Kesi ya Mbowe: Namba A5340 kwanini imekuwa issue kubwa?

Yasemekana mshitakiwa #2 alikamatwa na bastola ambalo anakanusha.

Kwamba alikamatwa na bastola au hakukamatwa na bastola, hayo ni mambo mengine.

Kukamatwa na bunduki kinyume cha sheria mbona bado ni msala usio kuwa na kifani?

Kwanini upande wa mashtaka wameshupalia zaidi namba kuliko hata kuwa mshitakiwa anatuhumiwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria?

Kwanini pia upande wa utetezi wanasikika kuongea CZ 100 kwenye bastola na kuwa si A5340, badala ya kukomaa tu kuwa Adamoo hakukutwa na bastola?

Kwanini kumekuwa na marumbano haya kuhusiana namba A5340?

Ni kitu gani mahsusi kinatafutwa kwenye namba hii pendwa?
Inawezekana namba inayoshupaliwa sana ni ya bastola iliyopotea ambayo ilimilikiwa na Hamza.
 
Mwenendo na hukumu ya kesi vyote viko wazi.

Mwenendo:
--- hoja zote zisizoathiri hukumu ya kesi ya msingi zitaamriwa in favor ya utetezi.

--- Hoja zote zenye kuathiri hukumu ya kesi msingi zitaamriwa in favor ya mashaka.

--- Hukumu ya kesi ya msingi ipo tayari.
Hapa simply unamaanisha vitu vidogo tunapewa sisi, lakini vile vikubwa wanapewa wao hata kama haki /sheria haiko upande wao ila kwasababu refa ni wa kwao.
 
Kijiko😀😀 mama mbege anasema aliitwa na alikuwa na dada Esther ila mahita kasema kulitokea tafran umati ukakusanyika ndo wakachagua mashahidi.....
Anita Valerian Mtaro anasema hali ya pale Rau Madukani hali ilikuwa tulivu na hapakuwa na watu mpaka wanaondoka.

Leo.mahita anasema baafa ya kupiga kelele za simama kaa chini watu walijaaa.
🤣🤣🤣
 
Raisi alitaarifiwa; hapana

DG wa tiss alitaarifiwa; hapana

Igp alitaarifiwa; hapana

RPC dar, arusha, kilimanjaro, mmeanza, morogoro mbeya walitaarifiwa; hapana

RCO wa mikoa husika walitaarifiwa: hapana

Hii kesi ni siri ya kingai na mahita na jumanne na goodluck, ndo maana washitakiwa walitolewa central moshi- dar na kupeleka mbweni Ili kuficha uhuni wao
Kwamba Kingai na Mahita wanaweza kuona Mpango kabambe wa Ugaidi kulipua vituo vya mafuta na kudhulu viongozi na Hata Usalama wa Taifa wasitonywe??

Maswali ya Kibatala yalikuwa Muhimu sana kwa Mahita.
 
Na siyo hilo tuu Mahita yeye amesema hawakuwa grocery wala bar ila walikuwa vibanda umiza... Halafu askari waliofika kukamata ni 6 na wala siyo 5 aliosema muuza mbege... Pia Habari ya kwenda kupata nyama choma na ndizi yeye hajui hiyo
Kingai wakati wa ushahidi wake alisema Gari lao liliharibika njiani wakakaa kwa muda na kula Nyama choma na Mo energy.

Mahita anasema gari lao halikuwa kuharibika na wala hakuna nyama walizokula njiani.

Mnasema ili nielewe hii kesi natakiw akujua technicalities za mahakama na Degree mbili za sheria??

No way!
 
Anita Valerian Mtaro anasema hali ya pale Rau Madukani hali ilikuwa tulivu na hapakuwa na watu mpaka wanaondoka.

Leo.mahita anasema baafa ya kupiga kelele za simama kaa chini watu walijaaa.
🤣🤣🤣
Kwa hili wewe ndio unayedanganya,majibu yao hayajatofautia
 
CZ100 ni aina ya bastola tu ambazo ziko zimetapakaa duniani kote, A5340 ni serial number ambayo iko moja tu duniani kote. Serial number ya silaha huwa ni moja tu, hapa ndipo mchezo ulipo.
Yasemekana mshitakiwa #2 alikamatwa na bastola ambalo anakanusha.

