Kesi ya Mbowe: Hadi sasa sijaona ushahidi wowote unaoonesha kulikuwa na ugaidi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Takribani mashahidi wanne hadi sasa wameshatoa ushahidi wao lakini kati ya hao wote sijaona ushahidi wenye nguvu ya kuwatia hatiani watuhumiwa wa ugaidi.

Shahidi badala ya kuthibitisha uhusiano wa silaha iliyokamatwa na mtuhumiwa anakuja kutuambia silaha zilizokamatwa ni nzima kwani silaha kuwa nzima ni uthibitisho kuwa hiyo silaha ni ya mtuhumiwa.

Shahidi anasema alikutana na Mbowe January 2020 akiwa na gari la KUB wakati Mbowe alinyang’anywa gari tangu 2019 na January 2020 alikuwa mahabusu.

Shahidi anasema saini zinatofautiana kwasababu zingine alisaini akiwa amesimama zingine akiwa amekaa.

Mwingine anasema hakumbuki rangi ya shati maana hakuvaa miwani lkn aliweza kuona rangi ya bastola na kusoma namba zake.

Shahidi mwingine anasema watuhumiwa walipanga kulipua vituo vya mafuta, kukata miti, kupulizia viongozi sumu na kuua viongozi, walipoulizwa mliwakuta na vilipuzi hakuna, mapanga au shoka za kukatia miti hakuna, kuna vituo vya mafuta vilivyolipuliwa hakuna, kuna kiongozi kauawa hakuna.

Labda kama wamepanga kumfunga Mbowe wamfunge tu tujue moja lkn kwa ushahidi huu wa kuhisi kwa kesi kubwa kama hii ni kumuonea bure.
 
Ni kweli ushahidi wa jamhuri juu ya suala hili haueleweki na sisi bush lawyers tunasema mpaka sasa Mbowe yuko huru..

Tuiachie mahakama itoe maamuzi dhidi ya Mbowe, maamuzi ya mahakama ndio yatatoa njia nini kifanyike ili Mbowe apate haki yake.

Kama mahakama itamuachia huru basi afungue shauri kudai fidia kuuubwa na kusafishwa kupitia magazeti yote yakilipiwa na jamhuri kichwa cha habari kisomeke MBOWE SIO GAIDI ALISINGIZIWA TU kwa muda wa miezi sita.
 
Ujue haifurahishi hata kidogo yaani mashahidi wote hakuna hata mmoja aliyeleta ushahidi wenye mashiko badala yake wamegeuka kuwa komedian.

Terrorism eti na mambo ya utalii, Mara walikuwa watatu wamekaa wanasajili laini wakati huohuo walikuwa wanaongea simu huku wanatembea wanaenda mwelekeo huu wanaenda mwelekeo ule.

Mara walikuwa wanakunywa pombe kichekesho sijui pombe walipewa bure wakati mwenye bar na wanatuhumiwa hawafahamiani.

Mara alikuwa na simu moja ya tecno mara ooh alikuwa na smartphone. Haya kwenye muda wa tukio mbona nako kichekesho
 
Mpaka leo bado sijaelewa lengo mahsusi la yale mahojiano kati Salim Kikeke na huyu Mama! Na wakati huo huo mchakato wa kesi ukiwa unaendelea mahakamani.

The way alivyokuwa anajieleza mbele ya camera siku ile! Namna alivyo elezea kwa kujiamini!, na ukija kwenye uhalisia! unaona kabisa aina ya Mtawala tuliye naye.
 
Hadi sasa hakuna ushahidi wowote wa kigaidi dhidi ya Mbowe.

Wanachofanya serikali ni 'kutengeneza' mashihidi wasio na ushahidi.

Kwa ufupi ni kesi inayowavua nguo 'washtaki' na kuwaacha uchi!

Pesa za walipa kodi zinapotea kwa mambo ya kipuuzi na ujinga mtupu
 
Wakili wa Serikali: Shauri linakuja kwa ajili ya Kusikilizwa. Mpaka Jana Jioni tulipata Shahidi ambaye tulipanga Kuja naye Leo. Lakini Asubuhi amepata Tatizo la Ki Afya lililosababisha Kushindwa Kuja Mahakamani. Kwa sababu hiyo tunaomba Hairisho Mpaka Kesho

Jaji: kuzingatia maombi yalitolewa na wakili mwandamizi Robert Kidando shahidi kushindwa kufika mahakamani

Na kuzingatia ukweli kwamba maombi hayo hayajapingwa na utetezi

Nahairisha Shauri mpaka kesho saa 3 ambapo upande wa mashtaka mnaaelekezwa kuleta mashahidi

Jaji anatoka!

Zingati walisema wana mashahidi 24, hadi sasa ni 5 tu ndio wametoa ushahidi wao.
 
Back
Top Bottom