Kesi ya kina Mbowe: Wakili John Malya naye alimbananisha SSP Ngichi

C

chidayo

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Messages
264
Points
500
Age
31
C

chidayo

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2016
264 500
_
MALYA: Ulipojiunga na Jeshi la polisi ulikuwa na miaka mingapi?

SSP Ngichi: 28

MALYA: Kwa mujibu wa PGO ni sahihi kwamba mtu akiwa na miaka 28 haruhusiwi kujiunga na jeshi la Polisi?

SSP Ngichi: Inategemea na elimu yake

MALYA: Kesi unayoitolea ushahidi inahusiana na maswala ya uchaguzi, nyie kama wadau mlipewa elimu ya usimamizi wa uchaguzi?

SSP Ngichi: Natolea ushahidi kesi ya maandamano sio mambo ya uchaguzi

MALYA: Lakini hayo maandamano si yanatokana na uchaguzi?

SSP Ngichi: Ndio

MALYA: Ulipewa ratiba ya mikutano ya vyama vya siasa?

SSP Ngichi: Ndio

MALYA: Nani alikupatia?

SSP Ngichi: RPC Kinondoni

MALYA: Yeye alipewa na nani?

SSP Ngichi: Mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni

MALYA: Kifungu cha 51 (5) cha sheria ya Uchaguzi kinamtaka Mkuu wa Wilaya ndiye awape polisi nakala ya Ratiba za kampeni. Kwa kifungu hiki, huoni kwamba mmevunja sheria?

SSP Ngichi: Kimya

MALYA: Vituo vya kupiga kura vilikuwa vingapi?

SSP Ngichi: Sikumbuki idadi yake

MALYA: RCO unasimamiaje uchaguzi ambao hujui hata idadi ya vituo?

SSP Ngichi: Vilikua zaidi ya hamsini

MALYA: Unafahamu mawakala lazima wale kiapo?

SSP Ngichi: Ndio

MALYA: Unafahamu kila mgombea anaweka utaratibu na Mkurugenzi wa namna mawakala wake kuapa?

SSP Ngichi: Ndio

MALYA: Kwahiyo mlifanya makosa kuvuruga mawakala wa Chadema kwenda kuapa?

SSP Ngichi: Walifanya maandamano

MALYA: Ulijuaje ni maandamano?

SSP Ngichi: Walivuka barabara

MALYA: kama walivuka barabara ulijuaje kama walikuwa wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba?

SSP Ngichi: Hazifanyiki barabarani

MALYA: Zinafanyika wapi?

SSP Ngichi: Nyumbani

MALYA: Ili ufike nyumbani unapita wapi?

SSP Ngichi: Barabarani

MALYA: Kwahiyo unakubali walikua wanavuka barabara ili wakafanye kampeni za nyumba kwa nyumba?

SSP Ngichi: Waliandamana

MALYA: Kwanini?

SSP Ngichi: Kwa sababu walikua na viongozi wao

MALYA: Wataje

SSP Ngichi: Heche, Matiko, Msigwa na wengine

MALYA: Unajua sifa za mtu kuwa wakala?

SSP Ngichi: Hapana

MALYA: Unajua kuwa Heche, Matiko na Msigwa walikua mawakala?

SSP Ngichi: Sifahamu

MALYA: Je unakubali kwamba viongozi hao walikua wanaongozana na mawakala wenzao kwenda kwa Mkurugenzi kula kiapo?

SSP Ngichi: Kimya
 
Terrible Teen

Terrible Teen

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2017
Messages
358
Points
1,000
Terrible Teen

Terrible Teen

JF-Expert Member
Joined May 1, 2017
358 1,000
Dah! Hii ni zaraui, siku mkiingia mikononi mwao ........
sasa kwani wanalala ndani? hawa watu walitakiwa wawe marafiki wa raia na sio kuwanyanyasa. Polisi wana maisha magumu sana, wanalala nje kulinda maboss wao ndani wakila matunda ya ndoa zao.
 
upendodaima

upendodaima

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Messages
3,249
Points
2,000
upendodaima

upendodaima

JF-Expert Member
Joined May 23, 2013
3,249 2,000
Hakimu aingilie kati haraka iwezekanavyo,anachofanyiwa Afande Ngichi ni udhalilishaji. 😂 😂 😂
 
uungwana classic

uungwana classic

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2014
Messages
1,847
Points
2,000
Age
25
uungwana classic

uungwana classic

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2014
1,847 2,000
Mahakamani ni balaa kwa hali hii unaweza ingia kama shahidi na ukatoka mtuhumiwa au hata mshatakiwa
 
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2011
Messages
910
Points
500
Age
37
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2011
910 500
Sehemu ya mahojiano kati ya Wakili msomi John Malya na Mkuu wa upelelezi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Mrakibu mwandamizi wa Polisi (SSP) Gerald Ngichi.

MALYA: Una miaka mingapi?

SSP Ngichi: 47

MALYA: Ulizaliwa mwaka gani?

SSP Ngichi: 1972

MALYA: Wakati unajiunga na Jeshi la Polisi ulikuwa na Miaka mingapi?