Kwamba alikamatwa na bastola au hakukamatwa na bastola, hayo ni mambo mengine.

Kukamatwa na bunduki kinyume cha sheria mbona bado ni msala usio kuwa na kifani?

Kwanini upande wa mashtaka wameshupalia zaidi namba kuliko hata kuwa mshitakiwa anatuhumiwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria?

Kwanini pia upande wa utetezi wanasikika kuongea CZ 100 kwenye bastola na kuwa si A5340, badala ya kukomaa tu kuwa Adamoo hakukutwa na bastola?

Kwanini kumekuwa na marumbano haya kuhusiana namba A5340?

Ni kitu gani mahsusi kinatafutwa kwenye namba hii pendwa?
 
Me nilivyoelewa ni kwamba hiyo A5340 ni serial number ya silaha na Cz100 ni model, kwahiyo unapoongelea A5340 unakuwa very specific kwenye hiyo silaha husika ambayo haifanani na silaha nyingine yeyote duniani, Ila ukiongelea Cz100 maana yake zipo nyingi za model hiyo ikiwemo hiyo inayosemwa ni ya Adamoo no.A5340 sasa pengine kuna A5341, A5342 n.k Ni sawa na Corolla TI zipo nyingi ila namba T 123 DUD iko moja tu

Hata kama A5340 ni specific katika kundi la CZ 100, kwanini mashtaka hawataki kukubali kuwa ni CZ 100 pia?

Kwanini ufafanuzi kama wako tu hautolewi kuondoa sintofahamu hii?
 
Kuna limjaa flan lilikuwa mkoa mmoja una samaki wa maji barid lkn wakubwa! Alikuwa kila akiitisha press kupitia gesh ra porish anakuwa na mabunduki meng meng akidai yalikamatwa wakat wa mapambano na magambaz alikuwa anayaonyesha huku akiwa na glove nyeupe! Ingawa kwa sasa tupo nae pale kwa mkapa kila mech ya ligi! Labda kipind kile aliwah kuitaja hyo namba a ngap ngap cjui! Sasa labda utetez wanajua hyo binduk iliwah kuonyeshwa kwenyd press! Huwez jua
Hapa kwa hili inawezekana.
Chama changu ccm hili litatuangusha kwani ukweli utabaki kuwa ukweli na uongo hautaweza kutuweka huru tutarudi ktk zile zama za KUZOMEWA TENA.
Chama kiingilie mapema ndo maana tunamwona Ndugai, Mpina,Msukuma,Polepole wameshaona chama kama chama upepo ushaanza kubadilika.
Upinzani bungeni haupo lakini ndani ya chama na bungeni upo wazi ndo maana gazeti letu la UHURU lilipewa likizo ya kuwa KIGAZETI.
Hii kesi haitatuweka pazuri kisiasa labda tuwe tumekosa hoja kwani kesi inaonekana inavyowatesa mashahidi.

Sent from my TECNO K8 using JamiiForums mobile app
 
denooJ, hapa hakuna kesi...

Mwisho wake ndiyo huo na sababu ni hizi;

1. KWA UPANDE WA WAANDAAJI WA IGIZO HILI NA KULIITA "KESI YA UGAIDI WA MBOWE:"
Ni kweli nami naamini jaji ameshaona jamhuri wamepeleka kitu cha hovyo mahakamani, lakini jaji huyo huyo ataamua kesi kwa kuwapa ushindi jamhuri huku akitabasamu, huyu tayari atakuwa ametimiza wajibu wake kwa mabosi wake na sio kwa taaluma yake kama kesi inavyotaka, wakati mwingine nawahurumia mawakili wa upande wa utetezi kwa akili kubwa wanayotumia kushindana na hawa wasanii na genge lao.
 
CZ100 ni aina ya bastola tu ambazo ziko zimetapakaa duniani kote, A5340 ni serial number ambayo iko moja tu duniani kote. Serial number ya silaha huwa ni moja tu, hapa ndipo mchezo ulipo.
Ni kweli kabisa...
Screenshot_20211106-092317.jpg
 
Back
Top Bottom