Kesi ya Liyumba: Wadau mnasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya Liyumba: Wadau mnasemaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Masanyiwa, Oct 23, 2009.

 1. M

  Masanyiwa Member

  #1
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau siielewi vizuri hii kesi ya Liyumba ni njisi gani hakimu aliweza kutoa maamuzi

  Cheo chake naona kwa maamuzi kama yale ni kama haiwezekani
   
 2. M

  Mwanaume Senior Member

  #2
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 11, 2009
  Messages: 122
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  may be through delegated authority
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Jukwaa la Sheria kweli limevamiwa! Sasa hapa unazungumzia hakimu yupi mwenye cheo kipi kwenye kesi ya Liyumba na alitoa maamuzi yapi? Kaazi kweli kweli!
   
 4. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Unjust country,and still big fish are still on the street!
  Poor Liyumba,i guess a low profile fisadi!

  The whole of Mkapa government should be charged!
  DPP is a joke
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Taratibu mkubwa.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Vera we ni lawyer
   
 7. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hii kesi ya Liyumba bado haileweki, kama kula wala hakula peke yake. Nadhani kuna kuna kitu kingine nyuma ya panzia.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Wanawake wanampenda kweli liyumba,ona mnavyomtetea....ha ha ha..
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Oct 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kwanini unauliza bwana Mkubwa?
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  just curious........
   
 11. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #11
  Oct 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Curiosity killed the cat remember?
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  i am one tough cat.nna roho tisa.....
   
