Kesi ya Masheikh wa Uamsho yaahirishwa baada ya Jamhuri kuomba udhuru tena

Sep 19, 2019
43
383
Bismillahir Rahmaanir Rahiim

SHURA YA MAIMAMU TANZANIA

KESI YA MASHEIKH LEO TAREHE 26.05.2021, IMEAKHIRISHWA BAADA YA UPANDE WA JAMUHURI KUOMBA UDHURU TENA

Shauri la Masheikh lililopangwa kuendelea kusikilizwa leo limeakhirishwa baada ya upande wa Jamhuri kuomba kupewa muda kwa sababu ya kutokukamilisha baadhi ya mambo ya kisheria.

Tarehe 20. 05. 2021, Mahakama Kuu iliakhirisha shauri hilo baada ya upande wa Jamhuri kuomba muda ili DPP mpya aweze kushiriki katika shauri hilo kwa ajili ya kuongeza nguvu katika jopo lao.

Mahakama Kuu kwa mara nyingine imekubali ombi la Mawakili wa Jamuhuri hivyo imeakhirisha shauri hilo na kupanga kusikilizwa tena Juma tatu tarehe 31.05.2021

Kwa upande mwingine jopo la Mawakili wa Utetezi lilikua tayari kuendelea na shauri hilo.

Shura ya Maimamu Tanzania inawaomba watanzania kufatilia mwenendo wa mashauri haya kwa karibu.

Ibrahimu Zuberi Mkondo.
Msemaji wa Shura ya Maimamu Tz
0713118812
 
Kila siku wao wenyewe hunena kuwa haki iliyo cheleweshwa ni sawa na haki iliyo nyimwa.

Bunnge letu Tukufu lina wajibu wa kubadilisha sheria zote zinazo kandamiza uhuru na haki za watuhumiwa.
 
Hawa mashekh wana kesi ya kujibu na ni nzito sana upande wao. Kila anayepita atawaacha umo humo segerea vinginevyo vyombo husika viamue tu kuwasemehe "makusudikally".
 
Hawa mashekh wana kesi ya kujibu na ni nzito sana upande wao. Kila anayepita atawaacha umo humo segerea vinginevyo vyombo husika viamue tu kuwasemehe "makusudikally".
Mbona washaomba msamaha na hawatarudia tena kwa upuuzi waliotaka kuufanya
 
Hawa mashekh wana kesi ya kujibu na ni nzito sana upande wao. Kila anayepita atawaacha umo humo segerea vinginevyo vyombo husika viamue tu kuwasemehe "makusudikally".
Mwaka watisa huu mbona hamjaona Hilo kosa WACHENI UKOLONI HUO wewe angelikua baba yako kateseka hivyo ungesema hayo WACHENI USHENZI WAZANZIBAR NA BINADAMU PIA KM NYINYI
 
WANAZANI NCHI HII YA KUFANYA UHALIFU ILA WAMESHIKA ADABU
Mama yako jee hajashika adabu issue ya Muungano bado nztitoo usolijua mkoloni mweusi wewe litakusumbuwa eti wwmeshika adabu jinga mojaw
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom