngapi 15/03/2021

Wakili wa Serikali: Unahusu nini

Shahidi: Kufanya Uchunguzi Wa Silaha Luger namba A5340

Wakili wa Serikali: Uchunguzi Ulikuwa unataka Kubaini Jambo Gani

Shahidi: Kubaini Taarifa ya silaha niliyoitaja Endapo Inamilikiwa na Mtu yoyote

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Kielelezo Cha Mahakama namba 10 (Barua Yako) Matokeo ya Uchunguzi wako ni nini

Shahidi: Kumbukumbu za Silaha aina ya Bastola yenye Kumbukumbu namba A 5340 haijawahi Kusajiliwa

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Barua Yako Kwenye Yahusu Mojawapo ya Vitu Ulivyo andika Jalada Ndani Ukirejea Kumbukumbu Namba za Barua ya aliyekuleta no ya 15 Nov 2020 Eleza Mahakama Namba sahihi hapo ni Ipo

Shahidi: Barua ambayo tuliletewa Maombi ya Kufanya Uchunguzi Ili onyesha Kumbukumbu ya Jalada husika, Ili Kumsaidia Aliyeomba Taarifa hiyo, Kwamba Inahusiana na Lile alichokiomba Kwenye Barua hii ambayo tuliipokea ni ya Tarehe 15 CID HQ SO. 63 VOL XI / 41/25, Nov 2020

Shahidi: Ukija Kumbukumbu ya Jalada ni CD/IR/2097/2021 Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji nilichobaini hapa kwa Haraka Haraka palikuwa na Mistake ya Kiuandishi Naomba Msamaha Mheshimiwa Jaji Kwa Mapungufu ya yalijitokeza

MTOBESYA: OBJECTION. anachokifanya Shahidi hakiruhusiwi, Document inatakiwa kujieleza yenyewe na wenzetu wanajua hicho cha kumuomba msahama Jaji hakiruhusiwi kabisa.



KIBATALA: kwa kuongeza hapo kifungu 63 ya Sheria ya ushahidi na 64 (1) ya sheria ya ushahidi inazuia hapo

Wakili wa Serikali: Pamoja na Vifungu walivyorejea Vya Sheria ya Ushahidi hakuna Mahala popote ambapo Shahidi anazuiwa Kuelezea (fafanua) Ushahidi wake Na Shahidi Yupo Kizimbani na Yupo Chini na Mwongozaji wa Dodoso nafiikiri Wamesoma Vifungu bila Kujipa Muda

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji sidhani kama tunatakiwa Kujiingiza Kwenye Mambo yaliyowazi Basi tupewe Muda tulete Nyaraka, Hayo ni Mambo yapo wazi tangu tupo shule

Jaji: Nafikiri Kifungu kipo wazi Kwamba Documents Hauwezi Kufanyia Marekebisho

Jaji: Lakini anachokifanya yeye anafafanua hafanyi Marekebisho Sasa Kwenye Maamuzi Ya Mahakama itarejea hivyo Vifungu ulivyotaja

Mtobesya: Nina Mtazamo tofauti, proove ya Documents wakati huu ambapo Mahakama imeshapokea, Ndiyo tunasema Sheria inakataza

Jaji: Ndiyo sasa hiyo itafanyika wakati wa maamuzi ya Mahakama, Labda kama Una wasiwasi Mahakama haitotafsiri sheria vizuri

Mtobesya: Hapana Jaji: basi iachie Mahakama

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Shahidi ulikuwa unasema Kumbukumbu ya Jalada

Shahidi: Kumbukumbu Ya Jalada iliyopo kwenye Taarifa CD IR 2097 2021 na Ilipaswa Kusomeka CD IR 2097 2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kuwasilisha

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kabla hujamualika Mshtakiwa Wa Kwanza, kwa kuwa sisi sote wawakilishi wa washtakiwa. VIfurushi Vya Committal, Hatuna Statement ya Shahidi ili tuweze kutumia wakati wa Cross examination Na Tunatumia Maombi haya Kifungu cha 264 cha Sheria ya Ushahidi

Jaji: Serikali Mapingamizi?

