Kesi ya kupinga ubunge wa mh.tundu lissu yanguruma tena leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya kupinga ubunge wa mh.tundu lissu yanguruma tena leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NGAGHE, Mar 14, 2012.

 1. N

  NGAGHE Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na ubunge wa mh. Tundu Lissu imenguruma tena leo baada ya kuahirishwa jumatatu 12/3/2012.Jaji MZUNA alitupilia mbali madai 7 ya walalamikaji(selema na paskali),kamtaka Lissu hoja 6 na kuwataka walalamikaji wathibitishe madai yao 6.Baadhi ya hoja ambazo Lissu anapaswa azijibu ni kuhonga mawakala kwa chakula,askari polisi kumpigia kampeni siku ya uchaguzi,kusafirisha wapiga kutoka Taru hadi Mangonyi,msimamisi wa kituo kimojawapo kuchakachua matokeo kuhonga wapiga kura n.k.Walalamikaji waliamriwa wakalipe gharama ya shauri Dodoma ambazo 200,000/= na wamelipa 12,500/= pamoja na kuleta ushahidi wa yale wanayomtuhumu. kesi hiyo itaendelea tena jumanne ijayo.Tutapeana taarifa kadri mambo yatakavyoenda.
  source:nilikuwepo mwenye mahakamani.kesi ilianza yapata saa saba mchana.
   
 2. M

  MASEBUNA JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tuna shukuru kwa taarifa lakini binafsi kujakusoma vema naomba ufafanuzi unaposema aliwataka wakalipe gharama za shauri dodoma tsh lak 2 then wakalipa 12500 = hapo kiukweli sijakusoma naomba ufafanuzi
   
 3. N

  NGAGHE Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walalamikaji haohao walifungua kesi mara baada ya uchaguzi na kesi ilifika hadi mahakama kuu kanda ya kati ambapo lissu aliibuka mshindi.gharama za kufungua kesi ya uchaguzi mahakama kuu ni 200,000/= lakini lakini ukilipa pungufu kesi inaendelea.Lissu alisimamia hoja kwamba walipe gharama ya kesi ile ya kwanza ndipo hii iendelee kwani wao walilipa 12,500 tu kwa kesi ya kwanza.ndo maana jaji jawamuru wakamalize lile deni la kesi ya kwanza.
   
 4. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hao walalamikaji uchwara wameshaingizwa mjini tayari na mgombea wa CCM aliyeshindwa baada ya yeye kuusoma upepo ndiyo maana hawapatii hela kama DIALLO alivyowaingiza mjini wazee fulani hapa Mwanza na kusabisha Highnes Kiwia mbunge wa Ilemela kushinda kesi yake wiki iliyopita chini ya usimamizi wa Lissu.
   
 5. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawemwezi kamanda lissu bora waifute hiyo kesi
   
 6. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii wala haitusumbui,mbele ya gwiji la sheria.werema na kombani plus bibi kiroboto hawataki kutia mguu mmoja na lissu,itakuwa hawa wachovu wa manyoni
   
Loading...