Kesi ya mauaji ya Aneth Msuya: Shahidi asema mke wa Erasto alikiri kumuua wifi yake

Makafara ya utajiri na utafutaji Mali mwisho wake uwa mbaya sana..

Damu inamwagika mpaka kizazi cha tatu yote sababu ya mali.

Ni rahisi Ngamia kupenya katika tundu la Sindano , kuliko tajiri kuona ufalme wa mungu.
UFALME WA MBINGUNI UKO NDANI YA MWANADAMU WALAHI
TAFAKARI, acha uwoga!
 
By Hadija Jumanne na James
Magai, Mwananchi
Moja ya matukio yaliyovuta hisia
za wengi na kuendelea
kufuatiliwa kesi yake katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, ni mauaji ya Aneth Msuya,
dada wa aliyekuwa
mfanyabiashara maarufu na tajiri
wa madini mkoani Arusha, Erasto
Msuya, maarufu kama Bilionea
Msuya. Aliuawa Mei 25, 2016,
nyumbani kwake Kibada,
Kigamboni, Dar es Salaam. Mauaji
hayo yalitikisa kwa jinsi
alivyouawa kinyama.
Wanaotuhumiwa kuhusika nayo
walikamatwa na kufikishwa
Mahakama ya Kisutu
ilikofunguliwa kesi ili kukamilisha
hatua za awali na upelelezi
ambao sasa umekamilika.
Mauaji ya Aneth Msuya ni moja ya
matukio ya simanzi yaliyopata
kutikisa jijini Dar es Salaam
kutokana na namna alivyouawa
kinyama na mtiririko wa matukio
ya mashambulizi na mauaji katika
familia yao.
Aneth, ambaye ni dada wa
aliyekuwa mfanyabiashara
maarufu na tajiri wa madini
Mirerani mkoani Arusha, Erasto
Msuya ‘Bilionea Msuya’, aliuawa
Mei 25, 2016, nyumbani kwake
Kibada, Kigamboni jijini Dar es
Salaam.
Mwanamama huyo aliuawa
kinyama kwa kuchinjwa na mwili
wake kuachwa uchi ikiwa ni
miaka mitatu tangu kuuawa kwa
kaka yake, Bilionea Msuya.
Simulizi hii inatokana na maelezo
ya mashahidi wa upande wa
mashitaka katika kesi
inayowakabili washitakiwa wa
kesi ya mauaji hayo.
Maelezo hayo yalisomwa na
mawakili wa Serikali wakati jalada
la kesi hiyo lilipofungwa rasmi
katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu ilikofunguliwa ili
kukamilisha hatua za awali ikiwa
ni pamoja na upelelezi. Baada ya
hatua hizo kukamilika
itahamishiwa Mahakama Kuu
ambako ndiko itakakosikilizwa na
kutolewa uamuzi.
Maelezo hayo ya mashahidi wa
upande wa mashitaka yanawataja
watuhumiwa wa mauaji hayo,
sababu, mipango na namna
yalivyotekelezwa.
Aneth ni nani
Aneth Simon Msuya, ambaye jina
lake halisi alilopewa na wazazi
wake ni Anathe alizaliwa Aprili 3,
1986 katika Hospitali ya Machame
mkoani Kilimanjaro.
Baada ya kufikisha miaka sita
alianza elimu ya msingi katika
Shule ya Msingi Msaleni, iliyopo
mkoani Kilimanjaro ambako
alihitimu. Baadaye alijiunga Shule
ya Sekondari St Dorcas Seminary
iliyopo Moshi.
Katika mtihani wa kidato cha nne
alifanya vizuri kwa kupata daraja
la kwanza (division one) ya alama
nane (8). Kisha alijiunga na Shule
ya Sekondari Lutheran Junior
Seminary iliyopo Morogoro.
Katika mtihani wake wa kuhitimu
kidato cha sita, pia Aneth alifanya
vizuri kwani alipata daraja la
kwanza kwa alama nne (4).
Alijiunga masomo ya elimu ya juu
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) akichukua shahada ya
uchumi, ambapo alihitimu
shahada yake huku akifanya vema
na kuwa mwanafunzi bora wa
kwanza kwa kozi hiyo.