Wakili wa Serikali: Hapana

Jaji: tukubaliane tuna' break kwa muda gani Mawakili wote wanateta

Kibatala: Tumekubaliana Kwa dadika 45, Turudi hapa saa 8:15

Jaji: tunahairisha mpaka saa 8:15 mchana, naelekeza Maofisa wangu wawapatie hizo nyaraka

Jaji: anatoka

Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire na Wenzie imetajwa

Jaji: Wakili wa Mshtakiwa wa kwanza

Mtobesya: Shahidi Unakumbuka Ushawahi Kuandika Maelezo Polisi

Shahidi: Nakumbuka

Mtobesya: Unakumbuka Uliyasoma Maelezo Yako na Ukahakikisha Kwamba ni sahihi

Mtobesya: Unakumbuka Uliandika Siku gani ya Tarehe Ngapi Mwezi na Mwaka

Shahidi: 20 Mwezi 03 Mwaka 2021

Mtobesya: Kuanzia wakati huo Mpaka Sasa ni Muda gani umepita?

Shahidi: Miezi Saba

Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema wakati Unaandika Memory Yako ilikuwa sahihi wakati unaandika Maelezo yako ulikuwa Umesha andika Barua Iliyopokelewa Kama Kielelezo Namba 10?

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Uliongelea pia Kuhusu hiyo Barua Shahidi: Rudia Swali tafadhali

Mtobesya: Kwemye Maelezo Yako Unakumbuka Uliongelea Barua Uliyoitoa, Lakini hukukumbuka Wakati Ule kama Ulikosea Jalada Namba Umekuja Kukumbuka Leo?

Shahidi: Kwenye Maelezo Yangu nilikuwa nimesimamia kazi ya kile milichokifanya Kuhusu Uchunguzi Enheeeeeeee..

Mtobesya: Malizie hiyo Enheeeeeee

Shahidi: Sikuiangalia

Mtobesya: Barua yenye Matatizo ya Kiuandishi ndiyo hiyo hiyo ulikuwa unaielezea

Shahidi: Tatizo la Kiuandishi lilikuwa Kwenye Jalada

Mtobesya: Ndiyo nakuuliza sasa Barua yenye Matatizo ya Kiuandishi Ndiyo hiyo uliyoifanyia Uchunguzi

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Ulitaja Mapungufu ya Barua yako

Shahidi: Sikumbuki Kama nilitaja

Mtobesya: Mheshimiwa Naomba Original Statement ya Shahidi aweze Ku' refresh Memory

Mawakili wa Serikali Wanaitafuta Bado

Mtobesya: anampatia Shahidi

Mtobesya: angalia Kama haya Ndiyo Maelezo ya Kwako Uliyoyaandika Polisi Kama ni ya Kwako kwa Mujibu wa Kesi hii

Shahidi: Ndiyo yenyewe

Mtobesya: Soma yote kwa Sauti ilituone Kama Kuna sehemu Uliomba Kurekebishwa

Jaji: Sorry Kwani alisema yeye aliandika?

Mtobesya: alisema Hakumbuki Nimemwambia asome tusikie Kama alisema. Unless kama Mahakama ina maoni tofauti aseme Hakuna tuishie hapo

Jaji: anaposema hakumbuki, naona ungem' lead labda, Kusema asome statement Yote naona Mhhhh Sijui lakini

Shahidi: Kwenye Maelezo CD IR 2097 2020

Mtobesya: Unasoma Wapi

Shahidi: Juu kabisa

Mtobesya: Tupo Chini hapo Ndiyo kwenye Content yako

Shahidi: Hakuna Sehemu niliyoandika

Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kwamba Katika Maelezo Yako hiyo Kumbukumbu namba

Shahidi: Nakumbuka ilikuwa 15 March 2021 Baadae nikajua Kuandika Maelezo, kwa hiyo Makosa ya Kibinadamu tu

Mtobesya: Kwa hiyo Kipengele hicho kwenye Maelezo yako kipo au Hakipo

Shahidi: Hakipo

Mtobesya: Umesema Ulifanya kazi Kwa Kutumia Mfumo, Je uliweza Ku' Demonstrate namna huo Mfumo unafanya Kazi

Shahidi: Issue ya Kuwaita watu ili waweze Kushuhudia ninachokifanya ni suala lingine

Mtobesya: Je Uliwahi Kufanya?

