Kesi ya Makonda, Le Mutuz kupora Range Rover yapigwa kalenda

SemperFI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
1,018
2,151
1669215361165.png

Kesi ya tuhuma za uporaji wa gari aina ya Range Rover, inayomkabili aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda na mmiliki wa blogu ya Lemutuz, William Malecela imepangwa kutajwa Desemba 8, 2022.

Ni baada ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate kuwa kwenye majukumu mengine ya kikazi.

Shauri hilo limefunguliwa na mfanyabiashara, Patric Kamwelwe akidai alipwe fidia ya zaidi ya Sh 240 miliini ambazo ni gharama za kodi thamani ya gari hilo la kifahali.

Wakili Wabeya Kung'e anayemwakilisha Kamwelwe alidai mbele ya hakimu alidai shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mkuu, Mery Mrio amesema hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate anayesikiliza shauri hilo yupo kwenye majukumu mengine ya kikazi hivyo ameahirisha shauri hilo hadi Disemba 8,2022 kwa ajili ya kutajwa.

Kwa upande wa Makonda, akiwakilishwa na Wakili Simon Mbawala huku Limutuz akiwakilishwa na wakili Ruben Simwanza.

Katika hati ya madai ya mfanyabishara huyo anadai yeye na Lemutuz ni marafiki alitumia urafiki wake kumkabidhi Makonda gari aina ya Range Rover

Mfanyabiashara huyo alimkabidhi gari hilo Lemutuz ili ampatie Makonda aweze kutumia wakati akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa makubaliano alitumie kwa wiki mbili na kisha amrudishie.

Lakini imekuwa tofauti na makubaliano hayo ambapo Makonda ameendelea kulitumia gari hilo mpaka Leo hii hajamrudishia.

MWANANCHI
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
3,520
5,230
Mahakamani sasa wanakwenda kutafuta nini? Kwani wakati wa makabidhiano Mahakama ilihusishwa? Wawe wakweli tu kwamba Makonda kwa sasa hana Madaraka tena hivyo na urafiki wao umekoma rasmi.
 

fogoh2

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
4,223
3,866
Mahakamani sasa wanakwenda kutafuta nini? Kwani wakati wa makabidhiano Mahakama ilihusishwa? Wawe wakweli tu kwamba Makonda kwa sasa hana Madaraka tena hivyo na urafiki wao umekoma rasmi.
Kwani ishu zote zinazoamuliwa mahakamani ,mahakama ilihusishwa kabla
 
1 Reactions
Reply
Top Bottom