Kesi ya Mbowe: Lembrus Mchome - Shahidi Mwaminifu

Misahafu inakataza kumshudia mtu yeyote uongo (kutoka 20:16).

Lembrus Mchome akifuatilia kesi ya Mheshimiwa Mbowe kama ilivyo kwa wengine, alisikia D/C Msemwa H4323 akitoa yake jinsi alivyowapokea watuhumiwa akiwa polisi Central. Hiyo ikiwa katika shauri la mwanzo la Adamoo.

"Nani hakujua kuwa ushahidi wa Adamoo kuteswa na kuchukuliwa maelezo nje ya muda ulikuwa wa wazi mno kuweza kutupiliwa mbali ki vile?"

Nani alidhani mahakama ya Jaji Siyani ingeweza kuamua kuwa Adamoo hakuteswa na kwamba eti alitoa maelezo yake kwa ridhaa yake na ndani ya masaa 4 tokea kukamatwa?

Bila shaka ndiyo maana hata mawakili utetezi hawakuona haja ya kuwekeza mno kwenye kuikataa DR aliyokuwa amekuja nayo Msemwa mahakamani.

Kesi ya Adamoo ilikuwa funzo.

Hivyo kuhakiki nyendo za Msemwa kwenye shauri la Ling'wenya sasa, lilikuwa ni jambo la lazima.

"Lembrus Mchome shahidi mwaminifu hakuwezi tena kuuvumilia upotoshaji huu wa wazi kabisa."

Kwani nani anapenda kwenda mahakamani au polisi?

Kwa hakika Lembrus Mchome aliifanya sehemu yake ya uwajibikaji uliotukuka, kikamilifu:

"Kujitolea kuja na kuithibitishia mahakama kuwa D/C Msemwa alikuwa polisi Oysterbay na si Central katika kipindi tajwa."

View attachment 2030337

Pamoja na yote, ashukuriwe Jaji Tiganga kwa kumwelewa vyema shahidi Lembrus Mchome.

Nani kama Mchome?
Huyo shahidi ni mpare!
 
Ni yupi miongoni mwa watanzania wa leo; just "mpita njia" asikiaye jirani yake akishuhudiwa uongo tena na vyombo vya dola vyenye kila aina ya silaha na mamlaka akasimama na kuiweka iliyo kweli tena kwa ujasiri mkuu hata kwa gharama ya maisha yake?

Si rahisi zaidi kusema hayanihusu mimi ngoja nikatafute ugali? Mchome amechagua kusimama pamoja na haki maana Mungu ni Mungu wa haki. Mungu ambariki sana shahidi mwaminifu Lembrus Mchome!
 
Back
Top Bottom