Shahidi: Ndiyo Mara yangu ya kwanza

Jaji: Kuna sehemu hamuelewani naona

Mtobesya: labda Nirudie Swali Ulionyesha Wakati Unalekezwa na Wakili wa Serikali namna Mfumo unavyofanya kazi

Shahidi: Sikuonyesha

Mtobesya amemaliza, anaketi, anasimama John Mallya

Mallya: Dhumuni la Usajili wa Silaha ni Kudhibiti Silaha isifanye Uhalifu

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwa hiyo wewe Ulipewa silaha Kuchunguza ni Rahisi Kujua Kama ilifanya Uhalifu

Shahidi: Mie naletewa Kuchunguza Silaha ni ya nani

Mallya: Majibu Negative Unatazamaje Kujua Kama ni Negative

Shahidi: Kwenye Results inasema No Records

Mallya: Kwa hiyo No Records ndiyo Results

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Sasa ulisema Hapa Mahakamani Leo kuwa Results ni No Records? Shahidi anatoa Macho tu hajibu swali, anashangaa

Mallya: Mheshimiwa Jaji nasubiri Jibu

Shahidi: nilicho present Leo ndiyo kilichokuwepo

Mallya: Kwa hiyo umeleta au hujakileta

Shahidi: Hakipo

Mallya: Umeingia Polisi Ukiwa na Miaka 24

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwa hiyo unauzoefu Wa Miaka zaidi ya 20

Shahidi: Ndiyo

Mallya: hiko Kitengo Unamuda nacho gani

Shahidi: Miaka 20

Mallya: Ulipata Kujua hiyo silaha imepatikana wapi

Shahidi: hiyo siyo Kazi yangu

Mallya: Kwa hiyo wewe unatolea Majibu ya Uchunguzi Silaha iliyosajiwa tu?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Ulizungumzia Ufanisi wa huo Mfumo wakati unaongozwa

Shahidi: Data base Ipo Vizuri na ina Speed

Mallya: Ulizungumzia hilo suala

Shahidi: Sikuzungumzia

Mallya: Nilikusikia Kwamba Ukibonyeza Save, huwezi Kufuta bila Ruhusa ya Admin

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Je Kama hukueleza Admin Ndiyo Mwenye Mandate Vipi Kama Admin Alibadilisha umiliki wa Silaha Ya Kingai aweze Kumbambikia Mtu

Shahidi: Adimn hana Mandate ya Moja Kwa Moja

Mallya: Sasa Unabadili Ushahidi Wako?

Shahidi: Hapana Kuna mambo Sikuulizwa

Mallya: Je, ulielezea namna Admin anavyotoa ruhusa

Shahidi: Sikueleza

Mallya: Ulisema Pia Kuna Taarifa Unazitumia katikati, Je ulipata Mazingira ya Serial Namba Kufuta na wahalifu

Shahidi: Ni sahihi

Mallya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Namna kama hiyo inaweza kujitokeza

Shahidi: Endapo Parameters Zimefutwa tunashirikiana na watu wa Ballistic

Mallya: Kwa hiyo tunakubaliana Parameters Zako siyo Kitu Pekee cha kutambua Silaha

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwa hiyo Ulielezea wakati Unaulizwa

Shahidi: Hapana Sikueleza

Mallya: umewahi Kupata Mazingira ambapo namba imefojiwa kutoka namba 04 kwenda namba 07

Shahidi: Unajua kwa Mazingira yangu

Mallya: Jibu swali Shahidi

Shahidi: Issue za Ku temper hatujazishuhudia

Mallya: Ulieleza Kwamba Uliletewa Barua tu siyo Bastola

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwa hiyo Ujajisumbua Kama namba ulizo letewa zilikuwa tempered

Shahidi: Siyo Jukumu langu

Mallya: Unafanya Kazi Siku Ngapi katika wiki

Shahidi: Maasa 24 kwa Siku Saba

Fredrick Kihwelo: Ni kweli tarehe 25 ulipokea Barua Kutoka kwa ASP Msangi

Shahidi: Ndiyo nilipokea

Fredrick: Mpo wangapi Kwenye hicho Kitengo

Shahidi: Tupo 20

Fredrick: Barua ya ASP Msangi Ilikuwa inakutaka Ufanye nini

Shahidi: Kutoa Majibu ya Umiliki

Fredrick: Wewe Ulitoa Taarifa ya Umiliki au Uchunguzi

Shahidi: Nilifanya Uchunguzi nikatoa Taarifa ya Umiliki

Fredrick: Barua Yako ya majibu ni ya Uchunguzi au Umiliki

Shahidi: Umiliki

Fredrick: Ni sahihi Mnafanyia Uchunguzi Siku hiyo hiyo Mnapopokea Barua

Shahidi: Ndiyo

Fredrick: Wewe Ulipokea Barua Siku gani 25 /11/2020, ukatoa majibu lini?

