Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,396
Wazee wa baraza katika kesi ya mauaji ya mwafrika mmarekani George Floyd wanatarajiwa kurejea mchana huu na majibu ya hatia kwa mashtaka yote matatu.

Derek Chauvin ambae alikuwa askari polisi alimwekea goti shingoni George Floyd kwa dakika tisa na sekunde 29 alipokuwa akimkamata na kusababisha ukosefu wa hewa kwake hali ilompelekea kufariki.

Matarajio ya hukumu ya kukutwa na hatia kwa Wazee hao kunatokana na kutochukua muda mrefu wa kutafakari kila kosa kati ya matatu yanomkabili Derek Chauvin.

Kesi hiyo ya mauaji inafanyikia katika jiji la Minneapolis katika jimbo la Minnesota.

Chauvin anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni mauaji ya bila kukusudia katika daraja la pili kosa linalobeba miaka 40 ya kifungo. Kosa la pili ni mauaji kwa kudharau taratibu na kanuni za kazi miaka 25 na kosa la tatu ni linabeba miaka 10 ambalo ni kusababisha kifo kwa kuweka goti kwenye shingo ya George Floyd bila kuzingatia hali ya muathirika.

Chanzo:

Vyanzo mbalimbali vya habari.

Update:

1618975900092.png

Derek Chauvin akielekezwa kwenda nje ya mahakama akiwa amefungwa pingu mara baada ya kusomewa uamuzi wa kukutwa na hatia ya mauaji ya George Floyd: Picha na Reuters

Derek Chauvin amekutwa na hatia ya mashtaka yote matatu na hukumu itatolewa baada ya wiki nane.

Wazee wa baraza walikaa karibu masaa kumi na nusu kufikiri na kupima uzito wa mashtaka yalowasilishwa na upande wa mashtaka kwenye mahakama na hakimu mkazi ya Hennepin jijini Minneapolis katika kesi hiyo ilochukua wiki tatu.

Chauvin alikuwa akikabiliwa na mashtaka matatu ta kumuua George Floys baada ya kumwekea goti katika shingo yake tarehe 25 mwezi March mwaka 2020, tukio lilozua maandamano nchini Marekani na kuungwa mkono duniani kote.

Chauvin mwenye umri wa miaka 45, anatazama miaka 75 jela ikiwa atatumikia miaka yote iliomo kwenye kila shtaka kwa pamoja.

Ikiwa kila shtaka litatumikiwa kivyake , Chauvin atatumikia kifungo cha miaka 25 jela kwa kila shtaka.
 
Hii kesi itakuja kutumiwa kama mfano wa miongoni mwa kesi ambazo maamuzi yake yamekua influenced na hali ya nje ya mahakama.

Askari wakavunja goti.

Ligi za mpira wanavunja goti.

Black Tuesday.

Rais akavunja goti.

N.k.

Sioni akipona
 
Nawaona Wazungu na Weusi wanakumbatiana huku wakilia kwa furaha ya hukumu na majonzi ya namna George Floyd alivyouawa. Ubinadamu bado upo duniani.
 
Derek Chauvin alikuwa akiwafundisha kazi askari wenzie alokuwa nao wakati wakimkabili George Floyd. Mmoja wa askari hao alikuwa ametoka chuo cha mafunzo ya uaskari Police Academy akiwa na masaa 48 tu.
 
Aliyekuwa Afisa wa Polisi Minneapolis Derek Chauvin amekutwa na hatia ya kumuua George Floyd mnamo Mei 2020 kwa kupiga goti shingoni mwa George alipokuwa akimkamata.

Kitendo alichofanya Derek kimesemwa kuwa ni kinyume cha Mafunzo ya Polisi na kidachodaiwa kusababishwa ubaguzi wa rangi. Kifo cha George kilisababisha maandamano makubwa ya #BlackLivesMatter huko Marekani.

======

A jury has reached a verdict in Derek Chauvin's trial over the death of George Floyd, finding the former Minneapolis police officer guilty on all counts.

Chauvin was charged with two counts of murder and one count of manslaughter in Floyd's death. The video of Floyd pleading for help as Chauvin knelt on him was seen around the world last year, igniting a wave of protests over police brutality.
 
Back
Top Bottom