Kesi ya Mbowe mashahidi wa jamuhuri hawaeleweki

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Huenda nikawa nimechelewa lakini nimeanza kuifatilia kesi ya Mbowe tangu ile kesi ndogo ya kesi kubwa china ya jaji aliyejitoa Siyani (sijui ndio anaitwa hivyo kama sijakosea).

Baada ya maamuzi ya kesi ndogo pia nimefuatilia pia ushahidi wa mashahidi wa jamuhuri katika kesi kubwa ambayo ndio inayoendelea sasa.

Katika hayo yoote naona mashahidi wa serikali wanajichanganya wenyewe kila shahidi naona anakuja na leke jipya.

*Kingai huyu ni mkuu wa msafara wa ukamataji ambaye hafamiwi na mama muuza mbege aliwapa watuhumiwa nyama choma na energy ambapo mahita hajui hilo.

*Muuza mbege mama wa watoto 10 yeye anasema wakamataji walikuwa watano na mkamataji mkuu alikuwa ni Afande Jumanne na Kingai hakuwa kwenye huo msafara na watuhumiwa walikamatwa wakiwa wamekaa wanakunywa bia na kusajili lain za simu lakini kwenye upekuzi hawakukutwa na hela wala kitambulisho .

*Kaaya mpiga picha wa Sabaya yeye anasema alikamatwa na noti bandia ambazo baadae walimrudishia baada ya kufutiwa kesi pia sio mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini picha zake zilisambaa akiwa na viongozi wakuu wa CCM halafu huyu jamaa ni rafiki mnafiki sana haiwezekani uishi na Sabaya halafu uwape watu ramani ili wamfanyie mabaya rafiki yako Halafu anasema alipanda gari ya Mbowe KUB wakati Mbowe alipokonywa hilo gari.

*Mahita ndio funga kazi sasa yeye kasema huyo muuza mbege hamjui na wao walikuwa sita kwenye ukamataji sio watano mara anasema sita mara mara watano mara Jaji anamtetea baadae Jaji anaumbuka hajazungumzia hajasema kuhusu kuwapa nyama choma na energy wanasema walitaka kuua viongozi wa serikali wataje Sabaya nani Sabaya nani Sabaya kwaiyo ni kiongozi sio viongozi.

Lakini Sabaya yupo jela miaka 30 na afande jumanne nasikia kwenye ule uzi wa kumuwekea mzee pembe za ndovu na huyo Jumanne yupo.

Kwa hayo yanayoendelea ndio nafahamu kuna watu wengi sana wapo jela kwa kesi za uongo uongo kama hizo hata yule bilionea mwenye mashamba ya mkonge kule tanga aliyefariki huenda nae ni hivi hivi.

Hii kesi imetufundisha na kutuonyesha mengi sana ambayo tulikuwa hatuyajui kuhusu mahakama na jeshi la polisi.


Hebu ongeza makosa mengine ambayo wewe umeyaona katika muendelezo wa hii kesi.
 
mtanyooka tu mashabiki wa Mbowe lazima muone makosa lakini sheria haiangalii ushabiki wa mtu
 
Huenda nikawa nimechelewa lakini nimeanza kuifatilia kesi ya Mbowe tangu ile kesi ndogo ya kesi kubwa china ya jaji aliyejitoa Siyani (sijui ndio anaitwa hivyo kama sijakosea)...
Umenifurahisha hapo Kwa Jaji na washtakiwa watano/sita. Jaji anatetea alimsikia Mahita akisema walikuwa na dereva. Haya soma alipoasema dereva, hapaoni. Msishangae Jaji anaandika vitu vingine kabisa.
 
mtanyooka tu mashabiki wa mbowe lazima muone makosa lakini sheria haiangalii ushabiki wa mtu
Wakala wa shetani upo.Mungu ni wetu sote.Alikuwepo Magufuri alikuwa na Jeuri na majivuno Kama wewe.Alikuwepo Makonda kibri alichokuwa nacho Ni zaidi yako.Sabaya kila dakika alijiona MUNGU.

MBOWE hata mkifunga ,Lumumba siyo Mbinguni.
 
Darasa lina upana wa futi 6 kwa futi 6 urefu, mwalimu anasimama nje ya darasa wakati wa kufundisha wanafunzi 24 huku wanafunzi wengine wamening'inia madirishani. Kutokana na ufinyu wa darasa imekuwa vigumu kumuelewa mwalimu.
 