SSP Ngichi: Kimya

HAKIMU: Shahidi jibu tafadhali

MALYA: Kama hukumbuki nikusaidie?

SSP Ngichi: Nilikua na miaka 28

MALYA: Ulikuwa na taaluma gani?

SSP Ngichi: Degree ya Sheria

MALYA: Kwa mujibu wa PGO ni sahihi kwamba mtu akiwa na miaka 28 haruhusiwi kujiunga na jeshi la Polisi?

SSP Ngichi: Inategemea na elimu yake

MALYA: Kesi unayoitolea ushahidi inahusiana na maswala ya uchaguzi nyinyi kama wadau mlipewa elimu juu ya usimamizi wa uchaguzi?

SSP Ngichi: Natolea ushahidi kesi ya maandamano sio mambo ya uchaguzi

MALYA: Lakini hayo maandamano si yanatokana na uchaguzi?

SSP Ngichi: Ndio

MALYA: Ulipewa ratiba ya mikutano ya vyama vya siasa?

SSP Ngichi: Ndio

MALYA: Nani alikupatia?

SSP Ngichi: RPC Kinondoni

MALYA: Yeye alipewa na nani?

SSP Ngichi: Mkurugenzi wa Manispaa Kinondoni

MALYA: Kifungu cha 51 (5) cha sheria ya Uchaguzi kinamtaka Mkuu wa Wilaya ndiye awape polisi nakala ya Ratiba za kampeni. Kwa kifungu hiki, huoni kwamba mmevunja sheria?

SSP Ngichi: Kimya

MALYA: Vituo vya kupiga kura vilikuwa vingapi?

SSP Ngichi: Vingi sikumbuki idadi yake

MALYA: Unasimamiaje uchaguzi ambao hujui hata idadi ya vituo?

SSP Ngichi: Vilikua zaidi ya Hamsini

MALYA: Unafahamu mawakala lazima wale kiapo?

SSP Ngichi: Ndio

MALYA: Unafahamu kila mgombea anaweka utaratibu na Mkurugenzi wa namna mawakala wake kuapa?

SSP Ngichi: Ndio

MALYA: Kwahiyo mlifanya makosa kuvuruga mawakala wa Chadema kwenda kuapa?

SSP Ngichi: Walifanya maandamano yasiyo halali

MALYA: Ulijuaje ni maandamano?

SSP Ngichi: Walivuka barabara

MALYA: kama walivuka barabara ulijuaje kama walikuwa wanafanya kampeni za nyumba kwa nyumba?

SSP Ngichi: Hazifanyiki barabarani

MALYA: Zinafanyika wapi?

SSP Ngichi: Nyumbani

MALYA: Ili ufike nyumbani unapita wapi?

SSP Ngichi: Barabarani

MALYA: Kwahiyo unakubali walikua wanavuka barabara ili wakafanye kampeni za nyumba kwa nyumba?

SSP Ngichi: Waliandamana

MALYA: Kwanini?

SSP Ngichi: Kwa sababu walikua na viongozi wao

MALYA: Wataje

SSP Ngichi: Heche, Matiko, Msigwa na wengine

MALYA: Unajua sifa za mtu kuwa wakala?

SSP Ngichi: Hapana

MALYA: Unajua Heche alikua Wakala?

SSP Ngichi: Sifahamu

MALYA: Unajua Matiko alikua wakala?

SSP Ngichi: Sifahamu

MALYA: Unajua Msigwa alikua Wakala?

SSP Ngichi: Sifahamu

MALYA: Je unakubali kwamba viongozi hao walikua wanaongozana na mawakala wenzao kwenda kwa Mkurugenzi kula kiapo?

SSP Ngichi: Kimya

Hawa jamaa watamuua huyu SSP NGICHIView attachment 1098288
Ukiumbwa kusifia ni shida sana. hayo nayo kweli maswali?
 
EINSTEIN112

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Messages
4,310
Points
2,000
EINSTEIN112

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2018
4,310 2,000
Anayeuliza anajua anaelekea wapi we kilaza huwezi elewa. Kumbuka maswali ya leo ni muendelezo wa mahojiano ya jana so usidhani hawajui wanachouliza.
Ukiumbwa kusifia ni shida sana. hayo nayo kweli maswali?
 
T

TANSIS

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2018
Messages
810
Points
1,000
T

TANSIS

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2018
810 1,000
acheni upopoma huyo shahidi ni mwanasheria mwenye degree zake msifikiri anavyokaa kimya au ambapo hajibu anajua kukwepa maswali ya mitego siyo kilaza kama mnavyomfikiria hata kama angekuwa huyo malya anaulizwa maswali ya kijinga hivyo mengine angekaa kimya kama hujui sheria utasema kachemka ila anaye jua sheria anajua anafanya nini hizo siyo story za kijiweni mkumbuke
 
Kaziutumishi

Kaziutumishi

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2018
Messages
248
Points
500
Kaziutumishi

Kaziutumishi

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2018
248 500
MALYA: Vituo vya kupiga kura vilikuwa vingapi?

