Kesi ya kina Mbowe kweli ni ya ugaidi ukweli?

Tangu kesi ya Mbowe na wenzake ianze nimekuwa nikiisoma kwa umbali na ukaribu.

Katika nyakati mbalimbali nimewahi zungumzia kuhusia UGAIDI hasa ule unaotendwa na Mamlaka au kusababishwa na Mamlaka ambao huwa unaitwa "STATIE SANCTIONED TERRORISM"

Kesi hii washtakiwa karibu wote ni MAKOMANDO" au Special Forces.

Kesi Hii washtaki wote ni kikundi maalum cha kipolisi (TASK FORCE) ambao wote kwa karibu wanaonekana kuwa wametesa na kuua watu wengi na kwamba hata hawa waliofikishwa mahakamani waliponea kwa neema za MUNGU.

Hii kesi ni kesi ya Magaidi na Magaidi wenyewe ni wale wa upande Mashtaka yaani wakina Kingai na Wenzake.

Haihitaji akili kubwa sana kuliona hili.Wao wanaweza wakafikiri wako katika jitihada za kutaka kuthibitisha UGAIDI wa kina MBOWE lakini kwa hakika wako katika JITIHADA za kujitetea.Kwa kiasi kikubwa hii staili ya KESI KUBWA NDANI YA KESI ndogo imethibitisha kabisa kwamba SASA Hawa askari POLISI ambao wanatokea kama mashahidi sasa Wao ndio watuhumiwa katika KESI hii.TUHUMA ZAO ni kesi za UGAIDI na UHUJUMU UCHUMI.

Niwapongeze jopo la mashahidi wakiongozwa na MSOMI KIBATALA kwa kuweza kuibadili hii kesi kutoka kuwa kesi ya kawaida na kuwa kesi ya kihistoria kwa kutumia akili ndogo sana.

Niwapongeze pia mawakili wa serikali kwa kukubali kucheza mziki wa upande wa utetezi kwani inawasaidia pia nyie kujua kwamba kuna mengi ambayo hayako sawa.

SASA hivi watanzania wanawajua watu wasiojulikana ambao walikuwa wanateka na kuwaua ndugu zetu kwa sababu tu ya tofauti za kisiasa na kimtazamo.SASA hata mimi najua kwamba huenda wakina BEN na AZORY walikuwa chini ya MIKONO ya kina MAHITA na wenzake na kwamba kwa kiasi kama wamekufa basi Muuaji wao ni kati ya HAO wawili.

Sasa hivi watanzania wanajua kwamba kuna uwezekano kwamba wale tulioaminishwa kwamba ni Magaidi waliokuwa KIBITI huenda walikuwa wanau askari kwa sababu ya kunyanyaswa nao hasa kwa kuzingatia mwenendo wa kesi hii.

Sasa hivi watanzania wanajua kwamba hata yule BWANA KADA GAIDI WA CCM ambaye aliwaua askari pale SURRENDER badala ya kusurrender huenda alikuwa ni muhanga wa matendo ya kishenzi ya jeshi la polisi ambayo huenda KINA GOODLUCK na MAHITA walikuwa na MKONO wao.

SASA hivi watanzania wanajua kwamba kODI zetu zionatumika kuwalipa watumishi wa umma ambao wanatumia mamlaka yao kutunyanyasa na kututesa bila SABABU.


ILA kuna JAMBO la kipekee zaidi linaenda kutokea.SASA hivi TANZANIA inaenda kupata MAGAIDI WA KWELI.

Wanajeshi ambao wakao katika KIKOSI MAALUM 92 KJ Morogoro cha SPECIAL FORCES sasa wanajuwa kwamba wao na wenzao ambao wako katika KESI hii wanaweza sasa kuonesha UGAIDI wa KWELI kwa kutumia MAFUNZO yao ya kipekee.

SASA hivi tumefungua PANDORA BOX na JINI ametoka na hakuna atakayeweza kumrudisha NDANI kwani TAYARI watu wenye uwezo wa kufadhili UGAIDI wanajua ni wapi watapata watu wenye Mafunzo ya kuweza kufanya UGAIDI wa kweli.

Ni maoni yangu,ni Mtazamo wangu na Ni fikra zangu.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Hakika umenena vema. NI AIBU iliyoje,Kwa jeshi la Polisi. Hivi mkituhumiwa mtakataa. Mtasema matumizi mabaya ya mtandao? Hivi Unaingia akilini,Askari walewale,as if hakuna aSkari WeNgINE ,,WAende Moshi wakamate,warusi WAende Tabora,warusi WAende Mwanza,,Kwa akili mdogo Tu,kwanini wao Tu? Kunanini? Hawa ninauhakika hawajatumika kiseeikali,hawa NI kikundi cha uhalifu kinachotumia mwavuli WA kipolisi. Nina Imani tusilitupie lawama Jeshi letu la Polisi. Tuzitupie lawama hiki kikundi.
 
Back
Top Bottom