Kesi ya Mbowe inanikumbusha mbwembwe za Wakili msomi Lakha katika kesi ya Uhaini miaka ile ya 1980s

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,616
141,445
Kesi ya Ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA Mh Mbowe itakuwa ni darasa zuri la Sheria kwa wanaopenda kujifunza kwa njia ya vitendo siyo nadharia.

Sisi wahenga tulijifunza mengi katika kesi ya Uhaini iliyowakabili hawa akina Hans Pope wa Simba na wenzake waliotuhumiwa kutaka kumpindua Rais Nyerere wakati ule

Darasa lingine dogo la Sheria liko pale Arusha kwenye kesi ya Ole Sabaya

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Moja kati ya kesi kubwa kuwahi kutokea za wapambania haki ni Rivonia Trial kesi ya Mandela.....The kapengeria six kesi ya Joni Kenyata wakati wa maumau na
 
Kesi ya Ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA Mh Mbowe itakuwa ni darasa zuri la Sheria kwa wanaopenda kujifunza kwa njia ya vitendo siyo nadharia.

Sisi wahenga tulijifunza mengi katika kesi ya Uhaini iliyowakabili hawa akina Hans Pope wa Simba na wenzake waliotuhumiwa kutaka kumpindua Rais Nyerere wakati ule

Darasa lingine dogo la Sheria liko pale Arusha kwenye kesi ya Ole Sabaya

Mungu ni mwema wakati wote!
Ukimtaja tuu Wakili Murtaza Lakha, unanikumbusha mbali, Lakha ndiye alikuwa wakili wa late Mzee wangu, Mzee Andrew Mayalla (RIP), ndio alikuwa RSO wa Mwanza ile 1976 wakati kulitokea mauaji ya vikongwe. Katika kuwasaka wauaji, ikafanywa operation maalum, kituo cha mahojiano ni eneo la Kigoto.

Kuna watuhumiwa wawili, Masaga Mahulu Mazegenuka na Issack Ng'wana Ng'hoboko, walifariki. Kutokana na kadhia hiyo, Waziri wa Mambo ya ndani wa enzi hizo Ali Hassan Mwinyi aliachia ngazi, Waziri wa Usalama, Peter Siyovelwa aliachia ngazi. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, Emilio Mzena, IGP, Pundugu, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Peter Kisumo walistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mzee, Mayalla aliyekuwa RSO wa Mwanza, RPC wa Mwanza, DSI na OCD . Mzee alitetewa na wakili Murtaza Lakha na ndie pekee alichomoka, the rest walikula mvua nyingi.

Kufuatia hiki kilichotokea Mwanza 1976, Nyerere alikasirika sana ndio akaifuta katiba ya kikoloni tulioirithi na kuleta katiba ya kama ya 1977 hii iliyopo mpaka hii leo.

Yale maswali yangu ni maswali ya ki Lakha Lakha, kama hauko vizuri, unaweza kukimbia!.

RIP Mzee Mayalla, RIP Wakili Murtaza Lakha.

P
 
Back
Top Bottom