Kesi ya Mbowe na wanasheria wa Tigo na Airtel ikumbushe wenye mamlaka kutunza siri za wateja ni muhimu kujenga sekta imara ya benki na mawasiliano

Kwa mwenendo wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA freeman Mbowe na ushahidi na mashahidi wanaojitokeza kuna vilio vitakuja baadae.

Shahidi namba 05 wa leo ama kwa kujua ama kutokujua au kwa kushinikizwa unaona kabisa ameitumbukiza shimoni TIGO na MIC.

Huyu Shahidi wa TIgo anaonesha kabisa kuwa hajui ama alifanya kwa kufuata maelekezo. Kuna sehemu anasema wao mtu yeyote akipata barua toka Polisi kuhusu kuchunguzwa kwa mtu hawaangalii chochote.

Hapa anabanwa na sheria ya faragha. Mbowe anapiga hela hapa. Hata kama Mbowe atafungwa kwa case atakayofungua dhidi ya TIGO ana uhakika wa familia yake kuishi kwa raha.

TIGO wamejiingiza katika mgogoro mkubwa na watumiaji wengine. Wasijione wapo bora waulize gazeti kongwe duniani lilivyofutika katika uso wa dunia.

Mwanasheria wa TIGO kama mlinda siri wa Wateja.

Hii kesi inaleta mengi.
ulilosema ni kweli, ingekuwa kule kwa wenzetu,TIGO leo angeshalia mno kwa kukimbiwa na wateja, pia kushtakiwa mahakamani
 
Kwa hiyo polisi waombe idhini kwa mhalifu ili wamchunguze?
Yap! Taratibu za kisheria ziko hivyo, na mahakama itatoa amri, then uchunguzi unafuata.

Ila kibongobongo Polisi akitaka details, wahusika faster Kama upepo wanazitoa!!

Kama sheria zimewekwa kwa nini upande mmoja uzivunje makusudi?
Kama zina ukakasi wazitoe kabisa
 
Shaidi ambaye ni wakili katika kesi ya Mbowe kwa jina la Frank Kapara ameeleza kwa mlolongo mrefu uzoefu na utendaji wa kazi yake katika kampuni ya Tigo. Pia ameeleza jinsi gani anavyotoa taarifa za wateja kwa vyombo vingine pale anapohitajika kufanya hivyo. Maelezo yake anaonyesha ni rahisi sana kwa taarifa za wateja kutoka kampuni za simh kutolewa kwa vyombo kama polisi zinapotakiwa jambo ambalo si afya ksa faragha ya mawasiliano kwa wateja. Hali hiyo inaweza kuwa hivyo pia kwa mabenki.

Tatizo la upatikanaji kwa urahisi taarifa za wateja iwe kwenye mawasiliano, benki, hospitali au sehemu nyingine ni taarifa hizo kuweza kutumiwa vibaya na watu wenye nia ovu. Lakini pia kila binadamu anapenda na kuhusudu faragha. Hii ndio sababu imezifanya nchi nyingi zilizoendelea na kustaarabika kuweka sheria kali za kulinda siri za wateja hata za kawaida tu.

Pia duniani kuna ncho zinazotambulia kama nchi nzuri zaidi za watu kuhifadhi fedha zao na zimevutia watu wengi kutoka kila kona ya dunia kuhifadhi fedha zao. Nchi hizo ni pamoja na Panama, Cayman, Switzerland, Luxembourg, Seychelles,Singapore, Belize Ujerumani n.k. Sifa kuu katika nchi hizi ni utunzaji wa siri za wateja wao. Sifa hii imefanya nchi hizi kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kwa njia ya mitaji inayotumika kuziendeleza. Ili upate taarifa za mteja katika nchi hizi ni lazima usote sana mahakamani na majaji wajiridhishe kwamba kweli kuna ulazima huo jambo ambalo huwa nadra sana majaji kukubali.

