Kesi ya Mbowe: Commando Mhina, Shahidi Mwaminifu na Rafiki wa Kweli

Umeandika nini sasa hapo? Huyo Komando uchwara ni unfit kwa wale wako jeshini watajua vizuri maana ya Unfit. Ndiyo maana alifukuzwa Jeshini na ndiyo maana tena akalengeshwa na Urio kwa Gaidi Mbowe.

Komando kweli kweli hafukuzwi Jeshini akifanya makosa ya nidhamu anafungwa huko huko Jeshini na ikibidi kama bado anazigua anapelekwa vitani akakione chamoto, nafikiri unajua ninaposema vitani!!

Makomando walikuwa wakina Tamimu hata ukamataji wao ulikuwa kimbembe siyo hao wanakamatwa Rau sokoni hahahahaha... hapo kuna shield kibao tena wanakamatwa na askari watatu tu mmmmmh. Hao ni unfit commandos!!

Madawa ya kulevya yalishawamaliza stamina pamoja na uwezo wa akili zao za kufikiria ndio maana Urio akamwingiza mkenge Gaidi Mbowe.
Kamwambie shangazi yako akupeleke ukasalimie kaburi la baba ako Mana hata hulijui mtoto wakambo ww
 
Umeandika nini sasa hapo? Huyo Komando uchwara ni unfit kwa wale wako jeshini watajua vizuri maana ya Unfit. Ndiyo maana alifukuzwa Jeshini na ndiyo maana tena akalengeshwa na Urio kwa Gaidi Mbowe.

Komando kweli kweli hafukuzwi Jeshini akifanya makosa ya nidhamu anafungwa huko huko Jeshini na ikibidi kama bado anazigua anapelekwa vitani akakione chamoto, nafikiri unajua ninaposema vitani!!

Makomando walikuwa wakina Tamimu hata ukamataji wao ulikuwa kimbembe siyo hao wanakamatwa Rau sokoni hahahahaha... hapo kuna shield kibao tena wanakamatwa na askari watatu tu mmmmmh. Hao ni unfit commandos!!

Madawa ya kulevya yalishawamaliza stamina pamoja na uwezo wa akili zao za kufikiria ndio maana Urio akamwingiza mkenge Gaidi Mbowe.
Saguda47 amelike
 
Tanzania watu wake ni wakatili sana daah mpaka roho inasisimka hayo mambo wanayofanya ya utesaji ni kama makaburu tuu..
 
Ingekuwa nchi nyingine wangeambiwa "Thank you for your service"
 
Hakika
Hukusikia baadhi yao ni wakulima wa mahindi baada ya kufikuhwa kwa kuathirika kazini?

Hata kama kuna kazi ya maana maana mahali kwenu ikawa nongwa.

Kwa hiyo taabu yenu ilikuwa husuda tu ya kwa nini Mbowe alindwe na makomando. Hiyo ndiyo ikawa kisa tukafikishana huku:

View attachment 2031909

Kwa kweli mu waovu kweri kweri kuliko shetani mwenyewe!
 
Komando Mchina popote pale alipo na apokee salamu za kheri kutoka kwetu tunaoyaishi machungu yao.

Akiwa mtu huru, Commando Mhina alifika mahakamani kufanya sehemu yake ya kuuanika ukweli.

"Kwani nani anapenda kufika kwa ridhaa yake polisi au katika mahakama zinazosifika kwa dhuluma?"

"Kwa nini Commando Ling'wenya au awaye yote ahukumiwe kwa ushahidi wa uongo?"

Kama ilivyokuwa kwa ma Commando Ling'wenya, Adamoo, Malema, Urio, na Lijenje, Commando Mhina pia alikamatwa na kundi la akina Kingai, Jumanne, Mahita na Goodluck.

"Akihojiwa na wakili msomi Peter Kibatala 5/11/2021," Mahita Omar Mahita alikiri:

View attachment 2031579

Kwa maelezo ya Commando Mhina, kulikuwa na convoy kubwa kwenye kukamatwa kwake iliyokuwapo hapo bila kujihusisha moja kwa moja. Ikiwa tayari tayari kama angejaribu kujitetea.

Kwenye mazingira kama hayo haipo namna ambayo Commando Lijenje angeweza kutoweka RAU madukani.

