Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,510
- 8,536
Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mkubwa mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu. Nafuatilia kwa kwenda mwenyewe Mahakamani. Hata sasa nipo Viunga vya Law School of Tanzania ilipo Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Sitaki kupitwa wala kusimuliwa. Najionea na kusikia mwenyewe moja kwa moja.
Yanayozungumzwa Mahakamani hapa yanashtua, yanaogofya na kuanika hata visivyofaa kuanikwa. Wengi wanaofuatilia wanajua kuwa kesi hiyo sasa imezaa kesi ndogo. Kesi ndogo ni imezaliwa baada ya Maelezo ya Mshtakiwa wa pili (Adamoo) kupingwa na upande wa Utetezi Mahakamani hapa. Ndipo Jaji Siyani anayeisikiliza kesi kuu alipotoa amri ya kuendeshwa kesi ndogo ndani ya kesi kuu kuhusu pingamizi hilo.
Mwisho wa kesi ndogo inayoendelea kutolewa ushahidi sasa ni kukubaliwa au kukataliwa kupokelewa kwa maelezo ya Adamoo yanayodaiwa aliyatoa huko Polisi alipokamatwa na kuhojiwa/kuchukuliwa maelezo. Yeye mwenyewe Adamoo kwenye ushahidi wake ameyakana Maelezo hayo akisema aliletewa yakiwa yameshaandikwa na kusainishwa chini ya vitisho vikubwa vya polisi (ACP Kingai). Jana shahidi wa pili (Bwana Ling'wenya) alianza kutoa ushahidi wake na anaendelea leo hii.
Kuna mambo yameshasemwa hapa Mahakamani na mashahidi wa Utetezi yanaogofya sana. Kwanza, kuna idadi kubwa ya wanajeshi wamekamatwa na wanateswa kwenye vituo vya polisi. Kuna nini na kumetokea nini jeshini huko hadi kufikia hapo? Pili, aliyetajwa na ACP Kingai kama mtoa taarifa za uhalifu wa Mbowe na wenzake (Luteni Urio) naye alishakamatwa na kuteswa na polisi. Je, aliteswa ili 'amchome' Mbowe na wenzake?
Kuna jambo linaogofya zaidi. Ushahidi wa kwamba wanajeshi wanakamatwa na kuteswa na polisi waweza kupika chuki na hasira kwenye mioyo ya wawili hao na kuzua suitafahamu ambayo itashindikana hata kusemeka huko mbeleni. Yaani, kunaweza kukachemka 'bifu' kati ya wapambanaji hao. Ikifika hapo, hali itakuwa tete. DPP, hujachelewa kuzuia kuvuja zaidi mambo ya ndani kuliko maini ya nchi na kuzuia taharuki isiyo na hata mkuki.
Buriani Ole Nasha!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Je Askari waliotumikia nchi tena vitani kwa level ya komandooo wakiondolewa kazini kuna kosa kujitafutia kipato halali ? Mbona Lugumi naye alichukua wa aina hiyo walioko mitaani wakawa walinzi wake ? au wanataka wakawe walinzi wajummbani au walinde ATM ? au wanataka wakaajiriwe na waasi huko DRC na nchi zingine maana ajira ziko nje nje ….
Kama Rais Samia alivyosema ; Tutende haki ili Mungu asituadhibu….
Kama hii kesi haingeenda mahakamani tungejua vipi kuwa Komando huyu haonekani kama ilivyo kwa Komando Ramadhani Kadego ( na pengine wameuliwa
Serikali ya JPM imetuachia makovu sana na kimsingi tunahitaji mambo mengi zaidi kama haya yawe wazi ili tuweze kufanya marekebisho makubwa
Mfano leo hiii wanajeshi wanawafikiria vipi Polisi ?