Kesi ya kuhoji matokeo ya urais yafunguliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kesi ya kuhoji matokeo ya urais yafunguliwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Oct 15, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,618
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280  UCHAGUZI mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu unaweza kuingia mushkeli baada ya mkazi wa Dar es Salaam, Denis Maringo kufungua kesi ya kikatiba akihoji sheria inayozuia matokeo ya rais kupingwa baada ya kutangazwa na Tume ya Uchaguzi (Nec). Katika kesi hiyo ya madai namba 86 ya mwaka 2010 iliyofunguliwa juzi,

  Maringo anataka mahakama itoe ufafanuzi wa mambo hayo kabla ya kufanyika uchaguzi huo. Maringo pia anadai kuwa Rais Jakaya Kikwete alivunja katiba kwa kulivunja Bunge kabla ya kumalizika muda wake wa miaka mitano. Kwa mujibu wa Maringo, Bunge la Tisa la Jamhuri la Muungano wa Tanzania lililoingia madarakani mwezi Desemba mwaka 2005, lilipaswa kuvunjwa Desemba 5 mwaka huu badala ya Julai 17 kama alivyofanya rais.

  "Tunaitaka Mahakama itamke kuwa kifungu 41(7) cha katiba kinapingana na kifungu namba 13(6)(a) kinachohusu mgawanyo wa madaraka na uhuru wa mahakama kwa kueleza kuwa matokeo ya urais baada ya kutangazwa na Nec hayawezi kupingwa," inasema sehemu ya madai hayo. "Kitendo cha rais kulivunja Bunge tarehe 17 Julai ni kinyume na kifungu namba 65(1) cha katiba ya Jamhuri ya Muungano ambacho kinaeleza kuwa kipindi cha muda wa Bunge ni miaka mitano," imesema sehemu ya hati hiyo.

  "Kifungu cha 46A cha katiba kimetamka bayana kuwa rais hatalivunja Bunge wakati akijua kuwa mwenyewe (rais) bado yupo madarakani kwa lengo la kuleta uwiano wa madaraka." Maringo amefungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Nec akiwa ni Mtanzania aliyejiandikisha kupiga kura.

  Katika kesi hiyo, anashirikiana na Kituo cha Haki na Demokrasia (CJD). Mbali na madai hayo ya awali, walalamikaji wametaka wabunge kurejesha fedha za walipa kodi walizopewa kwa ajili ya mafao yao, wakidai kuwa hawastahili kulipwa kwa kuwa hawakulitumikia Bunge kwa muda uliotakiwa. Madai mengine yaliyotolewa na walalamikaji hao ni pamoja na kupinga umri wa mgombea urais kuwa miaka 40. Walisema Mahakama inapaswa kuirekebisha sheria hiyo kwa kuwa ni ya kibaguzi.

  Walalamikaji hao pia wameiomba Mahakama kuondoa zuio liliolowekwa na baadhi ya vyama vya siasa kwa wagombea wake kushiriki midahalo ya uchaguzi kwenye vyombo vya habari wakisema hatua hiyo inawanyima wagombea hao fursa ya kujieleza; na wapigakura haki ya kujua sera za wagombea wanaopaswa kuwachagua.

  Madai mengine yaliyoelezwa kwenye hati hiyo ni kupinga mipaka ya kijiografia ya majimbo ya uchaguzi na upigaji kura iliyowekwa na Nec kwa maelezo kuwa yataleta matokeo yasiyo ya haki kwa wapigakura.Walalamikaji wametaka pia Nec itafsiri sheria za uchaguzi kwa lugha ya Kiswahili kuwawezesha wapigakura wote kuzifahamu na kujua haki zao kabla ya kufanya uamuzi.

  "Sheria inayomtaka mgombea kujua kuzumgumza Kiswahili tu ni mbovu kwani sheria zote huandikwa kwa lugha ya Kiingereza ingawa mijadala bungeni na mambo mengine ya serikali hufanyika kwa Kiingereza," anasema Maringo katika hati hiyo.

  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nawaunga mkono kuhusu suala la matokeo ya urais kutokuhojiwa na mahakama japokuwa watakumbana na Ibara ya 74 (12) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 ambayo inadai kwamba

  "Hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililotendwa na Tume ya Uchaguzi katika kutekeleza madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii."

  Kwa kuwa Mahakama sasa hivi inaongozwa na CJ (Justice Augustino Ramadhan) ambaye ni POLITICIAN (refer kesi ya mgombea binafsi) jambo hili halitaweza kufanikiwa hata kidogo!

  Hili la Sheria ya Uchaguzi kutafsiriwa kwa Kiswahili wanaisumbua tu Mahakama kwani Sheria ya Uchaguzi (Cap. 343, R. E. 2002) imeshatafsriwa kwa Kiswahili.

  Kuhusu Bunge kuvunjwa kabla ya wakati (ie miaka 5) hata kama kifungu Rais amevunja Katiba, remedy yake sio kumpeleka mahakamani, bali ni Bunge kumshtaki (impeach) kulingana na Ibara ya 46A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977. Tukirejea Kesi ya MWALIMU PAUL JOHN MHOZYA v ATTORNEY GENERAL [1996] TLR 130 Mahakama Kuu ilikuwa na haya ya kusema katika ukurasa wa 131:


  (iv) As s 42(3)(d) of the Constitution states that the President shall be in office until he ceases to hold office `in accordance with the provisions of' the Constitution, and s 46A of the Constitution lays down the procedure by which the legislature may remove or suspend the President from office, any attempt to remove or suspend the President in a manner other than that laid down in the Constitution would not be legal;
  (v) No provision of the Constitution or any other law authorises the High Court to hold that the President can be removed or suspended from office by a body other than that which the Constitution specifically provides for;
  (vi) This Court has no jurisdiction to issue the order of injunction sought against the President.
   
 3. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ashirikiane na askofu mtiikila. Maombi zaidi yanatosha kupata jibu.ila mahakamani hadi uchaguzi upite ndo atapata maelezo.
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kazi ipo...waacheni akiingia DR Slaa hiyo katiba tunaifumua
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Oct 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ni kweli, Dr Slaa is a right man for the job! Sio muoga wa mabadiliko kama "Dkt" Kikwete!
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  mkuu umenifurahisha sana kumbe kuna Dr. na Dkt.
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mkuu, kwa mtazamo wangu Dr Slaa ataandika katiba. Hakuna katiba ya kufumuliwa hapa Tanzania, kwani tz haina katiba, na ndiyo maana
  1-hakuna respect ya rule of law
  2-mhimili mwingine wa dola unaweza kudharau mahakama na mahakama ikaufyata kumbuka kesi ya mgombea binafsi.
  3-watz hatuwezi kugoma wala kuandamana maana hiyo haki hatuna-hakuna mahali ilipoandikwa.
   
Loading...