View attachment 2031663

Commando Mhina alikamatwa akielekea Pub akapelekwa Central Polisi Tabora, moja kwa moja kwenye kinyumba nyuma ya jengo kuu (main block) kwenda kuteswa.

Baada ya kipigo kikali (cha masaa yasiyopungua 3) alipelekwa mahabusu Tabora Railways alikokaa kwa siku 2, kabla ya kuhamishiwa Nzega polisi mahabusu, alikokaa kwa siku 3.

Nzega, Mhina alikutana pia na Commando Malema aliyekuwa kaletwa hapo mahabusu polisi kwenye mazingira kama aliyofikishwa nayo hapo, yeye.

Makomando wawili hawa walisafirishwa kuja Dar chini ya ile ile himaya pendwa ya akina Kingai, Jumanne, Mahita, na Goodluck, ambako walifikishiwa 23/9/2020 moja kwa moja mahabusu Polisi Tazara.

Tokea 19/9/2020 Commando Mhina alipokamatwa na kufungwa pingu, hakuwahi kufunguliwa pingu hizo wala kupewa chakula hadi alipopelekwa mahakamani kisutu 25/9/2020.

Katika kipindi chote hicho hakuwahi kusajiliwa katika kitabu au register yoyote popote.

Wana nini cha kumwambia nani dhidi ya nani kina Kingai, Mahita, Jumanne au Goodluck naye akawaamini?

Bila shaka ni watu hawa hawa walio mkamata pia Mh. Mbowe usiku usiku Mwanza na kumsafirisha kuja naye Dar kibazazi wakimwahidi kuwa safari hii hachomoki.

Wapongezwe wote wanaokuwa na ujasiri wa kusimama imara kuufichua uongo dhidi ya ukweli.

Maisha na haki za watu haziwezi kuchezewa kwa kisingizio cha jina "serikali" kwa kiwango hiki. Kwani serikali hiyo itakuwa ina mwakilisha nani?

Nani kama Commando Mhina?

"Kudos Commando Mhina. Kwa hakika wewe ni shahidi wa haki na Rafiki mwema."

"Kwa hakika wapenda haki wote tutasimama nanyi kuona haipo haki yenu moja itakayopotea."

-----------
Sauti na Zipazwe Zaidi:

"Wako wapi makomando wetu. Wako wapi Urio, Malema na Lijenje ambao tunajua mara ya mwisho walikuwa mikononi mwa Kingai."
Unawatesa wtz wenzako ili upate nn na ufaidike na nn lkn malipo ni hapa hapa dunian hao watesaji zam yao itafika tu ni suala la muda katiba mpya ni muhimu saan
 
Una laana wewe si bure! Madaktari waliomtibu waliweka wazi ugonjwa uliomwua!! Siyo corona!! Usilazimishe mawazo yako ya kiibilisi!! Corona Haina nguvu kabisa Tz kwa sababu raid wa awamu ya Tano alimtanguliza Mungu katika vita dhidi ya corona na Mungu akasikia maombi yetu. Ndio maana uko hai Leo na corona unaisikia tu kwenye vyombo vya habari lakini kwenye jamii yetu haipo kabisa! Lakini Kama ukiamua kuishabikia itakuja kwako tu wakati watanzania wengine wakibaki salama!!.
Msukule wa jiwe
 
Mie mwenyewe nilishangaa sana comandoo unakamatwaje kizembe asee, tena kwenye pub za kuangalia mpira.... Wamedhalilisha sana fani ya ukomandoo..
Binafsi sielewi kwanini mbowe aliamua kuajiri hawa jamaa waluokua wamefukuzwa jeshini kwasababu mbalimbali....
Au siyo? wakati Hamza aliamua asikamatwe na Mpumbavu yeyote Yule.
 
Unawatesa wtz wenzako ili upate nn na ufaidike na nn lkn malipo ni hapa hapa dunian hao watesaji zam yao itafika tu ni suala la muda katiba mpya ni muhimu saan

Kwamba Samia kafunga kabisa macho na masikio anaangalia mitano yake mingine tu.

Ngoja tuone ..
 
