Kesi ya makame na kiravu kwa hilafu na wakichakachua chaguo la taifa!


Not_Yet_Uhuru

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
1,305
Likes
8
Points
0
Not_Yet_Uhuru

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2010
1,305 8 0
MAKAME, KIRAVU WASHTAKIWE HARAKA! :A S-danger:

Watanzani nchi nzima wanasubiria Matokeo ya Kura zao walizopiga kumchagua Rais, Wabunge na Madiwani wao. Cha kushangaza matokeo mengi yanatangazwa toka katika vyanzo tofauti lakini Tume ya Kiravu na Makame wanakalia Haki za Wananchi. Hivi hawa wana nini? Na wanajua Uhai wa Watanzania una gharama gani?

Mambo yafuatayo yanafanya Tume ikose credibility(Hadhi) ya kuwatangazia wananchi Ukweli na kuna wasiwasi kuwa wanasaidiana na walioshindwa ili kuharibu Haki na Ushindi wa Watanzania wengi. Hali hii ni Hatari sana.

* Kwanini Tume imekataa matokeo yasitangazwe Maeneo husika? Wanafanya uchakachuaji!
* Kwanini Tume inachelewesha Makusudi Matokeo, hata yale ambayo yameshatangazwa wazi na vyombo vingi?
* Dosari zote zilizotokea ni ushahidi wa uzembe na uvunjifu wa Haki za wananchi maana watu wengi wamekosa kupiga kura wakati Kiravu alisema uongo kuwa kila kitu kipo sawa, uhakiki na vifaa vilipangwa ipasavyo.
* Kusababisha Hasara kwa Taifa kwa Kura za Marudio jambo ambalo halikustahili kuwepo.
* Kuruhusu uvurugaji wa Makusudi wa Kura mfano wananchi kukutwa na Masanduku ya Kura zilizopigwa Tayari (Dodoma)
* Ucheleweshwaji unajenga chuki na hisia za hasira kwa wananchi ambao walipiga kura zao kwa amani, utulivu na kuondoka vituoni kwa utiifu, ila Tume inawatendea uharibifu.

Wanasheria makini wachukue hili kama dokezo ktk kulinda haki na ustawi, amani na utulivu wa Taifa. HAKI INAANGAMIZWA NA WATU HAWA. HII NI HATARI SANA!

:sad::sad::sad::sad:
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,401
Likes
487
Points
180
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,401 487 180
Tundu lissu ataanza nalo ilo
 

Forum statistics

Threads 1,250,688
Members 481,436
Posts 29,741,829