SSP Ngichi: Sikumbuki idadi yake

MALYA: RCO unasimamiaje uchaguzi ambao hujui hata idadi ya vituo?

Ni sawa na kumtaka mwanafunzi (STD VII, F4, F6, UE nk.k) ajue wanafunzi wanaoganya mtihani ni wangapi.

"These qn even if are not answered, they do not go to the root of the case"
Sawa low iq troll
 
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2011
Messages
910
Points
500
Age
37
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2011
910 500
Anayeuliza anajua anaelekea wapi we kilaza huwezi elewa. Kumbuka maswali ya leo ni muendelezo wa mahojiano ya jana so usidhani hawajui wanachouliza.
Hahahahahahahaha! Kilaza alikuwa mpiga gitaa, Mimi ni Dunstan Buberwa nisiyeficha ID yangu hata siku moja. Tafuta ujue na ujilinganishe, utaelewa.
 
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Messages
11,215
Points
2,000
Tulimumu

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2013
11,215 2,000
Ngichi atapata presha jamani!
 
EINSTEIN112

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Messages
4,310
Points
2,000
EINSTEIN112

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2018
4,310 2,000
Hahahahahahahaha! Kilaza alikuwa mpiga gitaa, Mimi ni Dunstan Buberwa nisiyeficha ID yangu hata siku moja. Tafuta ujue na ujilinganishe, utaelewa.
bro nikikujua itasaidia nini? maana ni kama kwamba unataka kujilinganisha na mimi? well i'm no body so chambua mahojiano na kama hayana maana tusubiri rulling baada ya jaji kusikiliza pande zote mbili
 
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2011
Messages
910
Points
500
Age
37
B

BUBERWA D.

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2011
910 500
bro nikikujua itasaidia nini? maana ni kama kwamba unataka kujilinganisha na mimi? well i'm no body so chambua mahojiano na kama hayana maana tusubiri rulling baada ya jaji kusikiliza pande zote mbili
wala mie sitaki shali na wala sio utamaduni wangu. hayo ya kunibadilisha majina uliyatoa wapi? Nadhani jf na huu utaratibu wa kujibanza katika ID feki umeharibu utu, uungwana, upendo, nidhamu, ustaarabu, n.k Mie twaweza tofautiana kwa kila hoja ila katu sitakubandika majina ya dhihaka. Tuwe wavumilivu kila jambo jema na lisilo jema ulionalo ni zao la msuguano.
 
M

Maelau

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
1,091
Points
2,000
Age
45
M

Maelau

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2011
1,091 2,000
acheni upopoma huyo shahidi ni mwanasheria mwenye degree zake msifikiri anavyokaa kimya au ambapo hajibu anajua kukwepa maswali ya mitego siyo kilaza kama mnavyomfikiria hata kama angekuwa huyo malya anaulizwa maswali ya kijinga hivyo mengine angekaa kimya kama hujui sheria utasema kachemka ila anaye jua sheria anajua anafanya nini hizo siyo story za kijiweni mkumbuke
Usitutishe na degree bwana. Kuna wenye degree wangapi hawajui kuandika hata assignment au insha ya maana. Kazi ku plagiarize tu.
 
T

TANSIS

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2018
Messages
810
Points
1,000
T

TANSIS

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2018
810 1,000
Usitutishe na degree bwana. Kuna wenye degree wangapi hawajui kuandika hata assignment au insha ya maana. Kazi ku plagiarize tu.
sikutishi ila nakutaarifu tu kuwa huyo siyo popoma kama unavyozani anaakili zake na elimu ya sheria anaijua ndiyo maana pamoja na maswalio ya kijinga ya huyo wakili mjinga hapanic wala hapotezi point
 
E

ernieboss

Member
Joined
Sep 4, 2018
Messages
83
Points
150
E

ernieboss

Member
Joined Sep 4, 2018
83 150
Mawakili maswali yao ni lazima UJIPANGE maana ukienda kama umelishwa maneno utajuta
 
residentura

residentura

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Messages
1,228
Points
2,000
Age
29
residentura

residentura

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2017
1,228 2,000
Ngichi anadhihirisha jinsi gani upolisi hata usome vipi hauelimiki
Mkuu,huu unatakiwa ujue kutii amri tuu,ubongo wa kufikiri unauacha kwa baba na mama yako,hivyo hata wawe na makaratasi yanayoomfanya awe "dokta wa piihechidiii" ,kichwani ni zero.
 
M

mwalwebe

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2015
Messages
587
Points
1,000
M

mwalwebe

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2015
587 1,000
Wadau akina Okwibobanisunzu tu naomba mwendelezo wa mahojiano ya upunde wa mashahidi wa mashitaka na Mawakili wa utetezi.

Tuone hawa mashahidi wa kuchonga wanavyodhalilika,nitashukuru wadau kama mtatuwekea hii Leo nawasilisha.
 
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,086
Points
2,000
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,086 2,000
ngoja waje Ila naskia wakili Malya Leo amemnyamazisha kopro mmoja aliepotezaga fahamu Siku ya tukio 😂😂
 
Forum statistics

Threads 1,295,975
Members 498,495
Posts 31,229,603
Top