Kutokana na ufaulu wake huo
mzuri alifanikiwa kupata ufadhili
wa Wizara ya Fedha, ambayo
ilimsomesha Shahada ya Uzamili
ya Uchumi hapohapo UDSM na
baada ya kuhitimu shahada hiyo
aliajiriwa na Wizara ya Fedha.
Licha ya uwezo huo mkubwa wa
kiakili aliokuwa nao Aneth, baadhi
ya watu waliokuwa karibu naye
wanaeleza hakuwa mtu mwenye
kujivuna bali alikuwa mpole na
hakuwa mzungumzaji sana.
Aneth alifunga ndoa mwaka 2011,
na (Wilbard Kimario) na
wakafanikiwa kupata mtoto
mmoja wa kiume, lakini ndoa yao
haikudumu kwani mwaka 2012,
wawili hao waliachana.
Kwa mujibu wa watu waliokuwa
karibu na marehemu Aneth, tangu
wakati huo hadi mauti yanamfika,
hawakuwahi kumuona Aneth
akiwa na mwanaume wala kusikia
ana uhusiano na mwanaume
mwingine.
Kutokana na mauaji hayo, watu
wawili walikamatwa kwa tuhuma
za kuhusika nayo na hatimaye
kupandishwa kizimbani na
kusomewa shitaka moja la
kumuua Aneth.
Washitakiwa hao ni Miriam Mrita
(mshtakiwa wa kwanza), ambaye
ni mke wa marehemu Bilionea
Msuya, yaani wifi wa marehemu
Aneth pamoja na mfanyabiashara
Revocatus Muyella.
Kwa pamoja washitakiwa hao
wanadaiwa kumuua kwa
makusudi, Aneth Msuya kinyume
na kifungu cha 196 cha Kanuni za
Adhabu (Penal Code- PC)
wakidaiwa kutenda kosa hilo, Mei
25, 2016 nyumbani kwa
marehemu maeneo ya Kibada,
Kigamboni, Dar e Salaam.
Kesi hiyo namba 5 ya mwaka
2016 ilifunguliwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu kwa ajili ya kukamilisha
hatua za upelelezi kabla ya
kuhamishiwa Mahakama Kuu
ambayo ndiyo yenye mamlaka ya
kusikiliza kesi za mauaji.
Mahakamani hapo kesi hiyo
ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu
Mkazi Mkuu, Thomas Simba.
Waendesha mashtaka walikuwa
Wakili wa Serikali Mwandamizi
(SSA) Patrick Mwita na Wakili wa
Serikali (SA) Faraj Nguka na
washitakiwa wote wanatetewa
na Wakili Peter Kibatala.
Baada ya upelelezi kukamilika,
Novemba Mosi, 2018,
washitakiwa hao walisomewa
maelezo ya mashahidi
watakaoitwa kutoa ushahidi
upande wa mashitaka,
kuthibitisha shitaka dhidi ya
washtakiwa hao.
Hatua ya washitakiwa kusomewa
 
Dah! maskini watoto baba kauliwa, mama kafungwa kwa kumuu shangazi, watoto wanachukizwa na muuaji wa baba wanajikuta wametoka kwenye tumbo la muuaji, wanaenda kwa babu wanamkuta mtoto wa shangazi amabe ni marehemu kifo kimesababishwa na mama yao mama yao nae ni muuaji, aisee kuna familia zina pitia kipindi kigumu sna jamani.
Ndipo utajua kuwa inafaa tuishi kwa tahadhari sana hakika bila tahadhari hiyo ndio matokeo yake. Tuchukue hii shule aysee..
 
Maelezo ya mashahidi
Baada ya kumaliza kutaja idadi na
majina ya mashahidi pamoja na
vielelezo, mawakili hao wa
upande wa mashitaka walianza
kuwasomea washtakiwa maelezo
ya mashahidi wote
wanaotarajiwa kutoa ushahidi
katika kesi hiyo.
