Kesi ya Mbowe na wenzake inaanika hadi 'mambo ya siri za nchi'. DPP hujachelewa kuifuta

Si tuliambiwa nchi inaendeshw na waziri mkuu (mtoto wa Magufuli) aliyebaki labda aamue yeye kuitoa kesi DPP anafuata tu maelekezo hadi maelekezo kutoka juu kwenda chini yafike .
Bila hivyo Mbowe anaweza kufungwa ili isemekane mashahidi walitoa utetezi wa uongo ili Mahakama isiwakute na hatia.
Moja 9 chuki itatamaliki miongoni mwa jeshi la wananchi na jeshi la polisi.
Kwa jinsi mahita kingai walivyofanyia unyama walinzi wa mbowe kuwafunga pingu mikono miguu saa 24 kila siku kuwapiga kuwatesa kumporeza Moses lijenje lt urio kwa kesi hewa tuhuma hewa feki ugaidi ambao hawana haupo ni lazima Asikari wa jwtz wajisikie vibaya kwani ni udhalilishaji wa kiwango cha kutisha sana
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa ukaribu mkubwa mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu. Nafuatilia kwa kwenda mwenyewe Mahakamani. Hata sasa nipo Viunga vya Law School of Tanzania ilipo Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi kwa ajili ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Sitaki kupitwa wala kusimuliwa. Najionea na kusikia mwenyewe moja kwa moja.

Yanayozungumzwa Mahakamani hapa yanashtua, yanaogofya na kuanika hata visivyofaa kuanikwa. Wengi wanaofuatilia wanajua kuwa kesi hiyo sasa imezaa kesi ndogo. Kesi ndogo ni imezaliwa baada ya Maelezo ya Mshtakiwa wa pili (Adamoo) kupingwa na upande wa Utetezi Mahakamani hapa. Ndipo Jaji Siyani anayeisikiliza kesi kuu alipotoa amri ya kuendeshwa kesi ndogo ndani ya kesi kuu kuhusu pingamizi hilo.

Mwisho wa kesi ndogo inayoendelea kutolewa ushahidi sasa ni kukubaliwa au kukataliwa kupokelewa kwa maelezo ya Adamoo yanayodaiwa aliyatoa huko Polisi alipokamatwa na kuhojiwa/kuchukuliwa maelezo. Yeye mwenyewe Adamoo kwenye ushahidi wake ameyakana Maelezo hayo akisema aliletewa yakiwa yameshaandikwa na kusainishwa chini ya vitisho vikubwa vya polisi (ACP Kingai). Jana shahidi wa pili (Bwana Ling'wenya) alianza kutoa ushahidi wake na anaendelea leo hii.

Kuna mambo yameshasemwa hapa Mahakamani na mashahidi wa Utetezi yanaogofya sana. Kwanza, kuna idadi kubwa ya wanajeshi wamekamatwa na wanateswa kwenye vituo vya polisi. Kuna nini na kumetokea nini jeshini huko hadi kufikia hapo? Pili, aliyetajwa na ACP Kingai kama mtoa taarifa za uhalifu wa Mbowe na wenzake (Luteni Urio) naye alishakamatwa na kuteswa na polisi. Je, aliteswa ili 'amchome' Mbowe na wenzake?

Kuna jambo linaogofya zaidi. Ushahidi wa kwamba wanajeshi wanakamatwa na kuteswa na polisi waweza kupika chuki na hasira kwenye mioyo ya wawili hao na kuzua suitafahamu ambayo itashindikana hata kusemeka huko mbeleni. Yaani, kunaweza kukachemka 'bifu' kati ya wapambanaji hao. Ikifika hapo, hali itakuwa tete. DPP, hujachelewa kuzuia kuvuja zaidi mambo ya ndani kuliko maini ya nchi na kuzuia taharuki isiyo na hata mkuki.

Buriani Ole Nasha!

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Kuna siri gani ya nchi hapo?
Kufukuzwa kwa makomandoo wawili jeshini au??
 
Je Askari waliotumikia nchi tena vitani kwa level ya komandooo wakiondolewa kazini kuna kosa kujitafutia kipato halali ? Mbona Lugumi naye alichukua wa aina hiyo walioko mitaani wakawa walinzi wake ? au wanataka wakawe walinzi wajummbani au walinde ATM ? au wanataka wakaajiriwe na waasi huko DRC na nchi zingine maana ajira ziko nje nje ….
Kama Rais Samia alivyosema ; Tutende haki ili Mungu asituadhibu….
Kama hii kesi haingeenda mahakamani tungejua vipi kuwa Komando huyu haonekani kama ilivyo kwa Komando Ramadhani Kadego ( na pengine wameuliwa
Serikali ya JPM imetuachia makovu sana na kimsingi tunahitaji mambo mengi zaidi kama haya yawe wazi ili tuweze kufanya marekebisho makubwa
Mfano leo hiii wanajeshi wanawafikiria vipi Polisi ?
Asikari mstaafu yupo huru kufanya kazi popote pale ili mladi anafuata Sheria za Nchi , Tambua kuwa kesi ya mbowe ni ushauri wa Sabaya kwa magufuli ambapo alipokea ushauri wa hovyo pasipo kutafakari kabla matokeo yake wanatengeneza kesi za kijinga kwenda kuwaonea walinzi wa mbowe kuwaua wengine kwa mateso ya kuwalazimisha waseme ugaidi feki ugaidi hewa ni vitendo vibaya kupata kutokea Nchini na itazidisha chuki tokea kwa wapenda haki za binadamu.
 
Kuna siri gani ya nchi hapo?
Kufukuzwa kwa makomandoo wawili jeshini au??
Walifukuzwa wapi? na ugaidi wenyewe upo wapi? aliyetengeneza kesi ya ugaidi hewa ugaidi feki ndiyo mtu mpumbavu na Siri za Nchi ni pamoja na kuwadhalilisha Asikari hata kama ni mmoja tu, ebu tuambie alipo Moses lijenje na Lt Urio kwanza?
 
Watengeneza kesi hawakutafakari kabla walikurupuka kutengeneza kesi tu huko moses lijenje akifa kwa mateso baada ya kuamua kuwa kimya kwa kuwambia kuwa hajui ugaidi wowote kwani yeye na Lt Urio walimpa mbowe Asikari wasitaafu kwa nia ya kuwapa ajila mpya tu wapate ridhiki, hawakujua chochote zaidi ya hayo, kitendo cha kutuma MP na Asikari kwenda kuwatesa kuwalazimisha waseme ugaidi hewa, ugaidi ambao hawana haupo kilikuwa kitendo cha kinyama ni kinyume cha haki za binadamu, ikumbukwe kuwa kesi ya mbowe ilisukwa na magufuli kwa lengo la kuidhoofisha chadema lakini washauri wa magufuli kipindi kile akina Sabaya ndiyo wakabuni mbinu za hovyo za kuwabambikia kesi za ugaidi huku mahita kingai wakipiga sana kuwafunga pingu mikono miguu saa 24 ni unyama ulioje, hawakutarajia siri kuvuja mahakamani ampapo sasa vichwa vinawauma kwa uonevu waliotenda dhidi ya mbowe na walinzi wake
Hii kesi iko vibaya.Ukisema umfunge ni kashfa na ukimwachia pia kashfa.
Hapo mwisho watendaji watajikuta wanabeba zigo ili kuisafisha system maana system italazimika kutenda haki kusafisha wakubwa.
 
64 Reactions
Reply
Back
Top Bottom