Tanzania watu wake ni wakatili sana daah mpaka roho inasisimka hayo mambo wanayofanya ya utesaji ni kama makaburu tuu..

Kwa hakika ni heri hata makaburu.

Kingai, Mahita, Jumanne, na Goodluck si wa kufumbia macho hata ichukue muda gani.
 
Umeandika nini sasa hapo? Huyo Komando uchwara ni unfit kwa wale wako jeshini watajua vizuri maana ya Unfit. Ndiyo maana alifukuzwa Jeshini na ndiyo maana tena akalengeshwa na Urio kwa Gaidi Mbowe.

Komando kweli kweli hafukuzwi Jeshini akifanya makosa ya nidhamu anafungwa huko huko Jeshini na ikibidi kama bado anazigua anapelekwa vitani akakione chamoto, nafikiri unajua ninaposema vitani!!

Makomando walikuwa wakina Tamimu hata ukamataji wao ulikuwa kimbembe siyo hao wanakamatwa Rau sokoni hahahahaha... hapo kuna shield kibao tena wanakamatwa na askari watatu tu mmmmmh. Hao ni unfit commandos!!

Madawa ya kulevya yalishawamaliza stamina pamoja na uwezo wa akili zao za kufikiria ndio maana Urio akamwingiza mkenge Gaidi Mbowe.
wewe ni mjinga sana.
 
Hakika kila mtu bado ana bakiwa na maswali kadha wa kadha!
Hakuna ugaidi pale kesi ile ilikuwa ya muda mrefu ilifunguliwa kabla ya uchaguzi na ilifanyika vile sababu jiwe alijiandaa kuharibu Nchi so walijua Chadema hawatakubali kama ulikuwa unafuatilia kauli za LISU so ilikuwa kujihami baada ya uchaguzi walikamatwa LEMA... MBOWE na BONIFACE nyakati yuko yule mwehu mwenye tumbo kubwa kama pipa la Chibuku akawa anaenda tbccm kutoa ushahidi wa namna Mbowe alivyotaka kulipua vituo vya mafuta....mwisho jiwe akaamua kuipotezea baada ya kugundua watu hawakuwa na mawazo hayo.so wakaachiwa...kumbuka nyakati hizo hao makomandoo tayari walikuwa nyavuni.... miongoni mwa sababu nyingi za Mbowe kutaka kukutana na Samia ilikuwa ni kuomba kuachiwa kwa hao makomandoo
 
Wafuasi wa chaggadomo ni kama wamedata aisee. Wote ukiwangalia ni kama wamerukwa na akili.
 
Hakuna ugaidi pale kesi ile ilikuwa ya muda mrefu ilifunguliwa kabla ya uchaguzi na ilifanyika vile sababu jiwe alijiandaa kuharibu Nchi so walijua Chadema hawatakubali kama ulikuwa unafuatilia kauli za LISU so ilikuwa kujihami baada ya uchaguzi walikamatwa LEMA... MBOWE na BONIFACE nyakati yuko yule mwehu mwenye tumbo kubwa kama pipa la Chibuku akawa anaenda tbccm kutoa ushahidi wa namna Mbowe alivyotaka kulipua vituo vya mafuta....mwisho jiwe akaamua kuipotezea baada ya kugundua watu hawakuwa na mawazo hayo.so wakaachiwa...kumbuka nyakati hizo hao makomandoo tayari walikuwa nyavuni.... miongoni mwa sababu nyingi za Mbowe kutaka kukutana na Samia ilikuwa ni kuomba kuachiwa kwa hao makomandoo

Nchi inanuka dhuluma:

1. Kesi hii kufutwa
2. Makomando wote kuachiwa
3. Kuwahikiki makomando wote waliotoweka
4. Kulishughulikia genge dhwalimu la kuna Kingai lililohusika na ukikwaji mkubwa huu wa haki
5. Kuwalipa fidia wahanga wote wa kadhia hii
6. Kufumuliwa kwa jeshi la polisi
7. Kuhakiki haki na ustawi wa makomando wote walioondoshwa jeshini
8. Nk.

Inaweza kusaidia kupoza chungu ya vidonda sugu vilivyomo mioyoni mwa watu.

Alaaniwe jiwe na washirika wake kokote kule waliko.
 
Back
Top Bottom