Mawakili hao waliwasomea
washtakiwa maelezo ya
mashahidi hatua kwa hatua, kwa
kupokezana kila baada ya kusoma
maelezo ya mashahidi kadhaa,
kazi ambayo ilitumia takribani saa
tano, kuanzia saa 5.15 asubuhi
mpaka saa 9.55 alasiri, Alhamisi
iliyopita
Pamoja na mambo mengine
yaliyomo katika maelezo ya
mashahidi hao, mawakili hao
walidai mshitakiwa wa kwanza,
Miriam alikiri kuhusika katika
mauaji hayo na kueleza sababu na
mpango wa namna
walivyotekeleza mauaji
Mipango ya mauaji
Wakili Mwita alidai washtakiwa
katika kutekeleza mauaji hayo
walimtafuta mfanyakazi wa ndani
wa Aneth.
Alidai Mei 5, 2016 , Miriam na
mwenzake walienda Kibada
alikokuwa akiishi Aneth na
kwamba kabla ya kufika katika
nyumba ya Aneth, alikutana na
mfanyakazi huyo wa ndani wa
Aneth, aitwaye Getrude Mafuru
ambaye alikuwa anaenda dukani
kununua karatasi za chooni (toilet
paper).
Wakili Mwita alidai mshtakiwa
Miriam alishusha kioo cha gari la
kifahari lenye rangi ya bluu
alimokuwamo na kumuita
Getrude ambaye aliitikia wito na
akamuuliza mahali Aneth
alikokuwa akiishi. Alidai kuwa
Getrude alimueleza kuwa Aneth
anakaa nyumba iliyokuwa
inafuata, kutoka walikokuwa
wamesimama na kisha Miriam
alimuahidi msichana huyo kuwa
angepita kesho, kisha alipandisha
kioo cha gari yake na kuondoka.
Siku iliyofuata, Wakili Mwita alidai
Miriam alienda tena hadi karibu
na nyumba aliyokuwa akiishi
Aneth, ambapo alimuona Getrude
akichota maji nyumba ya jirani na
akamuita na msichana huyo
alipomfikia, Miriam alimtaka
apande katika gari hilo. Kwa
mujibu wa maelezo hayo, Wakili
Mwita alidai msichana huyo
aliingia ndani ya gari hilo na
Miriam akampatia simu ndogo
yenye rangi nyeusi.
Mwita alidai kuwa wakati Getrude
anapewa simu na Miriam,
mshitakiwa wa pili yeye alikuwa
amekaa nyuma huku akiwa
amemuwekea Getrude bastola
begani na kwamba Miriam
alimwambia msichana huyo
asimwangalie Muyella bali
amwangalie yeye.
Wakili Mwita alidai Miriam
alimweleza Getrude kuwa simu
hiyo ni ya mawasiliano baina yao
wawili huku akimweleza sio kwa
ajili ya kumpigia mtu mwingine
yeyote.
Alidai Getrude ambaye alikuwa
analipwa mshahara wa Sh 60,000
alieleza kuwa sura ya Miriam
alishawahi kuiona Moshi, kwa bibi
yake yaani kwa mama yake
marehemu Aneth, alikokuwa
kabla ya kwenda kwa Aneth, na
kwamba Miriam alikwenda
nyumbani hapo na mumewe
Erasto Msuya enzi za uhai wake.
Wakili Mwita aliendelea kudai
kuwa Mei 23, 2016 saa tisa
mchana, Miriam alimpigia Getrude
na kumwambia anataka kuonana
naye, huku akimwelekeza mahali
alikokuwa.
Alidai kuwa Getrude alikwenda
hadi mahali lilipokuwa
limeegeshwa gari la washitakiwa
hao, karibu na nyumba ya Aneth
na kisha binti huyo aliingia katika
gari hilo.
Wakili Mwita alidai Getrude akiwa
ndani ya gari hilo aliiona pochi ya
Miriam ikiwa imejaa hela zikiwa
zimefungwa na mpira
mwembamba, na Miriam akampa
Sh 20,000.
Alidai baada ya kumpa fedha hizo,
Miriam alimsisitiza Getrude
aondoke nyumbani kwa Aneth
kabla ya Mei 25, 2016 na kwamba
simu hiyo aliyompa aitupe
sehemu ambayo mtu mwingine
hawezi kuiona.
