Kesi ya kutorosha Twiga: Mwandishi jela baada ya aliyemdhamini kutoroka

Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,101
1,195

Moshi.
Mwandishi wa habari wa siku nyingi, Peter Temba amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kushindwa kumpeleka mahakamani mshtakiwa aliyemdhamini katika kesi ya kutorosha twiga kwenda Uarabuni.

Mwandishi huyo anayeandikia Gazeti la Serikali la Daily News na mwenzake aliyekuwa akiandikia Gazeti la Nipashe, Jackson Kimambo walimdhamini mtuhumiwa huyo raia wa Pakistan, Kamran Ahmed ambaye ni mshtakiwa namba moja katika kesi hiyo.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro ilitoa amri ya kuwakamata wadhamini hao baada ya mshtakiwa waliyemdhamini kwa kutia saini hati ya dhamana ya maneno ya (bond) ya Sh14.2 milioni, kutoroka.

Waandishi hao walimdhamini mshitakiwa huyo Juni 11, 2011 baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Moses Mzuna kuamuru kila mshtakiwa akabidhi mahakamani Sh14.2 milioni au mali yenye thamani hiyo.

Sharti la pili lilikuwa kila mshtakiwa katika kesi hiyo ya kutorosha twiga wanne na wanyama wengine 148 kwenda Uarabuni, kuwa na wadhamini wawili wakazi wa Kilimanjaro watakaosaini dhamana ya Sh14.2 milioni kila mmoja na waliojitokeza ni waandishi hao.

Kesi hiyo ikiwa katika hatua za usikilizwaji, Ahmed aliruka masharti ya dhamana na kwa miezi takriban mitano vyombo vya dola vimekuwa vikimtafuta kwa udi na uvumba bila mafanikio na hata wadhamini wake walishindwa kumpeleka mahakamani hadi ilipotolewa hati ya kuwakamata.

Temba alikamatwa Jumatatu wiki hii na kufikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa Mfawidhi, Simon Kobelo na alipoulizwa alipo mshtakiwa huyo alisema hajui na hana Sh14.2 milioni alizosaini kama dhamana.

Wakili wa Serikali, Stella Majaliwa aliomba sheria ichukue mkondo wake kwa kuwa mshtakiwa katika kesi hiyo pamoja na mdhamini wa pili hawajulikani walipo.

Kobelo alisema sheria iko wazi na kwamba kulingana na Kifungu cha 160(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, mdhamini huyo atatumikia kifungo cha miezi sita jela.

Kufungwa kwa mwandishi huyo kumeibua simanzi kubwa miongoni mwa wanahabari na familia yake hasa ikizingatiwa kuwa ni mwaka jana tu, alikatwa mguu mmoja kutokana na maradhi ya kisukari.

Chanzo:
Mwananchi
 
TEKNOLOJIA

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
4,306
2,000
W.a.p.u.m.b.a.v.u sana hao natamani kama wafungwe jela kisha funguo zitupwe mbali kabisa.Jitu kutoka nje ya nchi linaiba wanyama wetu halafu hawa waandishi wasaliti wa nchi wanajitokeza kumtilia dhamani,Natamani adhabu yao ya kifungo cha jela kiongezwe kiwe cha miaka 20 ili iwe fundisho kwa wapuuzi wengine.
 
mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
2,967

Mbona hiyo miaka 20 ni kidogo sana, wangepigwa kifungo cha maisha ili wakafie jela. sasa hii hukumu ya kifungo cha miez sita kina maana gani?
 
kkarumekenge

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
1,710
2,000
W.a.p.u.m.b.a.v.u sana hao natamani kama wafungwe jela kisha funguo zitupwe mbali kabisa.Jitu kutoka nje ya nchi linaiba wanyama wetu halafu hawa waandishi wasaliti wa nchi wanajitokeza kumtilia dhamani,Natamani adhabu yao ya kifungo cha jela kiongezwe kiwe cha miaka 20 ili iwe fundisho kwa wapuuzi wengine.
Kweli kabisa! Hao waandishi wameponzwa na njaa, bila shaka mwarabu aliwapa vilaki viwili ili wamdhamini. Njaa yao! Waarabu waibe na kusafirisha wanyama wetu, mwandishi wa habari, kioo cha jamii, ati ndiye awe mdhamini???? Imekula kwao!
 
ssafari

Senior Member
Jul 17, 2013
177
225
Duuuuu.Hao waandishi inawezekana walipewa chao mapema, kwani haiwezekani mtu toka nje ya nchi aje kuiba wanyama ambao ni rasilimali zetu sote watanzania halafu wewe umuwekee dhamana mwizi. Tanzania ni nchi yangu yenye maajabu mengi sana na mengi ya maajabu haya inawezekana yanapatikana Tanzania Pekee.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
W.a.p.u.m.b.a.v.u sana hao natamani kama wafungwe jela kisha funguo zitupwe mbali kabisa.Jitu kutoka nje ya nchi linaiba wanyama wetu halafu hawa waandishi wasaliti wa nchi wanajitokeza kumtilia dhamani,Natamani adhabu yao ya kifungo cha jela kiongezwe kiwe cha miaka 20 ili iwe fundisho kwa wapuuzi wengine.