Kesi ya Mbowe inayoendelea iliamshe bunge kama mhimili na chombo cha kutunga sheria, kuweka sheria madhubuti za upatikanji taarifa za wateja katika simu, mabenki, hospitali na huduma nyingine. Hii itasaidia sana pia kuvutuia uwekezaji kutoka nje.
Bubge halijawahi tunga sheria zaidi ya kupitisha kwa ndio miswada ya wizara
 
Yap! Taratibu za kisheria ziko hivyo, na mahakama itatoa amri, then uchunguzi unafuata.

Ila kibongobongo Polisi akitaka details, wahusika faster Kama upepo wanazitoa!!

Kama sheria zimewekwa kwa nini upande mmoja uzivunje makusudi?
Kama zina ukakasi wazitoe kabisa
Una uhakika sheria yetu ipo hivyo? Au unazungumzia sheria za wenzetu

Sheria yetu inataka tu sababu na ndicho hicho mawakili wanachombana shahidi kwa nini ametoa taarifa bila kuambiwa sababu
Na hiyo sio kwenye Makampuni ya cm tu hata kwenye Mabenki yetu ni hivyo hivyo ndio maana kuna kipindi watu walikuwa wanalalamika kuchukuliwa pesa zao na TRA kutoka kwenye akaunti zao bila ridhaa

Kwa hiyo hapo tatizo ni sheria zetu sio tigo
 
Hivi hakuna watendaji wa hivyo vyombo ulivyotaja wanaotumia vibaya madaraka yao?
Utawatambua kwa kuwaona??
Kama wapo au hawapo ni nani atasimama katikati kama refa kulinda maslahi na haki za kila upande??
Je, ni nani atafanya maamuzi kuwa muamala fulani ni batili mwingine ni halali??
Trust no one!
Sawa. Nimekupata.
Kama " There is NO ONE"
Then hakuna uchunguzi.
Maana hata ingekuwa Mahakama ni Refa btn maadam ni chombo cha serkali wanaweza kuomba taarifa kupitia mahakama kwa WELIDI au Pasipo WELIDI
 
Inapohitajika kufanya hivyo na hivyo vyombo ni muhimu sana kukawa na pande ya katikati ambayo itahakikisha haki na mahitaji ya wote yanazingatiwa na huo upande duniani kote katika nchi zilizoendelea na kustaarabika huwa ni Mahakama. Mahakama inapaswa kusimama katikati ya mteja, chombo cha dola na kampuni kuhakisha utaratibu na haki za mteja zinazingatiwa.
Imekaa vzr
 
Hivi hakuna watendaji wa hivyo vyombo ulivyotaja wanaotumia vibaya madaraka yao?
Utawatambua kwa kuwaona??
Kama wapo au hawapo ni nani atasimama katikati kama refa kulinda maslahi na haki za kila upande??
Je, ni nani atafanya maamuzi kuwa muamala fulani ni batili mwingine ni halali??
Trust no one!

kama umeshindwa kuwa na imani na mtumishi mmoja wa taasisi nje ya mahakama,nikukumbushe tu mahakama haiwndeshwi na malaika kuna watumishi hawa hawa msiokuwa na imani nao.

tuacheni kutafuta vichaka kwenye matatizo.
 
Kukwepa haya ni kutumia Whatsapp calls na calls za app nyingine. App kama snapchat hata sms ikishafunguliwa inapotea.
 
Naendelea kuwashangaa usioona udhaifu wa maelezo ya Wakili wa Tigo Alfred Kapala. Tatizo si kutoa taarifa Polisi, tatizo kubwa ni maelezo yake kuwa;
1.Siri za wateja wao si kipaumbele chao.
2.Taarifa inaweza kutolewa kwa yeyote akitaka hata mtu binafsi isipokuwa kama anahtaji taarifa ya mtu mwingine. Yaani Leo wewe ukijifanya ni Mimi na ukawa na vielelezo ni Mimi unapata taarifa zangu. Hili ni kweli kabisa wala hajadanganya. Ndo maana Tigo na Voda zimetumiwa sana na wezi (Ile hela tuma kwenye Namba hii) kuibia wateja. Mtu anapiga simu huduma kwa wateja Tigo kwa Namba nyingine anaomba Namba yake nyingine (ya mtu mwingine) isitishwe kwa muda simu ina tatizo na wao bila kujiridhisha wanaistisha na wezi wanatumia muda huo kuihamisha kwenda line nyingine na kuitumia kuibia marafiki na ndugu wa mteja wa awali. Huyu MWIZI anajifanya ni wewe una shida ya laki 5 umekamatwa au unaumwa kumbe Tigo wamemsaidia MWIZI kusajili line ya ndugu yako.
3.Kwa maelezo yake hata Polisi wasipofuata matakwa ya sheria kuomba taarifa za wateja, Tigo itawapa tu. Ndo maana kipindi Fulani kiongozi mmoja akamwambia Mkuu wa wilaya wa kike Nina taarifa zako zote maana mawasiliano yako hata ya usiku wa manane ninayo.
NB; Bado unaona wako sahihi?