Wakili Mwita alidai Mei 25, 2016
Getrude aliondoka nyumbani kwa
Aneth na ufunguo wa geti
aliupeleka kwa jirani yao, kisha
akampigia simu Aneth kuwa
ufunguo wa ndani upo chini ya
kapeti la kufutia vumbi lililopo
mlangoni na kwamba ufunguo wa
getini upo kwa jirani yao.
Alidai Getrude aliondoka na
kwenda Chanika kwa mchumba
wake aitwaye Sabri Kombo, na
kwamba wakati akiwa kwenye
pantoni, aliitupa simu hiyo
baharini na alipofika kwa mpenzi
wake alimwelezea mambo
aliyoambiwa na Miriam. Akiwa
Chanika, Wakili Mwita alidai kuwa
Getrude alipigiwa simu na bibi
yake, yaani mama wa Aneth na
kumweleza kuwa Aneth ameuawa
kwa kukatwa koromeo.
Kwa upande wake Wakili Nguka
alidai baada ya tukio, hilo timu ya
askari wa upelelezi wakiongozwa
na Mkuu wa Upelelezi Kinondoni,
Mrakibu wa Polisi (SP) Richard
Mwaisamba ilifika eneo la tukio na
kukuta mlango wa nje ukiwa
haujafungwa.
Alidai timu hiyo ilikuta mlango wa
chumbani ukiwa umevunjwa kwa
kutumia tofali na kwamba chini
ya mlango kulikuwa na vumbi la
matofali. Ndani ya chumba cha
Aneth, Wakili Nguka alidai kuwa
wapelelezi hao walikuta mwili wa
Aneth ukiwa umekatwa koromeo
ukiwa sakafuni, huku ukiwa uchi
wa mnyama na mdomoni alikuwa
amewekewa kitambaa.
Alidai pembeni mwa mwili wa
Aneth, wapelelezi hao walikuta
nguo ya ndani yenye rangi ya
zambarau, kisu chenye damu na
filimbi iliyokuwa karibu na
kitanda. Kwenye kabati lililokutwa
wazi walikuta hereni, cheni za
dhahabu na simu.
Mshitakiwa adaiwa kukiri
Wakili Mwita alidai kuwa
wakaguzi wa Polisi, Latifa
Mohamed, ASP Jumanne
Malangehe na Koplo Mwaka
walienda Arusha kwa ajili ya
kufanya mahojiano na upekuzi
nyumbani kwa mshitakiwa
Miriam.
Alidai Agosti 7, 2016 akihojiwa na
wakaguzi hao, mshitakiwa huyo
alikiri kuhusika kupanga mpango
wa mauaji na aliwaelekeza
maeneo walikokuwa wanapangia
mpango huo. Alidai mbali na
kukiri kosa hilo mbele ya askari
hao ambao waliandika maelezo
yake, pia mshitakiwa alikiri
kutenda kosa hilo mbele ya Mlinzi
wa Amani (Hakimu wa Mahakama
ya Mwanzo). Alidai wakaguzi hao
wa polisi walirudi Dar es Salaam
na Miriam, wakiongozana na
wachunguzi wa picha za kawaida
na za video kutoka makao makuu
ya polisi na Miriam aliwapeleka
sehemu ambayo walikuwa
wanakutana na Getrude kwa ajili
ya kufanikisha mauaji hayo.
Wakili Mwita alidai katika
maelezo hayo ambayo
mshitakiwa wa kwanza aliyatoa
kwa askari na mbele ya Mlinzi wa
Amani, alieleza kuwa aliamua
kutenda kosa hilo kutokana na
mgogoro wa mali za mumewe
yaani Bilionea Msuya.
Pia, walidai kuwa mshtakiwa
huyo aliamua kutenda kosa hilo
kwa hasira kutokana na Aneth
kumtumia picha za kukashfu
umbile lake. Wakili Mwita alidai
mshitakiwa alieleza kuwa Aneth
alikuwa akimtumia picha za
wanawake wenye maumbile
makubwa mabaya, wenye
matumbo makubwa, jambo
ambalo lilimfanya apate hasira.
