Kesi Ya Kazi Mahakamani Miaka 15

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,939
Nimekutana na mzee mmoja sikukuu ya Pasaka akilalamika sana juu ya utendaji kazi wa mahakama zetu. Yeye na wenzake 9 waliachishwa kazi na Tanzania Breweries Mwaka 1993 na kufunguliwa mashtaka ya upotevu wa fedha na uzembe . Kesi hiyo imeendeshwa kwa mbinde mbinde hadi mwaka 2005 ilipoamuliwa kwamba hawana makosa na warudishwe kazini. Tanzania Breweries wakaamua kukata rufaa na hadi leo 2008 kesi hiyo inapigwa tu tarehe. In maana toka 1993 hadi leo ni miaka 15 kesi iko kwenye mzunguko wa hicho chombo cha haki. Kama angezaliwa mtoto bila shaka angekuwa kidato cha pili.

Mzee huyu analalamika kuwa wengine tayari wamefariki baada ya kuwa wanaenda Dodoma kila mwezi au kila inapopangiwa tarehe hadi leo. Licha ya kuwa hawana kazi na fedha bado wanatakiwa wahudhurie mahakamani kila mara kwa miaka 15. Hebu fikiria mtu anakaa Tanga ,au Dar .Hizo gharama ni mateso tu kama yale ya
Tabata Dampo.

Mimi binafsi nimeshindwa cha kumshauri maana kwa nyanja hizo mimi
sina light. Ila nimejiuliza maswali mengi sana hasa nikiangalia hali ya yule mzee amabaye anahisi TBL wanaihonga mahakama ili kesi hiyo isiendelee hadi wamekufa wote kwa sababu zao wenyewe.
Mbona kesi hata za mauaji hazichukui muda mrefu hivyo? Kesi ya Ditoplie ni mfano mmoja tu. Hii ya kazi ina nini zaidi?

Wana JF hebu saidieni hata mawazo tu. Kesi Yenyewe iko mahakama kuu Dodoma . Inawahusu waliokuwa wafanyakzi wa TBL Dodoma branch.Kama ni sahihi nitamwomba huyo mzee anipe namba ya kesi niiweke hapa.
Nadhani sio haki hata kidogo. Judiciary ,Lets be serious with peoples lives.??????
 
Mzee huyo anaitwa nani mbona ni kma familiar to that case
 
Back
Top Bottom