Njaa kali.

Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi kila mdhamini alilipwa dola elfu ishirini cash kama bond ikiwa mshtakiwa atakimbia basi walipe hizo Million 14 za dhamana na zinazobaki ni usumbufu wao.

Naona Mwandishi amma kazila zote na sasa hana cha kulipa au kaona Million 14 ni bora aende jela na kwa vile yeye ni mgonjwa na mipango ya hapa na pale hiyo miezi 6 ataipiga akiwa hospitali.

Bongo Bingo.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,292
2,000
Kweli kabisa! Hao waandishi wameponzwa na njaa, bila shaka mwarabu aliwapa vilaki viwili ili wamdhamini. Njaa yao! Waarabu waibe na kusafirisha wanyama wetu, mwandishi wa habari, kioo cha jamii, ati ndiye awe mdhamini???? Imekula kwao!

Ewe punguani habari zimesema "raia wa Pakistan, Kamran Ahmed ambaye ni mshtakiwa namba moja". Sasa hao Waarabu wametokea wapi au hujui tofauti ya Mpakistan na "mwarabu".
 
mwanafyale

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
1,641
1,250
W.a.p.u.m.b.a.v.u sana hao natamani kama wafungwe jela kisha funguo zitupwe mbali kabisa.Jitu kutoka nje ya nchi linaiba wanyama wetu halafu hawa waandishi wasaliti wa nchi wanajitokeza kumtilia dhamani,Natamani adhabu yao ya kifungo cha jela kiongezwe kiwe cha miaka 20 ili iwe fundisho kwa wapuuzi wengine.
Kaka umesema kweli. Wafungwe tu. Tena nasikia walipewa mshiko wa laki tatu ili wawadhamini wajinga hao. Ujinga ulioje unaishia jela kwa ajili ya laki tatu. Kuendekeza njaa kubaya sana
 
Mandla Jr.

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
3,101
1,195
Njaa kali.

Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi kila mdhamini alilipwa dola elfu ishirini cash kama bond ikiwa mshtakiwa atakimbia basi walipe hizo Million 14 za dhamana na zinazobaki ni usumbufu wao.

Naona Mwandishi amma kazila zote na sasa hana cha kulipa au kaona Million 14 ni bora aende jela na kwa vile yeye ni mgonjwa na mipango ya hapa na pale hiyo miezi 6 ataipiga akiwa hospitali.

Bongo Bingo.

FF,
Hizo taarifa hata mimi nimezisikia pia. Ila hao waandishi wamezitafuna hizo pesa zote. Kumbuka pia ni wachaga hao.
 
OLESAIDIMU

JF-Expert Member
Dec 2, 2011
19,161
1,250
Ukisikia Mpakistan, Muiran yuko nchi ya watu na anatingisha kaaa macho 24/7................

Ila hakimu amenisononesha sana!!!!!!!!!
Anatoa adhabu kama vile hiyo miezi tunachana kwenye kalenda kusema itaisha!!!!!!!!!
 
sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,492
2,000
Njaa kali.

Kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi kila mdhamini alilipwa dola elfu ishirini cash kama bond ikiwa mshtakiwa atakimbia basi walipe hizo Million 14 za dhamana na zinazobaki ni usumbufu wao.

Naona Mwandishi amma kazila zote na sasa hana cha kulipa au kaona Million 14 ni bora aende jela na kwa vile yeye ni mgonjwa na mipango ya hapa na pale hiyo miezi 6 ataipiga akiwa hospitali.

Bongo Bingo.

Aiseee kwenda jela na baada ya miezi sita unatoka ukiwa US $20,000 richer kwa mchagga inalipa kabisa hiyo..
 
salomoe

JF-Expert Member
Sep 5, 2012
757
500
Ewe punguani habari zimesema "raia wa Pakistan, Kamran Ahmed ambaye ni mshtakiwa namba moja". Sasa hao Waarabu wametokea wapi au hujui tofauti ya Mpakistan na "mwarabu".

Sasa kuna sababu yoyote kumuita mwenzako punguani? Haya tueleweshe Mwarabu ni nani? Maana inajulikana Waarabu ndio waliohusika na utoroshaji wa Twiga.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom