Kesi ya kumtishia mke wa Mbowe yaunguruma

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797




Na Angelina Mganga

KESI ya kutishia kuua kwa maneno iliyofunguliwa na mke wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe katika Mahakama ya
Mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam, imeanza kuunguruma.

Hakimu Jonas Mahende jana alianza kusikiliza ushahidi wa mlalamikaji dhidi ya mlinzi wa Klabu ya Bilicanas, Bw. Herman John (36) anayedaiwa kutishia kumuua kwa kumtumia ujumbe mfupi wa maneno.

Ilidaiwa mahakamani hapo na Karani, Bi. Hatanawe Kitogo kuwa Februari 3 mwaka huu, katika club hiyo iliyopo wilayani Ilala, Dar es Salaam, Bw. John alitishia kumuua Lilian.

Bi. Kitogo alidai kuwa, mshtakiwa alituma ujumbe mfupi wa maneno kupitia namba 0762 055605 uliosema kuwa anampa siku saba Lilian amuachishe kazi mtu anayeitwa Power, na kima cha chini cha mshahara wake kiwe 320,000/- la sivyo atakuwa hatarini.

Bi Mbowe aliileza mahakama kuwa mlamikaji alianza kazi ya ulinzi nyumbani kwake Mikocheni mwaka 2009 tangu alipoajiriwa na baadaye kulinda kwenye klabu hiyo.

Bi. Mbowe alieleza kuwa baada ya kupokea ujumbe huo, aliamua kushauriana na mumewe ili amhoji mshtakiwa, lakini mumewe alimwambia akaripoti polisi.

Shahidi namba moja FF 2255 DC Mboka (35) alithibitisha kuwa wakati wa upelezi, mshtakuwa alikutwa na laini mbili za simu na askari alipata uhakika kupitia Vodacom kujua simu iliyotumika kutuma ujumbe huo ni ya mshitakiwa.

Shahidi wa pili Julius Paul (51) ambaye ni Meneja wa Klabu Bilicanas, alimhamisha mshitakiwa kwenda kulinda Mikocheni kwa mama huyo na ndipo alitoa maneno ya vitisho ya kuongezwa mshahara na hadhi kwa wafanyakazi.

Kesi imeahirishwa mpaka Mei 3, mwaka huu ili mshtakiwa aanze kujitetea kutokana na vielelezo vilivyoletwa na mlalamikaji.
 
Back
Top Bottom