Jamaa alishasema hapa wanajitahidi kufukia mashimo lkn ndio wanazidi kuharibu zaidi

 
mtanyooka tu mashabiki wa mbowe lazima muone makosa lakini sheria haiangalii ushabiki wa mtu
Sema CCM haiangalii uchadema, sio sheria, ingekuwa sheria inafuatwa Basi watuhumiwa wote wangeshaachiwa mda mrefu Sana!

Hili timbwili la ugaidi, Ni Vita ya CCM VS CHADEMA Mahakamani!
Uzuri wa CHADEMA Wana asset ya vijana wasomi wengi, vinginevyo Hali ingekuwa tete kuliko hii iliyopo sasa
 
Huenda nikawa nimechelewa lakini nimeanza kuifatilia kesi ya Mbowe tangu ile kesi ndogo ya kesi kubwa china ya jaji aliyejitoa Siyani (sijui ndio anaitwa hivyo kama sijakosea)

Baada ya maamuzi ya kesi ndogo pia nimefuatilia pia ushahidi wa mashahidi wa jamuhuri katika kesi kubwa ambayo ndio inayoendelea sasa

Katika hayo yoote naona mashahidi wa serikali wanajichanganya wenyewe kila shahidi naona anakuja na leke jipya

*Kingai huyu ni mkuu wa msafara wa ukamataji ambaye hafamiwi na mama muuza mbege aliwapa watuhumiwa nyama choma na energy ambapo mahita hajui hilo

*Muuza mbege mama wa watoto 10 yeye anasema wakamataji walikuwa watano na mkamataji mkuu alikuwa ni Afande Jumanne na Kingai hakuwa kwenye huo msafara na watuhumiwa walikamatwa wakiwa wamekaa wanakunywa bia na kusajili lain za simu lakini kwenye upekuzi hawakukutwa na hela wala kitambulisho

*Kaaya mpiga picha wa Sabaya yeye anasema alikamatwa na noti bandia ambazo baadae walimrudishia baada ya kufutiwa kesi pia sio mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini picha zake zilisambaa akiwa na viongozi wakuu wa CCM halafu huyu jamaa ni rafiki mnafiki sana haiwezekani uishi na Sabaya halafu uwape watu ramani ili wamfanyie mabaya rafiki yako Halafu anasema alipanda gari ya Mbowe KUB wakati Mbowe alipokonywa hilo gari

*Mahita ndio funga kazi sasa yeye kasema huyo muuza mbege hamjui na wao walikuwa sita kwenye ukamataji sio watano mara anasema sita mara mara watano mara Jaji anamtetea baadae Jaji anaumbuka hajazungumzia hajasema kuhusu kuwapa nyama choma na energy wanasema walitaka kuua viongozi wa serikali wataje Sabaya nani Sabaya nani Sabaya kwaiyo ni kiongozi sio viongozi

Lakini Sabaya yupo jela miaka 30 na afande jumanne nasikia kwenye ule uzi wa kumuwekea mzee pembe za ndovu na huyo Jumanne yupo

Kwa hayo yanayoendelea ndio nafahamu kuna watu wengi sana wapo jela kwa kesi za uongo uongo kama hizo hata yule bilionea mwenye mashamba ya mkonge kule tanga aliyefariki huenda nae ni hivi hivi

Hii kesi imetufundisha na kutuonyesha mengi sana ambayo tulikuwa hatuyajui kuhusu mahakama na jeshi la polisi


Hebu ongeza makosa mengine ambayo wewe umeyaona katika muendelezo wa hii kesi

Ila kumbuka refa ni wao

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
kuna kipande iki
1636200404433.png


1636200314213.png
 
Stori nyingine kwenye kesi huwa n kama changamsha genge kuelekea kwenye hukumu maana unaweza kumuuliza mtu kutokea sehem flan had sehem flan ni klmtr ngap? Akisema 9 na wakat ni 15 haimaanishi umemshinda hizo huwa zinakuaga ngonjera tu maana mashahidi wengine hata elimu huwa hawana ila Kuna vitu flan tu vinahitajika kutoka kwake kama ushahidi vikipatikana inatosha kabisa
 
Back
Top Bottom