Shahidi: 15 March 2021

Fredrick: Ni Muda gani umepita

Shahidi: Miezi 05

Fredrick: Je, Katika Majukumu yako ulitaja Jukumu lako la Kutaja Umiliki

Shahidi: Hapana

Fredrick: Ni kweli Kuna Njia 2 za Kumiliki Silaha?

Shahidi: swali sijaelewa Fredrick: Katika Maelezo Yako ulisema Mtu anaweza Kumiliki Silaha Kwa Njia ya Kuingiza ndani ya Nchi, Kununua Ndani ya Nchi na Kama amerithi, Sasa Nakuuliza Je kuna namna Mbili tuh za Kumiliki Silaha

Shahidi: Si kweli

Fredrick Kihwelo anaketi na anasimama Peter Kibatala

Kibatala: Kielelezo Cha Mashtaka namba 10 umetaja Barua ya Tarehe 25 Nov Mwaka 2020 aje ni sahihi Kwamba Barua hii Ndiyo Chanzo Chote cha wewe Kuandika Barua

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba bila Barua hiyo wewe Usingeandika hiyo Barua

Shahidi: Ndiyo sahihi Kabisa

Kibatala: Siyo Kawaida yako kuandika tu barua

Shahidi: itakuwa Kinyume na kZii

Kibatala: Je, hiyo Barua iliyokufanya Uandike Barua Umekuja nayo?

Shahidi: Sikuja nayo

Kibatala: akwa Ufahamu wako wewe ni Muhimu au Siyo Muhimu

Shahidi: kwa Upande wangu sikuona Umuhimu wa Kuja nayo

Kibatala: na Kwa hiyo Barua ndimo ambapo tungepata Details za Hiyo Bunduki ambayo wewe Ulipswa Uifanyie Uchunguzi

Shahidi: Sahihi Kabisa

Kibatala: na Ndiyo humo tungeona Namba CZ 100,Callibre 9mm hatuwezi Kuona Popote zaidi ya hiyo Barua

Shahidi: Sahihi kabisa Kibatala: hujazungumza kabisa Kuhusu CZ 100 9MM za Ulikuwa unachunguza kwenye hiyo Barua Uliyoandikiwa

Shahidi: Sahihi Kabisa

Kibatala: sahihi Kabisa hujazungumza Kuhusu CZ 100, Callibre 09mm

Shahidi: Sahihi sikuzungumzia

Kibatala: Kuhusu Electronic Data Base Ulizungumza Kuhusu Mmiliki wa Risasi

Shahidi: Kwenye electronic Data Base inaonyesha kuwa Idadi ya Risasi zakutumia wakati wa Uhai wa Leseni

Kibatala: Je Katika huo Mfumo Usajili wa Bunduki na Risasi ni Kitu kimoja au tofauti Shahidi: Ni Kitu Kimoja

Kibatala: Kwa hiyo Ni kisha Sajiliwa Bunduki naona na Risasi zizlizopo? Mfano TRA Umiliki wa Gari Unaonyesha na Kiasi cha Mafuta Kilichomo

Shahidi: Hapana

Kibatala: Kwa hiyo Mfano niondoe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Risasi zinasajiliwa?

Shahidi: Hazisajiliwi

Kibatala: Na hujazungumza kuhusu Risasi

Shahidi: Sijazungumza

Kibatala: na wala Kwenye Barua p10 hujazungumza kuhusu Risasi

Shahidi: Ni sahihi Kabisa

Kibatala: Kuna swali umeulizwa kuhusu Umiliki Possession, Je Mtu aki import Bunduki inakwenda Wapi

Shahidi: Lisenced Warehouse

Kibatala: Wewe Katika System Yako Muda huo Inasomeka nini

Shahidi: Muda huo inakuwa haijaingizwa Kwenye Mfumo

Kibatala: Ulisema Chochote a kuwa Inae zekana Bastola Ile I weza Kuwa a Imetoka Lisenced Warehouse

Shahidi: Sikusema Chochote

Kibatala: Ulisema hiyo Possibility kwenye hiyo Barua yako

Shahidi: Sikuseme

Kibatala: Ulitaka Jaji akusemehe Kwa Makosa ya Kumbukumbu namba, Je ni sahihi Kwamba ili tukusamehe ni lazima marekebisho yako tuangalie Kwenye Barua (mama) ambayo yenyewe ndiyo ina mwaka sahihi

