Ole jaminati
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 226
- 200
Watu wameishapata promotion zA vyeo lazima waminye haki lkn wajue hawawez kuwa viongozi milele na malipo hapa hapa dunianHaki haijawahi kujificha.
Jaji Siyani kwa kujiridhisha kuwa:
1. Mshitakiwa wa pili alikamatwa akawasaidia polisi kumtafuta Mosses Lijenje Moshi, Boma Ng'ombe hadi Arusha,
2. Njiani wakapata mishikaki na Mo Energy,
3. Mshitakiwa wa pili akatoa maelezo kwa ridhaa yake ndani ya masaa 4 yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria,
4. Kwamba madai ya kuteswa kwa washitakiwa yalikuwa ni porojo tu,
Kama ilivyo kwa misahafu kuweza kutumika kufikia hitimisho lolote, ama kwa hakika Jaji Siyani hakubakia nyuma:
1. Jaji hakutaka kujishughulisha kujua walikuwa wapi wahanga wengine wa yaliyosemekana mateso Moses Lijenje au Luteni Urio,
2. Jaji hakutaka kujishughulisha wala kuhitaji uthibitisho wa madaktari kujiridhisha madai ya kuteswa ya washitakiwa.
"Kwa hukumu hii Sirro, Kingai, Mahita na polisi kwa ujumla mmepewa leseni ya kuuwa nzi. Kuwa uweni nzi wote popote mtakapowaona. Jaji Kiongozi mpya kawapa ruksa hiyo."
Haki kuonekana hadharani ikiporwa ni pigo kwa utawala wa sheria.
Kwa hakika leo imekuwa ni siku mbaya kabisa kwa mahakama na utawala wa sheria hapa nchini.