Kesi ya Kiongozi Uamsho: Mawakili watishia kujitoa, Sheikh Farid anyolewa ndevu...

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Kesi imetajwa leo katika mahakama ya Mwanakwerekwe na kisha ikahamishiwa katika mahakama ya Vuga.

Mawakili wametishia kujitoa katika kesi hyo kwa madai ya usumbufu wanaoupata wateja wao. Mawakili hao ni Salim Tawfik na Abdallah Juma wanaowawakilisha Sheikh Farid Hadi Ahmed na wenzake sita. Leo hii wamesusa kabisa kuingia mahakamani na wamesema wanakusudia kujitoa kutokana na uusmbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuhawangaisha.

Na sasa hivi mawakili hao wameshaondoka na watuhumiwa ndio wanafikishwa mahakamani wakiwa wamenyolewa ndevu zote wakiwa mahabusu. Kesi leo inatarajiwa kutolewa maamuzi ya masharti ya dhamana yaliyokuwa yanapingwa na mawakili wa utetezi ambao wameshaondoka mahakamani hapa.

Hatujui nini kitaendelea tena maana watu wamezuiliwa kuingia katika eneo la mahakamani. Nikipata updates nitawajulisha

Updates:
406877_300222736744489_1479620875_n.jpg

Mawakili wakisoma tamko la kutaka kujitoa kabla hawajaondoka mahakamani hapo.

293737_300224926744270_948112269_n.jpg


Sheikh Farid akiwa kanyolewa ndevu akiwasili mahakama ya Vuga leo.

MORE UPDATES:

Sheikh Farid na wenzake wasomewa mashtaka mapya:
1) Kusababisha uvinjifu wa amani zanziba
2) Kusababisha uharibifu wa mali kisiwani zanzibar kutokana na vurugu
3) Kushawishi na kuchochea vurugu zilizosababisha kuhatarisha maisha ya watu na serikali kuingia hasaraK

Aidha mtuhumiwa mmoja anatuhumiwa kumtukana Kamishna wa Polisi Zanzibar Musa Ally Musa


washtakiwa wote wamenyimwa dhamana kwani ni Jaji pekee ndie anayeweza kutoa dhamana kwa makosa yao lakini wana haki ya kukata rufaa kudai dhamana katika mahakama ya juu.
 
viongozi wa jumuia ya kiislamu zanzibar wameshitakiwa kwa makosa matatu katika mahakama ya vuga akiyaeleza mashtaka hayo kupitia afisi ya mkurugenzi wa mashtaka zanzibar ameseama kuwa ni

(1) viongozi hao wamesababisha uvunjifu wa amani nchini
...
(2) kisababisha uharibifu wa miundo mbinu nchini
(3) kuwashawishi rai kufanya vitendo vya fujo kitu ambacho kimeipelekea ser
ikali kuingia hasara kubwa sana na kosa la nne ameshitakiwa sheikh azzan pekeake kwa kumtukana hadharani kamishna wa polisi zanzibar bwana mussa ali musaa.

Washitakiwa hao wamenyimwa dhamana kwa sababu certificate inayoendesha kesi hio inamyima mrajisi wamashtaka kutoa dhamana kwa washitakiwa hao isipokuwa mtu ambae angeweza kutoa dhaman ya kesi hio jaji.

Na kwa upande wao washitakiwa hao wameiomba mahakama kuwapatia dhamana kwani ukitizama kabisa inaonekana kuwa kesi hio imepangwa kwa lengo la kuwadhoofisha kwanni hapo mwanzoni kesi hio ilipangiwa kwerekwe wameshangaa kuletwa mahakama ya vuga.

Pia wamesema kuwa wao ni raia halali wa nchi kwa hio wanastahiki kupewa dhamana iikinlinganisha wao kuwa ni wahudumikiaji wakuu wa familia.

Pia mrajisi huyo amesema kuwa washitakiwa hao wanayohaki yakukata rufaa kuhusu kupewa dhamana,kwa sasa washitakiwa hao wamerejeshwa tena rumande hadi uchunguzi utakapokamilika juu ya makosa yao.
 
Huyo jamaa anapenda sana kubeba hotpot kuna msahaafu ndani nn?
 
Back
Top Bottom