Kesi ya Mbowe: Kufanana na Kutofautiana kwa Barua ya Ling'wenya na DR ya Msemwa

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
16,451
2,000
Kesho ni kesho asiye na mwana na akaeleke jiwe.

Kesho Mh. Jaji Tiganga atatoa hukumu yake kuihusu barua ya Mohammed Ling'wenya.

Kama ilivyokuwa kwa DR na shahidi Jumanne, ilipingwa mahakamani. Hukumu ya Jaji ikaonyesha nini kilitakiwa kifanyike ili iweze kukubalika.

Bila ya ajizi WS Chavula, Kidando na timu yao wakaitumia fursa hiyo na DR ikapokelewa masharti na vigezo vya Jaji vikizingatiwa kupitia kwa shahidi Msemwa.

"Hii ikiwa ni pamoja na kuwa Msemwa hakuwa ameiomba DR hiyo kutokea popote wala kusaini kokote kwa ajili ya kuipokea."

Haiyumkiniki basi, kama ilivyokuwa kwa DR Mh. Jaji kama ataikataa ya Ling'wenya basi ataainisha nini kifanyike.

Kila na kheri kwao mashahidi wajao (bila ya shaka) Adamoo na Mama Ling'wenya. Kwani jukumu la kuimalizia penalti hii laweza kuwafikia wao.

Ama kwa hakika suala la barua ya Ling'wenya kama lilivyokuwa la DR ya Jumannena hatimaye Msemwa, yanafanana sawia.

Kwa hakika barua hii inapaswa kuingia mahakamani kwa namna ile ile ya DR.

Kwa mara nyingine barua hii itaiweka dhamira ya Mh. Jaji na mahakama kuelekea haki na usawa kuendelea kudhihirika.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
37,282
2,000
AIgmal.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom