Kesi ya kuku umshitaki kwa kunguru

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
MSAJILI WA VYAMA UKIMYA WAKO UNATIA SHAKA:

Kwa mujibu wa Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa Mwaka 2007, zilizotungwa chini ya fungu la 22(h) la Sheria ya Vyama vya Siasa (SURA YA 258) na kutangazwa Rasmi na Tangazo la Serikali Na. 215 la tarehe 12/10/2007, tunajifunza mambo kadhaa yakiwemo yafuatayo:

HAKI ZA VYAMA VYA SIASA:

Kanuni namba 4(1) (a)-(e) inataeleza Haki za Vyama vya Siasa. Kwa mfano, Kanuni ya 4(1)(e) inasema:

“ Kila Chama cha Siasa kitakuwa na haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na maandamano kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa”.

WAJIBU WA VYAMA VYA SIASA:

Kanuni namba 5 inazungumzia Wajibu wa Vyama vya Siasa, ambapo Kanuni ya 5(1)(c) inasema:

“Kila Chama cha Siasa kitakuwa na wajibu wa kutunza Maadili chini ya Kanuni hizi kwa kutotumia vyombo vya dola kukandamiza na kutoa vitisho kwa chama cha siasa kingine kwa manufaa yake”.
Isitoshe Kanuni ya 5(1)(i) inaeleza:

“Kila Chama cha Siasa kitakuwa na wajibu wa kutunza Maadili chini ya Kanuni hizi kwa kuepuka kutumia mamlaka, rasilimali za Serikali, Vyombo vya Dola, au Wadhifa wa Kiserikali, kisiasa au ufadhili wan je ama wa ndani kwa namna yoyote ile ili kukandamiza chama kingine”.

Ndugu Msajili wa Vyama, yanayoendelea Kufanywa na Serikali ya CCM chini ya Rais John Pombe Magufuli, yanapoka Haki ya Vyama vya Siasa kama zilivyoainishwa kwenye Kanuni Namba 4 na pia, Ndugu John Pombe Magufuli akiwa kama Kiongozi Mwandamizi na Mwenyekiti Mtarajiwa wa Chama cha Mapinduzi, anamaanisha CCM kama Chama cha Siasa kinagoma Kutekeleza Wajibu wake kama ilivyo kwenye Kanuni ya 5. Naomba nikukumbushe Wajibu wako kama ilivyobainishwa kwenye Kanuni namba 6.

WAJIBU WA MSAJILI:

6(1)(a) Kusimamia Maadili ya Vyama vya Siasa;

6(1) (c ) Kuzuia kitendo cha uvunjifu wa Kanuni za Maadili kisiendelee na kukitaka chama au kumtaka KIONGOZI WA CHAMA kujirekebisha;

6(1) (d) Kutoa onyo la maandishi kwa chama au kiongozi wa chama husika.

Ndugu Msajili wa Vyama, ninakuomba utekeleze Wajibu wako kuzuia Ukiukwaji wa Maadili ya Vyama vya Siasa unaoendelea kufanywa na CCM na Serikali yak echini ya Ndugu Magufuli. Kumbuka pia kwamba ni Wajibu wako Kukemea hadharani endapo ulishatoa Onyo la Maandishi na bado CCM au Kiongozi wake anakaidi. Ukimya wako kwa kipindi hiki ambapo Kanuni , Sheria na Katiba vinachezewa utaligharimu Taifa.
 
Back
Top Bottom