liwaya
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 2,378
- 1,627
Very brief summary nimekupenda bure kutoa mwenendo wa kesi ulivyoTakribani mashahidi wanne hadi sasa wameshatoa ushahidi wao lakini kati ya hao wote sijaona ushahidi wenye nguvu ya kuwatia hatiani watuhumiwa wa ugaidi.
Shahidi badala ya kuthibitisha uhusiano wa silaha iliyokamatwa na mtuhumiwa anakuja kutuambia silaha zilizokamatwa ni nzima kwani silaha kuwa nzima ni uthibitisho kuwa hiyo silaha ni ya mtuhumiwa.
Shahidi anasema alikutana na Mbowe January 2020 akiwa na gari la KUB wakati Mbowe alinyang’anywa gari tangu 2019 na January 2020 alikuwa mahabusu.
Shahidi anasema saini zinatofautiana kwasababu zingine alisaini akiwa amesimama zingine akiwa amekaa.
Mwingine anasema hakumbuki rangi ya shati maana hakuvaa miwani lkn aliweza kuona rangi ya bastola na kusoma namba zake.
Shahidi mwingine anasema watuhumiwa walipanga kulipua vituo vya mafuta, kukata miti, kupulizia viongozi sumu na kuua viongozi, walipoulizwa mliwakuta na vilipuzi hakuna, mapanga au shoka za kukatia miti hakuna, kuna vituo vya mafuta vilivyolipuliwa hakuna, kuna kiongozi kauawa hakuna.
Labda kama wamepanga kumfunga Mbowe wamfunge tu tujue moja lkn kwa ushahidi huu wa kuhisi kwa kesi kubwa kama hii ni kumuonea bure.