 13. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  haya Boss
   
 14. C

  Charuka Member

  #14
  Oct 25, 2009
  Joined: Oct 20, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yafuatayo ni mahojiano kati ya mawakili wa utetezi; Majura Magafu, Hillary Mkate, Onesmo Kyauke na Hudson Ndusyepo dhidi ya shahidi
  Wakili: Ndugu shahidi uliwahi kuchunguza ramani ya majengo?
  Shahidi: Nilipata fursa ya kuchunguza ramani.
  Wakili: Nani alileta mabadiliko ya upanuzi wa Minara Pacha?
  Shahidi: Liyumba.
  Wakili: Liyumba siyo injinia, aliwezaje kufanya hayo mabadiliko wakati yeye alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala?
  Shahidi: (Kimya) Uchunguzi unaonyesha Liyumba alikuwa akitoa maagizo ya kuidhinisha ongezeko la ujenzi.
  Wakili: Je, ukiambiwa ongezeko hilo liliidhinishwa na bodi utakubali?
  Shahidi: Watakuja wajumbe wa bodi wenyewe waeleze na katika uchunguzi wangu sikubaini hili.
  Wakili: Tukikuambia kulikuwa na idhini ya bodi utakubali?
  Shahidi: Katika uchunguzi wangu, Aproval ya bodi inayozungumzwa hapa ni ile Approval baada ya Liyumba kufanya mabadiliko ya upanuzi wa ujenzi.
  Wakili: Huo mkataba wa ujenzi ulikuwa ni kati ya Liyumba na kampuni ya ujenzi?
  Shahidi: Hapana, ulikuwa ni kati ya BoT na Kampuni ya Lead Consultant. Lakini baadaye Kurugenzi ya Utumishi na Utawala iliyokuwa ikiongozwa na Liyumba ndiyo ilikuwa ikiratibu mradi huo (Cordinator).
  Wakili: Huyo Liyumba alikuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala ndiyo apewe mzigo wa kushughulikia ujenzi wa mradi huo, je inaingia akilini?
  Shahidi: (Kimya) Nimesema ofisi ya Liyumba ilikuwa inaratibu na ilikuwa kiungo.
  Wakili: Mshitakiwa kwa cheo chake ndiye aliyeidhinisha mabadiliko hayo wakati yeye siyo mhandisi?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Wewe ni mhandisi wa ujenzi hilo swali siyo la kufikiria… jibu hilo swali upesi.
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Mabadiliko yote hayo yanatakiwa yaidhinishwe na bodi?
  Shahidi: Ndiyo.
  Wakili: Kwa hiyo mabadiliko yote hayo hayakuidhinishwa na bodi ya BoT?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Je, Gavana marehemu Daud Balali hakuusika na mabadiliko hayo?
  Shahidi: Gavana hakuhusika kabisa.
  Wakili: Mbona upande wa mashitaka wakati unamsomea maelezo ya awali mshitakiwa hivi karibuni, ulidai kuwa ni Liyumba na Ballali ndiyo walifanya mabadiliko hayo bila idhini ya bodi ya wakuregenzi?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Ulisema Liyumba alikuwa akiandika barua za maagizo ya mabadiliko hayo ya upanuzi wa ujenzi kama mtu binafsi au mtumishi wa BoT?
  Shahidi: Mahakama itajua.
  Wakili: Ballali alikuwa Gavana na kwa mujibu wa sheria ya benki, ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi, sasa unasemaje mabadiliko alifanya Liyumba bila idhini ya Bodi?
  Shahidi: Kwa sababu Ballali ameishakufa, siwezi kumzungumzia hapa.
  Wakili: Hapa, jibu swali kwani wakati Ballali alipokuwa hai, ndiye alikuwa na madaraka yote na maagizo aliyokuwa akiyatoa Liyumba angeweza kuyakataa?
  Shahidi: Mshitakiwa asingeweza kuyakataa.
  Wakili: Kwa sababu angeyakataa angeonekana ni mtovu wa nidhamu na hivyo basi Liyumba alikuwa ni mtiifu na alikuwa katika ofisi hiyo ya umma?
  Shahidi: Ndiyo.
  Wakili: Katika uchunguzi wako ulibaini mshitakiwa kafanya kosa la rushwa?
  Shahidi: Nimebaini kafanya kosa linaloendana na rushwa.
  Wakili: Kwa hiyo unataka kuiambia mahakama hata bodi ya BoT ilikumbwa na rushwa?
  Shahidi: Sina jibu.
