Kesi ya Mbowe: Jaji hana mamlaka na document yenye wrong citation. Court of Appeal ilishaonya mara nyingi

Kisanduku

JF-Expert Member
Jul 9, 2009
284
482
Leo (Nov 8. 2021) umetokea ubishi mahakamani kwamba akina Kibatala wamekataa document ya kumkamata mshitakiwa (seizure).

Hoja ni kwamba sheria kwenyw document hiyo haipo hapo nchini.

Kosa hilo kisheria linaitwa "wrong citation of the law".

Mawakili wa Serikali wamejenga hoja kwamba hili kosa ni dogo, siyo fatal, yaani mahakama inaweza kulifumbia macho.

Kina Kibatala wanasema ni kosa kubwa, yaani hakuna sheria hiyo waliyotumia.

Jaji kaomba siku nzima kuchambua hoja zote.

Je, ni nini kiko sahihihi?

Je, msimamo wa sheria zetu ukoje kwa kosa hili la wrong citation?

Msimamo uko wazi kwamba wrong citation ni kosa lisilovumilika. Mahakama haina mamlaka na kesi yako kama umefanya kosa la wrong citation.

Msimamo huu Majaji wote Tanzania wameusimamia.

Msimamo huu ni wa Mahakama ya Rufani kwenye kesi zake nyingi. Moja ya kesi hizo ni ile ya "Chama Cha Walimu Tanzania v. The Attorney General, Civil Application No. 151 of 2008, (Unreported) ".

Katika kesi hii Court of Appeal olitamka wazi kwamba wrong citation ni kosa lisilosameheka.

Hivyo Mahakama Kuu haina uwezo wa kukiuka maagizi ya Mahakama ya Rufani kama Mawakili wa Serikali wanavyojaribu kuishawishi.

Jaji wa kesi ya Mbowe hana mamlaka ya kwenda kinyume na Mahakama ya Rufani.

Jailing.
 
Mawakili wa serikali ni wasanii sana, wasingeweza kufaulu mitihani yao law school kama wangejibu kwa wrong citation, wanaipotezea mahakama muda wake bure wakijua watabebwa na jaji wao.

Huko mahakamani huwa wana msemo wao; "mahakama sio mama yako, haiwezi kukupa kitu ambacho hukuiomba".
 
Hili suala la kuomba siku nzima kupitia hoja za pande zote, Ni kujipa muda wa kuangalia namna iliyobora ya kupindisha pindisha ukweli kuwa uongo na hoja ya mawakili wa utetezi itupiliwe mbali!

Hawa majaji wa kupindisha pindisha washindwe na walegee!! Na aibu iwapate milele!

Majaji wanaosimamia haki na misingi
Ya sheria, Mungu awainue na nyota zao zing'ae milele na milele!
 
"WRONG CITATION" kwa wasiojua maana yake ni kumshitaki au kufanya maamuzi ya kisheria kwa kutumia SHERIA ISIYOSIMAMA na KOSA ANALOTUHUMIWA ÑALO MTUHUMIWA au KUFANYA MAAMUZI YA HUKUMU kwa SHERIA ISIYOKUWEPO...

Katika scenario hii ya leo ni kwamba shahidi Na. 8 wa upande wa mashitaka ambaye ni askari Polisi Jumanne aliwakamata na kuwapekua watuhumiwa na kuchukua [seize] mali zao kinyume cha sheria au kwa kutumia sheria isiyosimamia mchakato huo...

Na ktk kuthibitisha kuwa huyu polisi alifanya kosa la kisheria, katika maelezo yake akanukuu sheria au kifungu sheria cha sheria alichotumia kimakosa au ambacho hakipo kabisa ktk sheria za Tanzania...

Duuh, what a fatal mistake is this...!!!

Sasa ngoja tuone, Jaji atawasaidia vipi jamhuri....
 
Huyo Judge kwa wenye kuona kwa jicho la 3 elimu ya darasa la nne tu inatosha kujua ni wa namna gani.
JAJI WA KIMKAKATI huyo, aliwekwa na mwendazake kwaajili ya kazi moja tu. Kuhujumu upinzani na akina Mbowe kwa namna yeyote ile. Subiri uone maamuzi yake hiyo kesho.
 
Tatizo ni kwamba, anachokiamia Leo...siku chache zijazo, kitatumikia kuamua kesi ya MTU mwingine

Nandio maana watu wengi wamefungwa kwa sababu kuna makosa ambayo yalifanywa na majaji wapenda matumbo kama hawa!
Basi huyu jaji atakuwa ameweka record mpya kuwahi kutokea, tutamwingiza kwenye kumbukumbu ya historia ya matukio ya nchi!
 
Leo (Nov 8. 2021) umetokea ubishi mahakamani kwamba akina Kibatala wamekataa document ya kumkamata mshitakiwa (seizure).

Hoja ni kwamba sheria kwenyw document hiyo haipo hapo nchini.

Kosa hilo kisheria linaitwa "wrong citation of the law".

Mawakili wa Serikali wamejenga hoja kwamba hili kosa ni dogo, siyo fatal, yaani mahakama inaweza kulifumbia macho.

Kina Kibatala wanasema ni kosa kubwa, yaani hakuna sheria hiyo waliyotumia.

Jaji kaomba siku nzima kuchambua hoja zote.

Je, ni nini kiko sahihihi?

Je, msimamo wa sheria zetu ukoje kwa kosa hili la wrong citation?

Msimamo uko wazi kwamba wrong citation ni kosa lisilovumilika. Mahakama haina mamlaka na kesi yako kama umefanya kosa la wrong citation.

Msimamo huu Majaji wote Tanzania wameusimamia.

Msimamo huu ni wa Mahakama ya Rufani kwenye kesi zake nyingi. Moja ya kesi hizo ni ile ya "Chama Cha Walimu Tanzania v. The Attorney General, Civil Application No. 151 of 2008, (Unreported) ".

Katika kesi hii Court of Appeal olitamka wazi kwamba wrong citation ni kosa lisilosameheka.

Hivyo Mahakama Kuu haina uwezo wa kukiuka maagizi ya Mahakama ya Rufani kama Mawakili wa Serikali wanavyojaribu kuishawishi.

Jaji wa kesi ya Mbowe hana mamlaka ya kwenda kinyume na Mahakama ya Rufani.

Jailing.
Jaji Tiganga akipindisha nahii, basi kama alivyoshauri Lema, Mbowe anyamaze na mawakili wajitoe. Waamue wamfunge dunia ishuhudie ushenzi
 
Back
Top Bottom