Kesi ya kupinga uchaguzi Mkuu yafutwa rasmi

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
KESI YA KUPINGA UCHAGUZI MKUU 2020 KUONDOLEWA MAHAKAMANI

Mapema Leo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Kilimanjaro.
Diwani wa Machame Martini Munisi ameliondoa kusudiao la kufungua kesi ya ombi la kusogezwa mbele uchaguzi Mkuu wa 2020 kwa sababu ya janga la Covid -19 virusi vya corona.

Diwani huyo amesema kutokana na juhudi bora za Rais John Pombe Joseph Magufuli katika kupambana na janga hilo hadi kupelekea ugonjwa huo kutoweka kabisa nchini hana Shaka kabisa uchaguzi Mkuu utafanyika Kwa usalama wa hali ya juu.

Sambamba na hilo Diwani Munisi ameipongeza serikali Kwa kazi kubwa walioifanya ya kuwaongoza watanzania kwa kutumia njia mbadala na kutowafungia watanzania kisa gonjwa hilo.

Aidha Diwani munisi amewashauri wapinzani kutumia busara kwenye uchaguzi huu kwa kumwacha Rais John pombe Magufuli apite bila kupingwa kwani kwa kazi alizozifanya hakuna mtu anayeweza msogelea hata kwa kupata asilimia 2 ya Kura.Wapinzani tukutane kwenye majimbo na kata ila urais tumwachie JPM

 
Hivi mnaamini corona imekwisha! Mbona mpakani madereva wa Tanzania wanakutwa na Corona kila wakipimwa! Bila kupima tunathubutuje kusema imekwisha?
Kila siku majirani kama Kenya, Uganda na Rwanda wanatangaza takwimu, Tanzania hakuna takwimu.
Ukiambiwa, changanya na za kwako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom