Kesi ya kumiliki silaha kinyume na sheria inayomkabili mfanyabiashara Salehe Salim Alamri na wenzake yapigwa kalenda

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Kesi ya kumiliki silaha kinyume na sheria inayomkabili mfanyabiashara,Salehe Salim Alamri na wenzake imehairishwa leo katika mahakama ya wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Kesi hiyo nambari 11 ya mwaka 2020 imehairishwa leo na hakimu wa mahakama hiyo,Jumaa Mwambago hadi Agosti 21 mwaka huu baada ya upande wa jamhuri kueleza kwamba upelelezi bado haujakamilika.

Katika kesi hiyo Mfanyabiashara huyo anadaiwa mnamo Julai 26 mwaka 2019 akiwa katika eneo la Makame Kijenge jijini Arusha alikutwa akimiliki silaha aina ya Riffle CAR 22 No. 00104516 kinyume na sheria.

Pia mfanyabiashara huyo siku hiyo hiyo alikutwa na silaha nyingine aina ya Shotgun yenye nambari 00104513 mali ya HSK Safaris Ltd aliyokuwa akiimiliki bila leseni wala kibali cha umiliki kutoka mamlaka husika.

Mbali na mfanyabiashara huyo mtuhumiwa mwingine,Gerald Joseh Ole Kashiro anashtakiwa kwa kosa la kushindwa kutunza silaha sehemu salama kinyume na sheria nambari 59(1)(a) na sheria nambari 61 ya sera ya udhibiti wa silaha nambari 2 ya mwaka 2015.

Katika shitaka hilo Ole Kashiro anadaiwa mnamo Febuari 20 mwaka 2020 akiwa katika pori ya hifadhi ya akiba ya Simanjiro ndani ya wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara alishindwa kuhifadhi sehemu salama silaha aina ya Rifle 300mm No.A757677 na nyingine aina ya Shotogun 12bore No.T.0611018 na kishindwa kuzihifadhi sehemu salama hali iliyopelekea kuangukia mikononi mwa mtu asiyekuwa na uhalali kisheria.

Itakumbukwa ya kwamba mbali na mashtaka anayokabiliwa Ole Kashiro lakini pia anatumikia kifungo cha miaka 30 katika gereza la mkoa Manyara kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali katika kesi ya uhujumu uchumi nambari 21 ya mwaka 2019 hukumu iliyosomwa na hakimu Jumaa Mwambago.

Nje ya mahakama hiyo Mfanyabiashara Salehe Salim Alamri alionekana kusindikizwa na askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha aliyetambulika kwa jina moja la Koplo Idrisa hali iliyoibua mshangao mahakamani hapo.

Askari huyo ambaye hakuwa katika eneo lake la kazi alionekana mahakamani hapo akiambatana na mfanyabiashara huyo anayeishi mkoani Arusha kila kona ya mahakama na kisha kumfungulia mlango na kumpakia kwenye gari aina ya Vx Landcruiser nambari T366 DLX ambayo alikuwa akiiendesha mwenyewe na kisha kutokomea mahakamani hapo.

Mwisho.

Pichani chini mfanyabiashara Salehe Alamri anayekabiliwa na kesi ya umiliki wa silaha kinyume na sheria aliyevalia suruali ya kijani akisindikizwa na askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha,Koplo Idrisa kutoka nje ya mahakama baada ya kesi inayomkabili kuhairishwa leo.

Picha nyingine Askari huyo akionekana kumfungulia mlango wa gari mfanyabiashara huyo ili aweze kupanda.

847A1EE0-B960-47BD-A2A9-EC71D81C6ACA.jpeg

41BE1FD6-9F05-4B10-9154-C665BD52B7C6.jpeg

C5D024E9-211F-4027-BC38-50D0A64C1A72.jpeg
 
Back
Top Bottom