  Wakili: Shitaka linalomkabili mshitakiwa ni kuisababishia serikali hasara kwa sababu aliongeza upanuzi wa majengo, hivi Liyumba hayo majengo aliyachukua na kuyapeleka nyumbani kwake?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Hivi upanuzi wa ujenzi wa minara pacha ulitokea usiku wa manane, au uliota kama uyoga?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Hivi bodi ilikuwa haina akili hadi isikataze hayo mabadiliko ya upanuzi wa ujenzi unayodai yalifanywa na Liyumba?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Katika uchunguzi wako, Liyumba alikuwa ni mjumbe wa bodi?
  Shahidi: Hapana.
  Wakili: Tunakubalina kwamba yale majengo ya ghorofa 18 yapo na je, yana thamani nzuri?
  Shahidi: Yapo
  Wakili: Thamani ya majengo yale imeteremka?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Ebu iambie mahakama sasa, serikali inapata hasara ipi?
  Shahidi: Kwa kuwa hakukuwa na idhini ya bodi, ndiyo hasara yenyewe na wajumbe wa bodi watakuja kueleza (kicheko).
  Shahidi: Liyumba alikuwa ni mtu mdogo kwenye bodi na mabadiliko hayo angefanya bila idhini si bodi ingemtimua kazi?
  Shahidi: Ndiyo.
  Wakili: Utakubaliana na mimi wewe huwezi kuwa mchunguzi?
  Shahidi: Sikubaliani na wewe, mimi ni mchunguzi.
  Wakili: Unajua kazi za Takukuru zilizoainishwa kwenye Sheria ya Takukuru kifungu cha 7?
  Shahidi: Ndiyo.
  Wakili: Utakubaliana kimsingi kazi ya taasisi yenu ni kuchunguza kesi zinazohusiana na rushwa na si vinginevyo?
  Shahidi: Ndiyo.
  Wakili: Kwa hiyo utakubaliana na mimi makosa yanayomkabili mteja wangu hayahusiani na rushwa na ndiyo maana yanaangukia kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Kwa hiyo kazi hii ya uchunguzi katika kesi hii haikupaswa kufanywa na Takukuru ilipaswa kufanywa na jeshi la Polisi?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Ni nani mwenye mamlaka ya mwisho ya kuamua nini kifanyike na kipi kisifanyike BoT?
  Shahidi: Bodi ya BoT.
  Wakili: Uliwahi kuwahoji wajumbe wa bodi kwanini waliidhinisha mabadiliko ya upanuzi wakati mabadiliko hayo yalishatekelezwa?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Uliwauliza wajumbe hao ni kwanini wasikatae mabadiliko hayo kwa sababu wao walikuwa pale kwa ajili ya kulinda maslahi ya benki hiyo na serikali?
  Shahidi: Walisema walikataa bila mafanikio.
  Wakili: Uliwahi kuzisoma hizo minute za vikao vya bodi ilikuona?
  Shahidi: Ndiyo.
  Wakili: Kwanini hukuzileta hapa mahakamani?
  Shahidi: Zitaletwa na mchunguzi mwenzangu.
  Wakili: Uliwahi kuusoma mkataba wote wa ujenzi wa mradi huo?
  Shahidi: Ndiyo.
  Wakili: Kwenye huo mkataba kuna kipengele kinaruhusu kampuni ya ukandarasi wa mradi na BoT kufanya marekebisho kutokana na thamani ya shilingi kushuka?
  Shahidi: Ndiyo.
  Wakili: Timu yenu ya uchunguzi iliwahi kumhoji Ballali?
  Shahidi: Haikuwahi kumhoji ila nilimhoji Liyumba.
  Wakili: Ulivyomhoji Liyumba ulimuuliza hizo barua za marekebisho ya mkataba ya kupanua ujenzi wa majengo aliandika kwa maelekezo ya nani?
  Shahidi: Sikumbuki.
  Wakili: Ulimuuliza Liyumba ni kwanini Bodi ya BoT ilikubali ongezeko la ghorofa nne, nne badala ya 14 zilizoainishwa kwenye mkataba?
  Shahidi: Ndiyo na alinijibu ilikubali kwa sababu kulikuwa na ongezeko kubwa la wafanyakazi BoT kwa hiyo kulikuwa na uhaba wa ofisi.
  Wakili: Bodi ilikubali kuidhinisha baada ya kuridhika kwamba yale marekebisho ya upanuzi yalikuwa ni ya msingi na yasingeweza kuisababishia serikali hasara?
  Shahidi: Hapa.
  Wakili: Kama hapana, bodi nayo ilifanya makosa kuidhinisha marekebisho huku ikijua itaingiza serikali hasara?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Bodi ilikuambia hiyo na haikuwa na haja ya kukataa?
  Shahidi: Bodi haikukataa, ila wajumbe wa bodi walikemea.
  Wakili: Hayo mahesabu ya mteja wetu kusababishia hasara ya kiasi hicho cha fedha haliyafanya nani?
