Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Diallo Oktoba 17,2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Diallo Oktoba 17,2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, Oct 13, 2011.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  MAHAKAMA kuu ya kanda ya Mwanza itaanza kusikiliza shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita katika jimbo la Ilemela ambayo yalimpa ushindi mbunge Highness Samson (Chadema) dhidi ya Anthony Diallo (CCM), Oktoba 17 mwaka huu.  Shauri hilo namba 12/2010 lilifunguliwa na wakazi watatu wa Ilemela Yusufu Masegeja Lupilya, Nuru Ramadhani Nsubugu na Beatus Martin Madenge, limepanga kuanza kusikilizwa Oktoba 17 mwaka huu mbele ya Jaji Mfawidhi Gadi Mjemas wa mahakama kuu kanda ya Bukoba.


  Akizungumza na waandishi wa habari msajili wa mahakama wa wilaya ya Mwanza Isaya Arufani alisema katika shauri hilo, wakazi hao wa Wilaya ya Ilemela wanamlalamikia Mgombea ubunge wa Chadema Highness Samson, msimamizi wa Uchaguzi wa jimo la Ilemela ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Willson Kabwe na Mwanasheria mkuu wa serikali.


  “Baada ya kufunguliwa kwa shauri hilo mwaka jana, mahakama ilipitia hoja za maombi ya kufungua shauri hilo na kujiridhisha, tayari ameshapangiwa Jaji Mjemas hivyo sasa limepagwa kuanza kusikilizwa mwezi huu wa Oktoba 17,” alieleza msajili huyo wa mahakama.


  Matokeo ya uchaguzi huo yanayopingwa ni kuwa Highness Samson aliweza kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunge wa jimbo la Ilemela kwa kumshinda Anthony Diallo wa CCM kwa kura 31,269 dhidi ya kura 26,270 hii ikiwa ni tofauti ya kura 4,999.


  Hata havyo walalamikaji katika upigaji wa matokeo hayo ya uchaguzi wanapinga ushindi huo wakidai kuwa Tume ya Uchaguzi ilihamisha vituo bila utaratibu ikiwa ni pamoja na kuweka orodha ya majina ya wapiga kura ambao ni marehemu hivyo kuufanya uchaguzi kwa jimbo hilo kuharibika.


  Wakati huo huo, Msajili wa mahakama ya Wilaya ya Mwanza amesema katika shauri lingine la kupinga uchaguzi wa Matokeo ya Ubunge Jimbo la Mwibara wilayani Bunda limemalizika na sasa linangoja hukumu toka kwa Jaji.


  Alisema shauri hilo ambalo ni namba 7/2010 tayari limeshasikilizwa na pande zote mbili na kwamba kilichobakia ni kugojea jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo kukamilisha hukumu yake na ndipo itapangiwa siku ya kusomwa.


  Alisema shauri hilo lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa Tiketi ya Chadema Chiriko Harun David dhidi ya Alphaxad Lugora wa CCM, msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Mwibara pamoja na Mwanasheria wa serikali.


  “Baada ya shauri hilo kusikilizwa mahakama ilitoa muwa wa mwisho kwao pande zote mbili kuandaa majumuisho na tayari wamekamilisha ambapo yamekwisha wasilisha na kilichobakia ni kukamilika kwa hukumu ambayo inatayarishwa na Jaji Chocha, Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Songea,” alieleza.
   
 2. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa jinsi CCM ilivyo katika hali mbaya ningekuwa mimi ni Diallo ningeifutilia mbali hiyo kesi!
   
 3. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hata mimi
   
 4. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  diallo hajachoka akaachia vijana? Mbona mwenzio kaamua kwenda kusimamia bize zake? Wewe si billionaire hapa mwanza, kwa nini usitulie ukasimamia miradi yako?
   
 5. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #5
  Oct 13, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama inawezekana watengue tu matokeo leo hiihii na uchaguzi mdogo ufanyike kesho, ili tutoe somo kwa wa na igunga na magamba kwa ujumla it seems hawaamini kilichotokea na safarihii diallo ata pata kura 2 tu ,yake na ya wife wake periodii
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,651
  Likes Received: 21,866
  Trophy Points: 280
  Aliyefungua kesi hiyo si Diallo.
   
 7. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mara hii tena uchguzi mdogo unanyemelea? Tumechoka kuona fedha za walipa kodi zikiteketea
   
 8. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kabisa haruko tayari hela zetu zinateketezwa wakati kuna shida na mahitaji mahosipitalini, mashuleni, barabara, maji na huduma nyingine. Zile Bilioni 3 za Igunga zingefanya mambo makubwa sana.
  Hawa CCM niewachoka jamani
   
 9. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Huko Mwibala vipi kuna matumaini ya kushinda kesi kwa CDM?
   
 10. j

  juniorfeb18 Member

  #10
  Oct 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mimi natamani ccm washinde hii kesi ya ilemela,ili wanailemela tuwaaibishe zaidi ccm,nina hakika,katika kura 60000,hawatapata hata 5000!!natamani 2015 ingekuwa mwakani!!
   
 11. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Tafadhali sana badili heading yako, hakuna jimbo la uchaguzi Tanzania linaitwa jimbo la Diallo!
   
Loading...