kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,418
- 7,206
Hili suala la mamlaka nchini kuonekana kutumia nguvu isiyokua ya kawaida kuidhibiti chadema isiweze kuwavua wanachama wake uanachama linastaajabisha wengi.
Tumeona na kuzoea kuona chama cha mapinduzi kuweza kumng'oa kirahisi mbunge wake anayeenda kinyume na chama bungeni kwa kumfuta uanachama.
Hili linawezekana kutokana na haki iliyokua nayo chama cha siasa kumfuta mwanachama wake uanachama kufuatana na katiba na taratibu waliyojiwekea.
Akina Halima mdee baada ya chama chao kuona walifanya ulaghai kuteuliwa kuwa wabunge viti maaluum kwa kugushi nyaraka kiliwafukuza uanachama.
Katika hali ya kawaida speaker alitakiwa kusitisha ubunge wao ila la ajabu danadana zinaendelea wakiendelea kula mishahara na posho za ubunge karibu mwaka wa pili utaisha.
Inaelekea fedha inatumika kuhakikisha wanabakia wabunge ikiwezekana kwa muhula wote wa miaka mitano huku wakiwa sio wanachama wa chama chochote.
Haki ya kumtimua mtu uanachama isiwe jambo gumu kwa chama chochote cha siasa. Ukiona linaingiliwa na utawala hadi mahakama basi kuna matatizo makubwa kuhusu demokrasia nchini.