  Shahidi: Mimi
  Wakili: Haya tupe huo mchanganuo wa mahesabu uliyoyafanya hadi ukapata hiyo hasara?
  Shahidi: Sina.
  Wakili: Katika hayo maagizo ya upanuzi wa ujenzi yaliyokuwa yakitolewa na Liyumba yalikuwa yakitaja kiasi chochote cha fedha?
  Shahidi: Hapana.
  Wakili: Hicho kiasi cha gharama umekipata wapi wakati hujui hata vifaa vya ujenzi hujui vilinunuliwa kiasi gani?
  Shahidi: Kimya.
  Wakili: Nani alikuwa na jukumu la kutunza miniti za vikaa vya bodi licha uliieleza mahakama miniti nyingine hukuzipata na baadhi ulizozipata hazina saini?
  Shahidi: Katibu ambaye ni Mwanasheria wa BoT, Bosco Kimela.
  Wakili: Hivi miniti zisizokuwa na saini ya Mwenyekiti na Katibu ninakuwa miniti kweli?
  Shahidi: Miniti ili ziwe miniti ni lazima ziwe na saini ya watu hao.
  Kesi hiyo inayovuta hisia za wengi nchini imeahirishwa hadi leo ambapo shahidi wa pili ataanza kutoa ushahidi wake.
  Ifuatayo ni mahojiano kati ya jopo la Mahakimu wakazi na shahidi huyo?
  Jopo:Majengo yamejengwa hayajajengwa?Liyumba alifaidika binafsi na mabadiliko ya upanuzi wa ujenzi huo?Je kulikuwa na udanganyifu katika kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi huo?Sasa hasara inapatikanaje?
  Shahidi:Kimya(watu wakaangua kicheko).
  Awali kabla ya shahidi huyo kuhojiwa na upande wa utetezi, wakili wa serikali Juma Mzarau, Ben Lincoln,Thadeo Mwenepazi na Prospa Mwangamila,alimuongoza shahidi huo kutoa ushahidi wake:Yafuatayo ni mahojiano kati ya Mzarau na shahidi huyo:
  Wakili:Je lini ulikabidhiwa jukumu la kuchunguza shauri hili?
  Shahidi:Februali 2008.
  Wakili:Baada ya kukabidhiwa jukumu hilo uligundua nini?
  Shahidi:Niligundua shauri lilipokelewa April 2006 ofisi kwetu Takukuru.
  Wakili:Baada ya kukabidhiwa shauri hilo ulifanya nini?
  Shahidi:Kufanya uchunguzi wa wazi kwa kukusanya vielelezo na kukusanya vielelezo na kuhoji mashahidi pamoja na Liyumba na kutembelea mradi wa minara pacha na nilibaini Bot ilisaini mkataba na kampuni ya Group Five East(PTY) Ltd ya Afrika Kusini.
  Wakili:Ulishawahi kuona mkataba huo?
  Shahidi:Ndiyo naniaomba kuotoa mahakama kama kielezo(jopo limepokea kama kielezo Na.moja).
  Wakili:Kwa mujibu wa mkataba huo gharama za ujenzi zilikuwa kiasi gani?
  Shahidi:USD milioni 73.6
  Wakili:Unakumbuka gharama za kazi zilizoainishwa kwenye mkataba huo?
  Shahidi:Ni za ujenzi wa jengo la South Tower ghoroga 14,North Tower ghorofa 14,ukumbi wa mikutano,sehemu ya kuegesha magari ghorofa nne na kazi za nje.
  Wakili:Je katika uchunguzi wako uliwahi kutembeleza ujenzi wa mradi wa Minara Pacha?
  Shahidi:Ndiyo na niligundua jengo la South Tower,Noth zilijengwa ghorofa 18 badala ya 14 zilizoainishwa kwenye mkataba, vile vile kwenye ninara hiyo majengo hayo vilijengwa viwanja vya kutua Helkopta na kwenye kuta za majengo hayo kuliwekwa(glass curtain)badala ya rangi ya kawaida ambayo iliainishwa kwenye mkataba.
  Wakili; Je kulikuwa na jengo lilojengwa nje ya mkataba?
  Shahidi:Ndiyo.jengo la North block lilijengwa nje ya mkataba.
  ,Basement mbili badala ya basement moja.
  Wakili:Nani alikuwa Meneja mradi wa Minara Pacha?
  Shahidi:Deogratius Kweka.
  Wakili:Kielelezo gani kingine unakumbuka ulikipata kwenye uchunguzi wako?
  Shahidi:Cost Alasisy report toka 2002-2008 na ninaomba niitoe mahakamani kama kielelezo.
  Ghafla aliinuka wakili wa utetezi Majura Magafu na kuiomba mahakama isipokea kielelezo hicho kwani kinaonyesha wazi kiliandaliwa kwani mbaya na hakikuandaliwa kitalaamu kwani ina saini,jina la mwandishi wala mhuri wa kampuni, tarehe na kwa kifupi hiko kielelezo ni cha kuokoteza barabarani na wala haijaandikwa na shahidi huyo.