Shahidi: Sahihi Kabisa

Kibatala: Barua hujaitoa Mahakamani

Shahidi: sahihi Kabisa

Kibatala: Kwa hiyo sasa Msamaha wako Unaelea kwa sababu hatuna Control

Shahidi: Ni sahihi kabisa

Kibatala: hii Barua Yako inaonekana Ulikuwa unaipeleka ASP H. MSANGI, Je Kuna Mtu anaitwa Inspector Swila, Je Ulimtaja

Shahidi: Sikumtaja

Kibatala: Kwa hiyo akisema Inspector Swila Kuwa yeye Ndiyo aliyeandika hiyo Barua atakuwa anasema ni Uongo

Shahidi: Mimi nilipewa na ASP H. MSANGI

Kibatala: ASP H. MSANGI Hukum' Adress kwa Bahati Mbaya, Ni Kwa sababu Yeye ndiye alikuandikia Barua Mama, akija Inspector Swila kasema Ulimpelekea Majibu ya Uchunguzi atakuwa Muongo

Shahidi: Mimi Najua ASP H. Msangi

Kibatala: Wakati Unaandika Barua Ofisi yako ilikuwa Chini ya Mkurugenzi ya Makosa ya Jinai

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni sahihi wewe na Msangi Mlikuwa Mpo wote Chini ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kama Serial Namba ikichezewa Ikafutwa Je hilo no Jukumu la nani

Shahidi: Jukumu la Ballistic

Kibatala: Umesema ulipokea Barua Ukagonga Barua na Utaratibu Wa Kupokea Barua lazima Pawe na Kitabu Kama Ili Sajiliwa Kuingia Ofiini kwenu

Shahidi: Ikihitajia nitaileta

Kibatala: Lakini Hapa hujaitoa

Shahidi: Hapa Sijaitoa

Kibatala: Ulitoa Maelezo Kwa Jaji kwanini Hiyo Register hukuleta Kama Sababu ni Nzito au Kubwa

Shahidi: Sababu Sikutoa

Kibatala: ulisema kwamba Result ni Negative

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je ulifafanua Kwa Jaji Kwanini Hukuleta hiyo Negatove Results

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Unafahamu Kwamba Ushahidi Wako Lazima Upitie Sehemu kadhaa, Mahakama lazima Ipime Ushahidi wako

Shahidi: Hiyo nafahamu

Kibatala: Mwambie Sasa Mheshimiwa Jaji Kama Ulifafanua kwanini ulishindwa a kuleta Extract ya Negative Result

Shahidi: Sikufafanua

Kibatala: Nilisikia Kwamba Kuna Typing Error Kwenye P10

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sasa Mahakama Itajuaje Kama Hakuna tena Makosa ya Kibinadamu humu?

Shahidi: Ni Jukumu la Mahakama Sasa Kupima

Kibatala: Kuna Sheria Yoyote au Kanuni yoyote ambayo inasema usilete Barua Mama, Report iwe Inajitegemea

Shahidi: Hakuna Kibatala Ni wewe tu Uliamua

Shahidi: Kimyaaaaaaaaa

Kibatala: Swali langu la Mwisho

Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kuwa akuna Kosa Linajitegemea Kumiliki Silaha Bila Kibali

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sheria Inaitwaji+e

Shahidi: Inaitwa Sheria ya Umiliki na Udhibiti wa silaha Kifungu cha 20

Kibatala: Mheshimiwa Jaji sina Mengine

Wakili wa Serikali: Shahidi Umeulizwa Maswali Mengi kuhusiana na Barua Mama, Uliposema Hukuona Umuhimu ulimaanisha nini

Shahidi: Ile ilikuwa Inaonyesha Guidance Ya Uchunguzi Ninaopaswa Kufanya Baada ya Kukamilisha Kwangu Sikuona kama Kuna Ulazima wa Kuleta Ile Baru

Wakili wa Serikali: Uliona Umuhimu kitu gani

Shahidi: Taarifa ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Ulifanya Kazi Jambo gani Shahidi: Particulars nilizozitumia Kutoka Kwenye Barua Mama, Ndiyo Key Issues Katika Uchunguzi wa Umiliki wa Silaha

Wakili wa Serikali: Elezea Kuhusu Tukio la Uhalifu

Kibatala: OBJECTION hayo ni Mambo Mapya

Shahidi: Tunapopokea Taarifa hizo Majibu Kwamba Ni Chanya, Data Base Inaonyesha Silaha Inamilikiwa na Mtu fulani tuna Command Button, Kisha Report Inatoka

