Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,308
- 45,618
Shahidi ambaye ni wakili katika kesi ya Mbowe kwa jina la Frank Kapara ameeleza kwa mlolongo mrefu uzoefu na utendaji wa kazi yake katika kampuni ya Tigo. Pia ameeleza jinsi gani anavyotoa taarifa za wateja kwa vyombo vingine pale anapohitajika kufanya hivyo. Maelezo yake anaonyesha ni rahisi sana kwa taarifa za wateja kutoka kampuni za simh kutolewa kwa vyombo kama polisi zinapotakiwa jambo ambalo si afya ksa faragha ya mawasiliano kwa wateja. Hali hiyo inaweza kuwa hivyo pia kwa mabenki.
Tatizo la upatikanaji kwa urahisi taarifa za wateja iwe kwenye mawasiliano, benki, hospitali au sehemu nyingine ni taarifa hizo kuweza kutumiwa vibaya na watu wenye nia ovu. Lakini pia kila binadamu anapenda na kuhusudu faragha. Hii ndio sababu imezifanya nchi nyingi zilizoendelea na kustaarabika kuweka sheria kali za kulinda siri za wateja hata za kawaida tu.
Pia duniani kuna ncho zinazotambulia kama nchi nzuri zaidi za watu kuhifadhi fedha zao na zimevutia watu wengi kutoka kila kona ya dunia kuhifadhi fedha zao. Nchi hizo ni pamoja na Panama, Cayman, Switzerland, Luxembourg, Seychelles,Singapore, Belize Ujerumani n.k. Sifa kuu katika nchi hizi ni utunzaji wa siri za wateja wao. Sifa hii imefanya nchi hizi kuwa na ukwasi mkubwa wa kifedha kwa njia ya mitaji inayotumika kuziendeleza. Ili upate taarifa za mteja katika nchi hizi ni lazima usote sana mahakamani na majaji wajiridhishe kwamba kweli kuna ulazima huo jambo ambalo huwa nadra sana majaji kukubali.
Kesi ya Mbowe inayoendelea iliamshe bunge kama mhimili na chombo cha kutunga sheria, kuweka sheria madhubuti za upatikanji taarifa za wateja katika simu, mabenki, hospitali na huduma nyingine. Hii itasaidia sana pia kuvutuia uwekezaji kutoka nje.