  “Tunapinga kupokelewa kwa kielezo hicho kwani ni cha kuokoteza barabarani na wala hakikuandikwa na shahidi huyu tunataka aliyoandika hiyo ripoti afike hapa tumuulize maswali ..shahidi huyu atakuwa bubu tukianza kumuuliza maswali na sisi atutaki awe bubu”alidai Magafu kwa sauti ya ukali .

  Hata hivyo baada ya wakili Magafu kupinga kilelezo hicho kisipokelee wakili wa serikali Mzarau aliinuka na kudai hawataki kupoteza muda wa mahakama na hivyo upande wa mashitaka wanakiondoa kielelezo hicho na kisipokelewe na mahakama na kusababisha watu kuangua vicheko.

  Kiongozi wa Jopo Mkasimongwa,aliarisha kesi hiyo hadi leo ambapo shahidi wa pili ataanza kutoa ushahidi wake katika kesi hiyo ambayo umati wa wananchi wengi wanafika mahakamani hapo kwaajili ya kusikiliza kesi hiyo.

  Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Oktoba 23, 2009
   
 15. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #15
  Oct 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  "Yafuatayo ni mahojiano kati ya mawakili wa utetezi; Majura Magafu, Hillary Mkate, Onesmo Kyauke na Hudson Ndusyepo dhidi ya shahidi"

  Now you are talking!
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Oct 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mwelekeo wa mwanzo wa kesi upepo ni mbaya kwa upende wa mashtaka! Kama majengo yalishajengwa, ghorofa 18 badala ya 14 na value for money iko ok, then hasara ni nini kwa Serikali? Labda kama majengo menyewe yangekuwa hayapo! Hapa kazi ipo!
   
 17. N

  Nyani New Member

  #17
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Dear All,

  Kutokana na shahidi Tongola kuieleza mahakama kuhusiana na Maamuzi ya upanuzi wa machengo pacha......kwakweli Amatus J Liyumba wanamwonea bure.....Kama Board of Directors haijawahi kulalamika hata siku mmoja kuhusiana na upanuzi wa majengo au utendaji wa Liyumba.....huo ni ubabaishaji wa Mahakama hivyo anastaili kuachiwa uhuru....maana amefanya kazi kwaniaba ya Benk na nchi kwa ujumla.....

  PIA WADAU ANGALIENI HII( KESI HIZI ZIKO KISIASA ZAIDI NA KIKAMPENI ZAIDI HAKI ITENDEKE)
  Watumishi wa Bank Mkuu wasikunyingi wanne(Bosco Kimela,Mkango,Jengo na Farjallah)
  Inasemekana waliagiza pesa nyingi kwa niaba ya nchi je? Pesa hizo vipo au Zilitumika kwenye uchanguzi?je katika uagizaji bodi ilisema nini?

  Dr Hosea toa ushaidi wakutosha sio unajisafisha na Richmond.....
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Oct 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hii kesi imeshaanza kunukia 'uzombe.' Hebu angalia maswali ya jopo la mahakimu: "Majengo yamejengwa hayakujengwa? Liyumba alifaidika binafsi na upanuzi wa ujenzi huo? Je, kulikuwa na udanganyifu katika kiasi cha fedha kilichotumika katika ujenzi ujenzi huo? Sasa hasara inapatikanaje?" Hapa shahidi hakuweza kujibu swali hata moja na kusababisha kicheko toka kwa watu! Kaaazi kweli kweli!
   
 19. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0

  Inasemekana Balali na Liyumba ni mtu na binamu yake, aliyekuwa meneja mradi Kweka ni shemeji yake na Ben Mkapa sasa bado hapa kuna kesi?

  Majengo yapo lakini je kuna uwiano kati ya dhamani ya majengo na pesa halisi iliyotumika? Je kila kilichowekwa kwenye hayo majengo kilistahili kuweka kulingana na nature ya business ya shirika? Inawezekana tumewekewa madirisha bullet proof kwa vile supplier wa mjenzi alitushawishi tufanye hivyo kwa mtindo wa 10%. Huu ni ubadhilifu na ufisadi kwa manufaa binafsi.
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Oct 26, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Haya maswali yanafanana na yale ya jopo la mahakimu: "Je, kulikuwa na udanganyifu?" Hili swali linamaanisha kuhusu thamani ya jengo na fedha iliyotumika vinaendana? Sasa shahidi anaposhindwa kujibu swali hili la msingi si inaashiria kaupepo kabaya kwa upande wa mashtaka?
   
Loading...