Mallya: OBJECTION hiyo ni fact Mpya tunapinga

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sijui lakini ni Maoni yetu Kwamba Cross examination ndiyo imeibua Extract Kuhusu Negative Results Ameulizwa hiyo, Shahidi aachwe aeleze Kama Wakili angeona siyo Issues Sana alipaswa asiibue Ni hayo tu, Tunaomba Shahidi ajibu

Kibatala Wakili akatai Those are Neww matters anajaribu Ku Exclude New Matters

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Sahamani, halafu Hakuongelea Printabiliy ya Negative Results

Jaji: Hoja Mmelewa ya Upande wa Utetezi? Hapa anakuja na Ufafanuzi Kwamba Siku weza Ku' command ila Print na Mimi na kubaliana nao Kwamba hilo ni Jambo Jipya ambalo hakuzungumza na Sasa anataka Kuzungumza

Wakili wa Serikali: Shahidi Nitakuuliza suala hilo hiyo kama Majibu yakiwa Negative guwezi Kuprint, Kwanini sasa?

Wakili wa Serikali: Shahidi Nitakuuliza suala hilo hiyo kama Majibu yakiwa Negative huwezi Kuprint, Kwanini sasa?

Shahidi: Ukikomand ina Print...

Mallya: OBJECTION

Kibatala: OBJECTION

Mtobesya: OBJECTION

Jaji: nafikiri unaweza Kwenda Kwa anjia Nyingine

Wakili wa Serikali: Nilikia Umeulizwa kuhusu Inspector Swila kwamba Ile Barua Mama Kaandika Nani

Shahidi: ASP H. MSANGI

Wakili wa Serikali: Kwamba Ile Barua Mliandikiana Wenyewe, Hebu fafanua

Shahidi: Ni sahihi Kabisa Kwamba Vitengo Vyote Vipo kwa DCI, Yeye kazi yake ni Kuhakikisha Je tuna Mfumo, inapokuja suala la Kiuchunguzi yeye hauhisiki tena Ofisi yangu ya Mrajisi Kama Mtaalamu wa Kufanya Uchunguzi ni Kufanya Uchunguzi Bila Kuingilia na Maamuzi au Msukuko wowote wa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu forgery, ELEZEA Mahakama Ulichunguza nini

Shahidi: Mimi Sikuletewa Silaha nilichunguza Barua na Particulars Zilizokwepo kwenye Zile Barua zilikuwa ni Key Parameters zilizoniwezesha Mimi Kufanya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kuhusiana na Silaha inayoingizwa Nchini kutoka nje, wewe Maelezo yako hayajaondoa possibility Shahidi: Mfumo wetu wa Silaha na Usajili, Mfumo wetu Unamuingiza Mwishoni kabisa baada ya silaha Imeshaingia Nchini au Kukamilisha Utaratibu wa malipo wowote wa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu forgery, ELEZEA Mahakama Ulichunguza nini

Shahidi: Mimi Sikuletewa Silaha nilichunguza Barua na Particulars Zilizokwepo kwenye Zile Barua zilikuwa ni Key Parameters zilizoniwezesha Mimi Kufanya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia kuhusiana na Silaha inayoingizwa Nchini kutoka nje, wewe Maelezo yako hayajaondoa possibility

Shahidi: Mfumo wetu wa Silaha na Usajili, Mfumo wetu Unamuingiza Mwishoni kabisa baada ya silaha Imeshaingia Nchini au Kukamilisha Utaratibu wa malipo

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mimi naishi hapo Kama Kuna Wenzangu waendeleeeee

Wakili wa Serikali: Wenzangu na wao hawana kitu

Jaji: Shahidi tunakushukuru, unaweza Kuendelea

Wakili wa Serikali: Ndiye Shahidi Tuliyekuwa naye Leo, Tunaomba Hairisho Hadi Kesho Tuweze Kuendelea na Shahidi Mwingine

Jaji: Upande wa Utetezi

Kibatala: hatuna Pingamizi Jaji anaandika, Mahakama ipo kimya

Jaji: Maombi yaliyoletwa na mashtaka mahakama inakubali mpaka kesho Saa 3 asubuhi Upande wa Mashtaka mnaelekezwa kuleta mashahidi. washtakiwa wataendelea kuwa chini ya magereza mpaka kesho
 
Mungu wa mbinguni awabariki!
Nakuona Jo
giphy.gif
 
Back
Top Bottom