Alidai kwa mujibu wa maelezo
yake, mshitakiwa Miriam baada ya
kuchukizwa na kitendo cha wifi
yake kumtumia picha hizo
alizoziona kama za kumkashfu,
aliamua kutafuta ushauri kwa
mshitakiwa wa pili Muyella,
ambaye alimshauri kuwa huyo
dawa yake ni kumuua tu.
Wakili Mwita alidai baada ya
ushauri huo wa mshitakiwa wa
pili walikubaliana mshtakiwa wa
kwanza amlipe mshitakiwa wa
pili Sh20 milioni kwa ajili ya kazi
hiyo.
Alidai washitakiwa hao baada ya
makubaliano hayo ndipo
walipopanga na kutekeleza
mauaji hayo, na kwamba
mshtakiwa wa kwanza alimlipa
mshtakiwa wa pili Sh10 milioni
kwanza wakiwa jijini Dar es
Salaam na baada ya kutekeleza
mauaji hayo, alimmalizia Sh10
milioni jijini Arusha.
Soma zaidi: Jalada la Mke wa
Bilionea Msuya latua kwa DPP
Wakili Mwita aliieleza mahakama
kuwa mshitakiwa wa pili baada
ya kukamatwa na kuhojiwa
alikubali kumfahamu mshitakiwa
wa kwanza kuwa ni
mfanyabiashara mwenzake na
alikuwa akifahamiana na
marehemu mumewe, lakini
alikana kuhusika na mauaji hayo.
Soma zaidi: Upelelezi kesi ya mke
wa Bilionea Msuya wakamilika
Licha ya kukana kuhusika katika
mauaji hayo, Wakili Mwita
aliieleza mahakama kuwa
mshitakiwa huyo alitambuliwa na
shahidi mmoja (ambaye ni shahidi
muhimu kwenye kesi hiyo)
kwenye gwaride la utambuzi. Kwa
upande wake Wakili Nguka alidai
Agosti 4, 2016 timu ya upelelezi
kutoka Dar es Salama ilisafiri hadi
Arusha kwa ajili ya kumkamata
Miriam na walimkamata.
Wakili Nguka alidai Miriam
alikamatwa akiwa katika klabu ya
Tembo iliyopo Arusha kisha askari
hao waliongozana na mshitakiwa
huyo hadi nyumbani kwa
mshtakiwa na kuanza upekuzi.
Alidai katika upekuzi huo ulioanza
saa saba mchana hadi saa 10 jioni,
timu hiyo ya upekuzi ilichukua
suti mbili ikiwemo ya rangi ya
bluu na nyekundu, cheni za
dhahabu na viatu jozi mbili.
Alidai Miriam alikiri kuhusika
katika mauaji ya wifi yake
kutokana na mgogoro wa
kifamilia. Hata hivyo, kwa mujibu
wa maelezo ya mashahidi hao,
Miriam alipendekezwa na familia
ya mumewe, Bilionea Msuya, na
akateuliwa na mahakama kuwa
msimamizi wa mirathi ya
mumewe. Baadaye mshitakiwa
huyo alilalamikiwa na ndugu wa
marehemu kwa ufujaji wa mali na
kwamba kutokana na kushindwa
kuwasilisha mahakamani
mrejesho wa usimamizi na
mgawanyo wa mali hizo,
mahakama iliamua kumuondoa
katika usimamizi wa mirathi hiyo.
Kutokana na hali hiyo, mshtakiwa
huyo aliomba ushauri wa
mfanyabaishara aitwaye Muyella
kuhusiana na mgogoro huo na
kumueleza kuwa Aneth amekuwa
akimuingilia katika mirathi na
mali alizoachiwa na mume wake.
Kwa mujibu wa maelezo ya
mashahidi hao, baada ya
mahakama kumuondoa katika
usimamizi wa mirathi, kikao cha
familia kilimpendekeza dada
mwingine wa marehemu Msuya
pamoja na baba wa marehemu
kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo
lakini mshtakiwa Miriam aliweka
pingamizi.
 
In every murder, there is a motive, and money is among the motives.
Who is the beneficiary?
 
Back
Top Bottom