ulitaka tigo wakubembeleze kwa uongo!!!weww kama ni mzee wa vimeo na unahisi usalama ni sifuri kuwepo tigo unaweza watema tu.

nenda hata benk kaulizie taarifa za mtu uone kama utapewa hata majina yake matatu.
ila polisi wakienda ni sekunde tu wanapewa.

hawawezi kwamisha upelelezi kwa kigezo cha privacy,privacy inadai wajibu kwanza ndipo isimame.
 
Mfano wako mbona ni tofauti... Umeongezea facts mpya...!
Kutaka kuua. Majambazi...
Je, kwenye namba ya Mbowe na transactions zake umesikia kokote kuwa alitaka kufanya hayo??
Kama umeiita ile ni "fact"
Baadae uchunguzi utakuja kuprove Mbowe si Mhalifu.
Then its over
 
Naona tuna Kizazi cha ajabu hujawahi kuona.
1. Kizazi chenye ushabiki tu
2. Kizazi kisichohoji logic
3. Kizazi kisicho weledi kazini
4. Kizazi kinachotumia madaraka vibya
5. Kizazi kisichotaka kujua serkali inafanyaje kazi zake.
6. Kizazi kisichohitaji kuwajibika
 
kuna ishu moja ili trend sana dunian hapo kati ya kigaidi, kuna gaidi mmoja wa mashariki ya kati huko alikamatwa na jeshi la marekani asa ushahidi ulikuwa kwenye iphone so ilibid iphone ifunguliwe ili ushaidi uonekane,. asa gaidi mwenyewe aligoma kufungua sim yake kwaiy jeshi la marekani liliomba kampuni ya apple wafungue passcode lkn mpka mwish apple waligoma kufungua kwa kuwa wenyewe wanatunza siri za wateja.. nafikir hapo utakuwa umelewa
Wakaipeleka Israel ikafunguliwa.
 
Naona kila mtu anazungumzia usiri kuhusu kutoa taarifa za wateja. Hili jambo sijaelewa, mfano ikitokea kuna jambo lolote baya linafanywa na mteja, kisheria imekaaje? Tigo inapaswa kumlinda mteja mmoja hata kama jambo lolote hatarishi linalenga wateja wengi?

Mmmh
Yaani mi nashindwa kuwaelewa watu,inamaana kama kuna gaidi linataka kulipua nchi asifuatiliwe mawasiliano yake kisa usiri?hakuna kitu kama hicho na mkumbuke kuna taasisi zilizopewa mamlaka haya kisheria ambao ni Polisi,Takukuru,hawa wanauwezo wa kuchunguza au kufuatilia kama kuna Jambo linaloweza kuhatarisha uslama wa raia na mali zao,sio kila mtu tu akiamua anaenda voda au tigo kuomba report ya mawasiliano yako NOPE.
 
Kampuni za simu huwa wanasikiliza maongezi ya wateja wao?
Mfano Kuna watu wanaka kukuua mleta mada wanawasiliana na simu kupanga wakuulie wapi unataka kampuni ya simu wasiripoti polisi kuhusu Hilo ili kunusuru maisha yako? Na wahusika wadakwe?

Ulinzi na Usalama wa watumiaji wa simu na wananchi ni wa kila mtu zikiwemo kampuni za simu

Jirani yako ukiona majambazi yamemvamia huhitaji kibali chake kuripoti polisi
 
Back
Top Bottom